Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Ni sisi waha pekee na wahangaza tunaobaguliwa na uhamiaji. Hata usipotaja, wewe ni muha tu.

Watuoneshe nchi yetu twende
 
Makabila ya mipakani lazima kwa sababu ukishapata pasport yetu wewe ni mtanzania hata kama ni mrundi
Unaona sasa! Kwa nini utaje muha na si mhaya, mkurya, mmasai, mnyakyusa, makonde, mfipa, mndali, msambaa, mjaluo na wengine ili hali nao wapo mipakani?

Kwa nini burundi na rwanda inaogopwa na tanzania, na kwa nini mha na mhangazwa tunapachikwa uraia wa rwanda na burundi?
 
Ndo ujue kwamba Tanzania Muhindi, Mwarabu au Mchotara ana haki kuliko wewe mweusi na hii ni kwa mujibu wa Sheria zetu, Muhindi akienda kuomba hati ya kusafiria anapewa fasta kwani ana makaratasi yaliyonyooka kuliko wewe, kwa kifupi Muhindi aliyezaliwa Tanzania/Tanganyika ni Mtanzania kuliko wewe mweusi hata kama wengi hamtalikubali hili!

Hakuna Muhindi/Mwarabu/Mchotara ataambiwa athibitishe Babu au sijui Bibi alizikwa wapi, hawa kila kitu kiko documented, anahitaji kutoa makaratasi tu, mfumo uliopo unampendelea Muhindi/Mwarabu/Mchotara moja kwa moja zaidi yako wewe uliyezaliwa Biharamuro au sijui Mpwapwa, tumerithi huo mfumo kutoka kwa Muzungu kwamba sisi ni raia daraja la 3 baada ya Muzungu, Muhindi/Mwarabu/Mchotara.

Welcome to the second class citizen of JMTZ!
 
Ni sisi waha pekee na wahangaza tunaobaguliwa na uhamiaji. Hata usipotaja, wewe ni muha tu.

Watuoneshe nchi yetu twende
Kiukweli kabisa mkuu, mimi sio muha wala mhangaza!!
Ila ubaguzi huu unaofanywa na uhamiaji ni lazima tuupigie kelele kwa kweli. Haukubaliki!! ntamaholo
 
Makabila ya mipakani lazima kwa sababu ukishapata pasport yetu wewe ni mtanzania hata kama ni mrundi
Makabila ya mipakani ni yapi??
Wasukuma hawapo mpakani?
Wanyakyusa hawapo mpakani?
Wachagga hawapo mpakani?
Makabila yote hayo matatu hapo juu, nimeshuhudia wanasainiwa bila kujazishwa hilo lifomu lenye maswali ya kipumbavu.
Kwa hoja hiyo, sidhani kwamba hoja ni makabila ya mipakani. Jini Kisiranii
 
Ndo ujue kwamba Tanzania Muhindi, Mwarabu au Mchotara ana haki kuliko wewe na hii ni kwa mujibu wa Sheria zetu, Muhindi akienda kuomba hati ya kusafiria anapewa fasta kwani ana makaratasi yaliyonyooka kuliko wewe, kwa kifupi Muhindi aliyezaliwa Tanzania/Tanganyika ni Mtanzania kuliko wewe mweusi hata kama wengi hamtalikubali hili!

Hakuna Muhindi/Mwarabu/Mchotara ataambiwa athibitishe Babu au sijui Bibi alizikwa wapi, hawa kila kitu kiko documented, anahitaji kutoa makaratasi tu!

Welcome to the second class citizen of JMTZ!
Thank you very much madam!! Barbarosa
 
Kwanza ungetueleza were ni kabila gani kuna makabila yako Tanzania na nchi Jirani pia kuna wale wa mipakani lazima kuwepo na umakini wa hali ya juu
 
Mwaka juzi walisababisha niahirishe zoezi la kitambulisho cha taifa, nimeenda pale wanigongee muhuri waniambia nilete uthibitisho wa mzazi wangu kwamba ni mtanzania, nikawaambia hii passport hapa ambayo nyie wenyewe mmeitoa inasema mie raia wa wapi?
Niliishia kuahirisha zoezi.

Mwaka huu baada ya kuona siwezi kurenew passport bila kitambulisho nikaenda tena, wakaniletea habari zile zile, nashukuru kuna jamaa muelewa nilipompa kesi yangu alinipeleka sehem wakaniuliza maswali mawili matatu wakanigongea muhuri.
Pole sana mkuu. Kuna mambo yanasikitisha sana kwa kweli.
Wakati wa huu mchakato kwenye hizo siku mbili, at one point i thought of kuchukua uraia wa nchi jirani.
Very disappointing.
The Monk
 
Ndo ujue kwamba Tanzania Muhindi, Mwarabu au Mchotara ana haki kuliko wewe na hii ni kwa mujibu wa Sheria zetu, Muhindi akienda kuomba hati ya kusafiria anapewa fasta kwani ana makaratasi yaliyonyooka kuliko wewe, kwa kifupi Muhindi aliyezaliwa Tanzania/Tanganyika ni Mtanzania kuliko wewe mweusi hata kama wengi hamtalikubali hili!

Hakuna Muhindi/Mwarabu/Mchotara ataambiwa athibitishe Babu au sijui Bibi alizikwa wapi, hawa kila kitu kiko documented, anahitaji kutoa makaratasi tu!

Welcome to the second class citizen of JMTZ!
Hayo yote ni matokeo ya CCM iliyojaa laana na ufisadi
 
Kwanza ungetueleza were ni kabila gani kuna makabila yako Tanzania na nchi Jirani pia kuna wale wa mipakani lazima kuwepo na umakini wa hali ya juu
Nikikwambia kwamba kuna baadhi ya watu ambao makabila yao ni ya mipakani kama Wasukuma, Wachagga, na Wanyakyusa ambao nilishuhudia wakisainiwa fomu zao za NIDA bila shida yoyote mara tu baada ya kuulizwa makabila yao na kutaja kuwa wao ni Wasukuma, Wachagga au Wanyakyusa (nimeona hili kwa macho yangu mawili nikiwa pale uhamiaji). Sasa sijui mipaka gani unayoizungumzia ndugu yangu.
rodrick alexander
 
Back
Top Bottom