Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Na kweli,bora wangeweka wazi kabisa hayo makabila ambayo yanahitaji mchakato mrefu zaidi wa kuhakiki uraia wao.
Lakini, hilo jambo haliwekwi wazi sana kwa sababu na wao wanajua imekaa kibaguzi baguzi sana!! Na pia sio utaratibu ambao uko rasmi sana (kwa nilivyogundua);maana kuna jamaa yangu ainiambia kuwa pia na yeye alipewa hilo lifomu, ila kabla hajaanza kujaza, akatokea mtu anaefanya ofisi hiyo ambae anafahamiana nae akamnyang'anya hilo lifomu, akamwambia achana nalo usilijaze... Na akasainiwa vizuri tu fomu zake za NIDA, akasepa!! bbade
Kujuana ndio kunakosaidia tu harafu jmn unapoenda kweny hizo ofis za serkal usiavae kishamba piga mapigo ya kisasa na kimjini hamna atakaepoteza mda wake kukuuliza vimaswaki vya kijinga.
 
Kujuana ndio kunakosaidia tu harafu jmn unapoenda kweny hizo ofis za serkal usiavae kishamba piga mapigo ya kisasa na kimjini hamna atakaepoteza mda wake kukuuliza vimaswaki vya kijinga.
Nilivaa kikawaida tuu mkuu... Maana ilikua siku ya kazi, kwa hiyo nilikua nimetokea kazini ndo nikapotezea siku nzima huko!!
Bujoro
 
Uhamiaji ukiwa msukumaunasaidiwa mapema sana. Au kama ukimfahamu msukuma aliyemo humo ambao nafikiri ni wengi sana humo uhamiaji. Dar pale pia.
 
mbona ujasema we ni kabila gani?
kuna makabila mengine ya mipakani yanaingiliana na chi jirani{yani yapo kote)
 
Ndo ujue kwamba Tanzania Muhindi, Mwarabu au Mchotara ana haki kuliko wewe na hii ni kwa mujibu wa Sheria zetu, Muhindi akienda kuomba hati ya kusafiria anapewa fasta kwani ana makaratasi yaliyonyooka kuliko wewe, kwa kifupi Muhindi aliyezaliwa Tanzania/Tanganyika ni Mtanzania kuliko wewe mweusi hata kama wengi hamtalikubali hili!

Hakuna Muhindi/Mwarabu/Mchotara ataambiwa athibitishe Babu au sijui Bibi alizikwa wapi, hawa kila kitu kiko documented, anahitaji kutoa makaratasi tu!

Welcome to the second class citizen of JMTZ!
Uko sahihi mkuu huku ni kunyanyasana kishamba wakat wote ni watz
 
mbona ujasema we ni kabila gani?
kuna makabila mengine ya mipakani yanaingiliana na chi jirani{yani yapo kote)
Wasukuma, Wanyakyusa na Wachagga (a few examples) wao hawapo mipakani??
Hayo makabila matatu niliyokutajia kama mifano, wapo mipakani, ila wao wala hawapati shida yoyote kwenye hizo process, ni fasta tuu!!
Labda ufafanue ni mipaka gani unayomaanisha??
casanova69
 
Siku chache zilizopita, ilinibidi kujongea katika ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kupata sahihi ya afisa ya uhamiaji katika fomu za kitambulisho cha utaifa (kwenye hizi fomu kuna sehemu ambayo inabidi isainiwe na uhamiaji).Kilichonikuta ndio kimenifanya niandike huu uzi.
Baada ya kufika ofisi husika na fomu zangu, swali la kwanza nililoulizwa ni, "wewe ni kabila gani"? Baada ya kumjibu yule mdada alieniuliza, kilichofuata alinikabidhi fomu nyingine ambayo ina page 9, iliyojaa maswali ambayo kiukweli yamejaa ukakasi sana; Mfano: Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa baba (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji), Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa mama (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji). Mahali ambapo babu au bibi yako alifariki (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji), na maswali mengine mengi ya aina hiyo (imagine kujibu page 9 za maswali ya aina hiyo).

Lakini, kilichoni irritate zaidi, niligundua kwamba si waombaji wote wanajazishwa hii fomu (wengine wanasainiwa kirahisi kabisa bila kujaza chochote); na kinacho determine wakujazishe au wasikujazishe hilo lifomu ni *kabila* lako!! Kuna makabila fulani ukienda pale ukitaja, wanakusainia bila tashwishwi nyingi, ila kuna makabila mengine ndo process inakua ndefu mno (nimetumia muda wa siku mbili ofisi ya uhamiaji kukamilisha hilo,while my other colleagues spent hardly 15 minutes for a similar purpose!!). Fikiria unamuona mtu mnaefanya nae kazi, yeye anakuja na fomu zake, anaulizwa kabila anataja kabila fulani, anaambiwa lete fomu zako, anasainiwa... Huku wewe umekaa pembeni unahangaika kujaza page 9 za maswali yanayotia ukakasi, hadi wenzako wanakushangaa kwani wewe vipi? Mbona sisi hatujasumbuliwa?
Siku ya kwanza, nimejaza hilo lifomu lao nikaambiwa niliache, nirudi next day saa tatu asubuhi (hapo nilitumia masaa 6 ofisi za uhamiaji). Nimerudi siku ya pili, nikaambiwa subiri, baada kama ya nusu saa yule mdada akatoka. Nilisubiri kwa zaidi ya masaa sita tena, ambapo ndipo niliweza kukamilisha mchakato huo na wakanisainia fomu yangu hatimaye (namshukuru sana yule kijana alienihudumia siku ya pili, alikua ni mstaarabu na mnyenyekevu sana na hata yeye alionyesha kushangazwa kwa nini nimezungushwa vile).
Nimesikitika sana, kwamba kumbe sisi makabila mengine ni second grade citizens ndani ya nchi yetu!!
Kwa nini kuwe na preferential treatment (huduma tofauti) kwa raia wanaohitaji huduma ya uhamiaji, ambayo iko based kulingana na kabila??

Form si unajaza online hizo form za mkono mmh
 
Form si unajaza online hizo form za mkono mmh
Fomu zipi hizo mkuu za kujaza online?
Nahisi umechanganya madesa.
Fomu za vitambulisho vya uraia haujazi online, ni hard copies. Pia, hizo fomu za kibaguzi za kuulizana makaburi ya mababu na mabibi (zina page 9), na zenyewe sio za online, ni hard copies hizo ndo ukiwa 2nd grade citizen (baadhi ya makabila), ndo unapewa ujaze kwanza halafu ndo waamue (uhamiaji) kama wakusainie au wasikusainie fomu za NIDA.
SIERA
 
Wasukuma, Wanyakyusa na Wachagga (a few examples) wao hawapo mipakani??
Hayo makabila matatu niliyokutajia kama mifano, wapo mipakani, ila wao wala hawapati shida yoyote kwenye hizo process, ni fasta tuu!!
Labda ufafanue ni mipaka gani unayomaanisha??
casanova69
Tena wasukuma wana muingiliano mkubwa sana na wanyakyusa sema watu wakigoma kagera ndo wanapaa shida
 
Nimefatilia kitambulisho tangu 2016 ndo juzi nimekipata kwahivo endelea kuwa mvumilivu
 
Tena wasukuma wana muingiliano mkubwa sana na wanyakyusa sema watu wakigoma kagera ndo wanapaa shida
Exactly on point!!
Nawashangaa sana wanaoleta point ya 'makabila ya mipakani'.
Wanyakyusa ni kati ya makabila ambayo yana muingiliano mkubwa sana na nchi za jirani (Malawi na Zambia); Tukubaliane tu kwamba kabila kuwa mpakani wala si hoja ya huu ubaguzi unaofanywa na uhamiaji, maana hiyo ingekua ni hoja, Wanyakyusa wala wasingepona!! Vivyo hivyo kwa Wachagga na hata wasukuma!!
Watafute hoja nyingine!!
cariha
 
Back
Top Bottom