Iko hivi mkuu...
Hili zoezi lilifanyika katika setting ambayo ni kwamba fomu za NIDA tulichukulia mahali ambako ninafanyia kazi, na wafanyakazi wengi ambao hatuna hivyo vitambulisho tulichukua hizo fomu, tukazijaza vizuri kila sehemu inayotakiwa, including serikali za mitaa. Sasa, sehemu ya mwisho ilikua ni uhamiaji; Kwa hiyo nilienda uhamiaji, na
baada ya kutaja kabila langu la daraja la pili, nikakabidhiwa fomu nyingine yenye page 9 (sio fomu tisa), nijaze vitu kibao including walipozaliwa na kufia mababu na mabibi zangu; Ila sasa, wenzangu ninaofanya nao kazi ambao wao wanatoka makabila ya first class, walipofika na kuulizwa makabila yao, wakayataja, walisainiwa hizo fomu za NIDA haraka sana bila maswali ya ziada (within 15 minutes); Makabila ambayo nimeshuhudia kwa macho yangu wakisainiwa fomu za NIDA bila shida pale uhamiaji, wakati huo mimi najipinda kujaza zile page 9 ni pamoja na Wanyakyusa, Wasukuma na Wachaga. Hadi wafanyakazi wenzangu walinishangaa sana kunikuta pale najaza lile lifomu, hadi wengine wakaniuliza, mwenzetu vipi, ni kwamba ndo unaomba uraia wa Tanzania au?? Mbona sisi hatujasumbuliwa?? Nadhani sasa utakua umeelewa the basis ya my claims mkuu
Roman Israel Esq