Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Hao unaosema ni wamalawi na wakiongea wanasikilizana na wanyakyusa, hilo ni sahihi. Lakini je hayo maeneo yana shida na uhamiaji haramu? Wenzetu wanasema "if it ain't broken, why fix it"?

Mimi nakushangaa wewe kuushangaa mfano wangu wa kuhusu "wanyarwanda kujiita wanyakyusa", huo ulikuwa ni mfano tu, ningeweza kusema "wahutu kujiita waha", lakini cha msingi ni wewe na members wengine kuupata ujumbe uliokusudiwa. Hapo kushangaa kwako umepoteza nguvu za bure tu kusema ukweli.

Wataita pia nawafahamu sana. Wapare asili yao ndipo wanapodaiwa kutokea asili yao. Na wengine wanasema wachagga pia.

Nakubaliana kabisa na hoja ya kwamba kuna shida kwenye maeneo ya mipakani, lakini siyo mipaka yote yenye shida za wahamiaji haramu. Sasa kule uchaggani mhamiaji hata hiyo ardhi ataipata wapi? Kuna maeneo yenye makabila flani flani ambayo yana issue sugu sana kuhusiana na uhamiaji haramu. Kuwa kabila la mpakani peke yake siyo sababu. Kuna "Other factors"
Kwa hiyo una declare maeneo ya Mbeya hayana shida ya wahamiaji haramu? Unaifahamu Tunduma? Hebu ona hoja yangu hapa. Kwa mfano, Mmalawi akajiita mnyakyusa na kwa sababu idara yetu ya uhamiaji inawachukulia wanyakyusa kama 1st grade citizens, wasimfanyie verification na wakampatia go ahead ya kwenda kupata kitambulisho cha utaifa NIDA, hapo hauoni tatizo?? Kwamba hakuna Wamalawi ambao wanajichanganya na Watanzania na kutamani Utanzania kwa njia ambazo si halali?
Ninachokiona mkuu, ni ku regard makabila fulani kuwa wao ndio 1st grade citizens, na makabila mengine hayo uliyosema yana "other factors" kuwa treat as if ni 2nd grade. Kwani hiyo verification ingefanyika kwa kila mtu kungekua na hasara gani? Ambacho sikubaliani nacho mimi, ni kum label kila Mnyakyusa (kwa mfano) kama Mtanzania halisia, na "muha" kwamba ni Mtanzania anaehitaji verification (kutumia makabila kama basis ya kwamba verification ifanyike au isifanyike) Roman Israel Esq
 
Mkuu makabila ya mipakani lazima verification iwe tight ukilinganisha na makabila kama wazaramo, watengereko, nk. Sasa kama walikubagua wewe mzaramo then itakuwa kuna shinda lakini kama unatoka mipaka ya magharibi kweli ni lazima wakufanyie tight verification kutokana na background ya mipaka hiyo!
Background ipi hiyo mkuu ambayo watu wa mipaka ya magharibi wanayo ambayo ni tofauti na, kwa mfano watu wa mipaka ya nyanda za juu kusini? UCD
 
Huwezi kuwa na fomu tofauti kwa watu nchi hiyo hiyo moja.
Kuna walakini mahali.
Kwa anayetakiwa deep verification lazima atoe taarifa zaidi. Same when you visit some countries kama unatoka kwenye nchi zinazotakiwa more info lazima utoe more info. Hivyo hata hata TZ kama unatoka sehemu ambako kuna tatizo la uhamiaji haramu then ni muhimu deep verification lazima ifanywe kwa mhitaji kutoa taarifa zaidi. Mimi sioni shida pia itafundisha vijana kujua historia yako siyo kujua mambo mengine tu wakati hata ukoo wako huujui!!!
 
Hayo makabila ie wanyakyusa na wachagga, ni shida kuwa na mapandikizi au wahamiaji haramu,halafu wakadai wametokea hayo makabila na wasigundulike.

Pia hata kama uki fake, ukajidai wewe ni mojawapo ya hayo makabila, sidhani kama ukisema wewe ni mnyakyusa, halafu una lafudhi ya kinyarwanda utaeleweka, utapa shida hapo pia.

Pia kuna makabila ambayo yako pande mbili za mipaka. Mfano huko Kigoma kwa wahutu, pia kuna wacongo nk. Huwezi kukuta mchagga wa Kenya. Hata kama wale wataita wana asili hiyo lakini utofauti upo. Kwingine ni shida sana. Mhutu anaweza kujipakazia kuwa ni mha nk.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya waha,warundi na wanyarwanda. Ni rahisi sana kwa mnyarwanda kumwelewa mrundi kuliko hao wawili kumwelewa muha. Matamshi, maandishi na rafudhi ya kiha ni tofauti sana na hayo mawili.. Hii ndio sababu inayomfanya mrundi au mnyarwanda asiweze kujificha miongoni mwa waha kwa sababu ni watu kutoka koo mbali mbali ... inahitaji kazi ya ziada kuwapambanua hawa, hii ndio kazi wanayoifanya uhamiaji kwa sasa.
 
Kwa anayetakiwa deep verification lazima atoe taarifa zaidi. Same when you visit some countries kama unatoka kwenye nchi zinazotakiwa more info lazima utoe more info. Hivyo hata hata TZ kama unatoka sehemu ambako kuna tatizo la uhamiaji haramu then ni muhimu deep verification lazima ifanywe kwa mhitaji kutoa taarifa zaidi. Mimi sioni shida pia itafundisha vijana kujua historia yako siyo kujua mambo mengine tu wakati hata ukoo wako huujui!!!
Makabila kama Wanyakyusa, wachagga, wasukuma wao vijana wao hawatakiwi kujua ukoo wao? Unaijua Tunduma? Haina tatizo la wahamiaji haramu? UCD
 
Sasa mtu kama mjaluo, mngara, ulitaka tusiwe na haja ya kuwajazisha hilo liform kweli, lazima utajazishwa tu, hamna namna
 
Background ipi hiyo mkuu ambayo watu wa mipaka ya magharibi wanayo ambayo ni tofauti na, kwa mfano watu wa mipaka ya nyanda za juu kusini? UCD
Tunajua Rwanda, Burundi na DRC kumekuwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha wakimbi wengi magharibi ya TZ na hao wakimbizi mara nyingi wamekuwa kukijihalalisha kuwa ni watz wakati si kweli na kuleta matatizo kwenye nchi husika angalia Banyamrenge wanavyowasumbua DRC wale ni wakimbizi toka Rwanda toka enzi ya 70's leo wanasumbua DRC. Hivyo TZ lazima tujifunze toka kwa wenzetu wa DRC.
 
Hakuna kitu kitakacho justify unachojaribu kusema.
Kwa hiyo msukuma yeye ni Mtanzania zaidi kuliko mrangi kwa mfano??
Kuna shida katika hilo.
Halafu, hivi mtu ambae ana proof ya kuzaliwa Tanzania, ana proof ya kusoma Tanzania kuanzia primary hadi chuo kkkuu ana proof ya kuajiriwa ndani ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 7; halafu una wasiwasi nae?? Kama utatilia mashaka Utanzania wa mtu wa aina hii, that speaks more of the weakness of immigration department than the legality of citizenship of that person!! FRESHMAN
Kwani Warangi wako mpakani?
 
Makabila kama Wanyakyusa, wachagga, wasukuma wao vijana wao hawatakiwi kujua ukoo wao? Unaijua Tunduma? Haina tatizo la wahamiaji haramu? UCD
Hata kama wapo huko lakini si wasumbufu kama Banyaburenge! Waulize DRC watakueleza!
 
Makabila ya Dodoma yana muingiliano gani na nchi jirani?
Kati ya makabila ya Dodoma na Wasukuma kwa mfano, wapi wana muingiliano sana na nchi jirani?
Mkimbizi anazaliwa nchini kwako, anasoma nchini kwako, anafanya kazi nchini kwako kote huko akijitambulisha kama raia wa Tanzania (for more than 30yrs). Hapo nani atakua na shida?? Yeye mkimbizi au idara ya nchi yenu ya uhamiaji??
ubongokid
Hoja yako ya ukabira haina mashiko jaza form hizo sioni Shida nahasa ukiwa raia utajua kweli uhamiaji wako makini ,Shida yako moja hutaki kuamini kana kwamba wakimbizi ha wapo,hivyo jaza hiyo form tatizo haripo ni utaratibu wa kawaida acha kuriaria bira sababu.
 
Dar ndiyo nini ,ukizariwa dar unataka uwe unapigiwa makofi sijakuelewa,fuata utaratibu.
Hahahahahahahaha!! umenichekesha mkuu.
Nitafuatilia hilo la muonekano. By the way, mimi nimezaliwa Dar es Salaam, nimekulia Dar es Salaam,mambo ya makabila kwangu ni none issues!! Last time nimefika kijijini alikozaliwa mzee it was back in early 2000s.
Mtoto wangu ni mchanganyiko wa makabila mannne, hata ukimuuliza yeye ni kabila gani kwa kweli atabaki anakushangaa tuu!!
Anyways, to each its own!!!
ubongokid
 
Hoja yako ya ukabira haina mashiko jaza form hizo sioni Shida nahasa ukiwa raia utajua kweli uhamiaji wako makini ,Shida yako moja hutaki kuamini kana kwamba wakimbizi ha wapo,hivyo jaza hiyo form tatizo haripo ni utaratibu wa kawaida acha kuriaria bira sababu.
Jifunze kuandika kwanza mkuu.
Nina wasiwasi kama umeweza kusoma na kuelewa nilichoandika, maana hata kuandika tu ni tatizo.
Sina shida na kujaza fomu. Shida yangu ipo kwenye criteria ya kujaza hizo fomu, kwamba kuna watu wa makabila fulani fulani tu ndo wanaambiwa wajaze, ila makabila mengine wao wala hawaambiwi wajaze hizo fomu; na hakuna ambae atakupa jibu la kueleweka kwamba kwa nini makabila fulani tu? nyamatala.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya waha,warundi na wanyarwanda. Ni rahisi sana kwa mnyarwanda kumwelewa mrundi kuliko hao wawili kumwelewa muha. Matamshi, maandishi na rafudhi ya kiha ni tofauti sana na hayo mawili.. Hii ndio sababu inayomfanya mrundi au mnyarwanda asiweze kujificha miongoni mwa waha kwa sababu ni watu kutoka koo mbali mbali ... inahitaji kazi ya ziada kuwapambanua hawa, hii ndio kazi wanayoifanya uhamiaji kwa sasa.
Nadhani umenielewa zaidi mkuu. Na mimi nimekuelewa vilevile. Ni matarajio yangu kuwa ndugu mwanzisha thread na yeye ataelewa mwishowe.
 
Back
Top Bottom