Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,858
- 7,847
Siku chache zilizopita, ilinibidi kujongea katika ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kupata sahihi ya afisa ya uhamiaji katika fomu za kitambulisho cha utaifa (kwenye hizi fomu kuna sehemu ambayo inabidi isainiwe na uhamiaji).Kilichonikuta ndio kimenifanya niandike huu uzi.
Baada ya kufika ofisi husika na fomu zangu, swali la kwanza nililoulizwa ni, "wewe ni kabila gani"? Baada ya kumjibu yule mdada alieniuliza, kilichofuata alinikabidhi fomu nyingine ambayo ina page 9, iliyojaa maswali ambayo kiukweli yamejaa ukakasi sana;
Mfano: Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa baba (mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji), Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa mama
(mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji).
Mahali ambapo babu au bibi yako alifariki (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji), na maswali mengine mengi ya aina hiyo (imagine kujibu page 9 za maswali ya aina hiyo).
Lakini, kilichoni irritate zaidi, niligundua kwamba si waombaji wote wanajazishwa hii fomu (wengine wanasainiwa kirahisi kabisa bila kujaza chochote); na kinacho determine wakujazishe au wasikujazishe hilo lifomu ni *kabila* lako!! Kuna makabila fulani ukienda pale ukitaja, wanakusainia bila tashwishwi nyingi, ila kuna makabila mengine ndo process inakua ndefu mno (nimetumia muda wa siku mbili ofisi ya uhamiaji kukamilisha hilo,while my other colleagues spent hardly 15 minutes for a similar purpose!!).
Fikiria unamuona mtu mnaefanya nae kazi, yeye anakuja na fomu zake, anaulizwa kabila anataja kabila fulani, anaambiwa lete fomu zako, anasainiwa... Huku wewe umekaa pembeni unahangaika kujaza page 9 za maswali yanayotia ukakasi, hadi wenzako wanakushangaa kwani wewe vipi? Mbona sisi hatujasumbuliwa?
Siku ya kwanza, nimejaza hilo lifomu lao nikaambiwa niliache, nirudi next day saa tatu asubuhi (hapo nilitumia masaa 6 ofisi za uhamiaji).
Nimerudi siku ya pili, nikaambiwa subiri, baada kama ya nusu saa yule mdada akatoka. Nilisubiri kwa zaidi ya masaa sita tena, ambapo ndipo niliweza kukamilisha mchakato huo na wakanisainia fomu yangu hatimaye (namshukuru sana yule kijana alienihudumia siku ya pili, alikua ni mstaarabu na mnyenyekevu sana na hata yeye alionyesha kushangazwa kwa nini nimezungushwa vile).
Nimesikitika sana, kwamba kumbe sisi makabila mengine ni second grade citizens ndani ya nchi yetu!!
Kwa nini kuwe na preferential treatment (huduma tofauti) kwa raia wanaohitaji huduma ya uhamiaji, ambayo iko based kulingana na kabila??