Unawezaje kumwambia mtu ananuka?

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
Je unawezaje kumwambia mtu 'ananuka 'katika lugha ya kistarabu? iwe ni pafyume mbaya, kikwapa , 'mdomo' nk? Kwa watu wa kupita tu(say kwenye daladala) pengine ni rahisi tu kuvumiulia kwa dakika mbili au tatu, lakini kwa mtu ambaye uponaye karibu kwa muda mrefu (say manafanya kazi wote) inakuwa ngumu kweli.

Niliwahi kupata mgeni, ambaye alikuja mjini na ilibidi nimpe hifadhi nyumbani kwangu kwa takribani miezi miwili. Huyo mgeni alikuwa ana tatizo la kutoa harufu mbaya. Yaani kama alikuwa nje halafu akaingia sebuleni, harufu mbaya itasambaa sebule nzima. Nilipofanya uchunguzi nikagundua kwamba huwa haogi, pamoja na kumkarimu bafu zuri la kuoga likiwa na maji massa 24. Hali hii ilikuwa inaniboa sana lakini tatizo langu ilikuwa ni jinsi gani ninaweza kumweleza bila kumfanya ajisikie vibaya.
 
Kama uko nae karibu unaweza kumpa vishawishi kama ni perfume basi uwe na suggestion nzuri ya perfume kwa ajili yake unajaribu kumpulizia unamwambia unaona hii inakuvutia sana mambo kama hayo na mtu anayetoa harufu anajijua so atajua unamwambia nini
 
Vipi mzee hujaoga leo? maana nasikia kwa mbali kaperfume kanaleta leta. Unafanya kama utani vile lakini ujumbe umefika :)
 
Aisee hili ni jambo sensitive sana. Fikiria wewe ndio unaambiwa unanuka....utajisikiaje?
 
Aisee hili ni jambo sensitive sana. Fikiria wewe ndio unaambiwa unanuka....utajisikiaje?
Inauma kishenzi........kuna kunuka sehemu za mwili ambazo ni dhalili(za kudhalilisha) mfano akuambia unanuka sehemu za siri lina uzito kuliko ukiambia unanuka miguu(labda shauri ya soksi).
Wavuta sigara na wanywa pombe ni rahisi kumwambia anatema mdomo kuliko kumwambia mtu ananuka kikwapa!

Hapo kwanza lazima uangalia ni mtu wa namna gani kwako unamuambia.
 
Aisee hili ni jambo sensitive sana. Fikiria wewe ndio unaambiwa unanuka....utajisikiaje?

Hamna kitu kinaochoitwa sensitive katika hili swala, wewe mpe tuu kiaina aina kama alivyosema BAK. Hata akikasirika utakuwa umemsaidia tayari. So weka haya pembeni na msaidie mwenzako.
 
Unambia kabisa..kama kuna wengine wanapiga mswaki wanasau ulimi ambao ni kiungo muhimu..sasa huyo unaweza mwambia kabisa wazi wazi kabisa hivi kuliko kujifikiria sana.
 
Hamna kitu kinaochoitwa sensitive katika hili swala, wewe mpe tuu kiaina aina kama alivyosema BAK. Hata akikasirika utakuwa umemsaidia tayari. So weka haya pembeni na msaidie mwenzako.

Ndugu yangu you need to have tact. Huwezi tu kuropoka eti unanuka. Utaumiza hisia za mwenzako bure. Inabidi kuwa mwangalifu sana na mambo haya kwa sababu unaweza kumsababishia maumivu mtu kuliko unavyodhani umemsaidia.
 
Muelezee faida za usafi na kama ni mgeni ni lazima atambue utaratibu wa nyumbani kwako mojawapo likiwa ni usafi . Unachotakiwa unatakiwa umhit indirect asijue unamaanisha nini kama kuna housegirl unamuassign awe anamuandalia maji ya kuoga atleast atambue kuwa anahitaji nini. Hizo zikishindikana mueleze ukweli lakini sio kumwambia ananuka.
 
Unajua suala kubwa hapa ni kuwa muwazi katika kumueleza mtu ukweli kuliko kuzungusha maongezi. Kama kweli huyo mtu ni mtu uliyekaribu nae na mnaheshimiana unatakiwa kutumia lugha ya kiungwana kumwambia kuwa ananuka so ni budi azingatie usafi. Kwa mfano mtu mvivu kuoga, au hasafishi mdomo/kinywa chake vizuri, miguu na soksi zake zinatoa harufu mbaya unamwambia tu kuwa ndugu yangu unahitaji kuzingatia usafi wa mwili na mavazi yako mzee maana hali ya hewa inakuwa mbaya.

Kuna wengine anaweza kujisikia vibaya lakini akajisafisha na pia kuna wengine hawaoni kuwa hilo ni tatizo kwa hiyo ataishia kukulalamikia kwa watu kuwa unamuona mchafu but mwisho wa siku utakuwa umefikisha ujumbe kwa mlengwa!!!
 
Inategemea kama huwa hapendi kuoga wewe mwambie tu ukweli ndugu vipi umeoga leo, kama huwa hapigi mswaki, mwambie nasikia kama kuna mtu hajapiga mswaki vile yeye mwenyewe atajihisi tu na ataenda kuswaki, kama ananuka kikwapa mnunulie DEODORANT mpe kama zawadi mwenyewe atajishitukia.
 
Hii si kitu rahisi. Uwezekano wa kumwambia mtu unategemea jinsi ulivyomzoea. Binafsi nimepata tatizo sana na watu wanaotoa harufu mdomoni (kwa kizungu "halitosis") au ya mwili ikiwa ni pamoja na matumizi ya manukato. Kama mtu nimemzoea namwambia moja kwa moja na kumpa ushauri. Ila kama hujamzoea inakuwa taabu sana.

Lakini kwa mtu ambaye atakaa kwangu mwezi mzima, nitamwambia tu. Kwani muda huo ni mrefu sana kiasi kwamba kujaribu kuvumilia ni kujipa mateso makubwa sana na yasiyo ya lazima. Hata hivyo ni muhimu kujaribu kumweleza kwa njia ambayo haitamuumiza. Na kama ni vijana vijana kama wale wanaokuja likizo (kupumzika kwa baba mdogo au mjomba) ni kuwambia moja kwa moja tu. Tuna tatizo kwamba vijana wetu (hasa wa kiume) hawaelezwi na wazazi au walimu wao umuhimu wa kuoga, kufua chupi, kujipima kama wanatoa harufu mdomoni n.k. Hawa unawapiga shule tu na kwa uzoefu wangu huwa wanapokea vizuri na kushukuru. Lakini kama ni mtu mzima na anakaa kwako siku 2-3, na hujamzoea, pia anaonekeana si mtu anaweza kupokea ushauri wa kitu kisichofurahisha; basi unaweza kuacha naye. Hapo itakubidi ukachukue tahadhari ya kupunguza harufu ndani ya nyumba kwa kutumia dawa (deodorants) na kuhakikisha kuna mzuguko mzuri wa hewa.
 
umegusia swala moja ambalo wengi wanasahau kabisa- matumizi ya manukato, kuna wale wanaotumia mipa fyumu gani sijui, halafu wanapuliza nyiingi, basi wakikupitia karibu kichwa kinauma
 
Last edited:
Hii issue ilishawahi kunitokea miaka kadhaa iliyopita, nilipata demu bomba ile mbaya alikuwa akiishi apartment complex moja na brother yangu. Safari zikaongezeka kumtembelea bro maake hatukuwa tukiishi mbali sana, nikafanikiwa kumpata yule mtoto, siku ya siku nilipompeleka maskani baada ya mamboz huko ndani kukawa hakukaliki harufu mtindo mmoja. Nikausugua, siku nyingine nikaenda kumchukua, mambo yakawa vile vile, nikajisemea kimoyomoyo kwamba huyu demu simleti tena maskani kwangu maake anaharibu mazingira. Nikapotea kwako muda hivi, akagundua kwamba namkwepa, siku kaibuka nyumbani baada ya story nikampeleka nyumba ya kulala wageni tukafanya mambo yetu akarudi kwao, siku nyingine hivyo hivyo, akawa anashangaa kwa nini nampeleka guesthouse. Hapo ndo nikamtolea uvivu, nikamwambia njoo kesho maskani, kweli kaja kama kawa nikamuuliza tukifanya mamboz huwa unasikia nini? nikamuuliza, kanambia hakuna kwani nini, nikamweleza kuwa kuna kuwa na harufu inayonifanya nishindwe kuvumilia ndo sababu nakupeleka motel, jibu alilonipa ni kwamba nashukuru kisha akaondoka. Baada kama mwezi hivi karudi kanishukuru, alimpa story shangaziye ndo kampeleka kwa wamasai kariakoo, Baada ya hapo ile harufu ikapotea kabisa. Ushauri wangu ni kwamba kama mtu mpo karibu siyo vibaya ukatafuta muda muafaka wa kumweleza!!
 
tafakari neno kabla hujalitamka. Utapotamka, jisikize hilo neno weye ungelipokeaje.

...some people can tell you Go to hell!...so diplomatically that you really look forward for that trip!

...there is always a way to convince someone to be hygienical without offending or hurting her/his feelings.
 
Nadhani binadamu huwa hanuki hata siku moja ila labda hiyo siku awe ametembea sana ametokwa na jasho ndio itakuwa hivyo.....Lakini huwezi kumwambia binadamu mwenzako ananuka na kuna washenzi wa tabia wanajifanya wanajuwa kuongea sana mungu yupo maana kuna mahali nimeona kuna mtu kamwita mwezie etii wewe unanuka kweli ni sahihi kumuita binadamu mwenzako ananuka hata kama hamuelewani???Kuna msemo unasema kwamba hujafa hujaumbika nadhani mwenyezi mungu analipa hapa hapa duniani!!!
 
tafakari neno kabla hujalitamka. Utapotamka, jisikize hilo neno weye ungelipokeaje.

...some people can tell you Go to hell!...so diplomatically that you really look forward for that trip!

...there is always a way to convince someone to be hygienical without offending or hurting her/his feelings.

Daaa kwa kweli mkuu ulivyosema ni sawa kabisa yaani maana sio vizuri kumuita binadamu mwenzako neno ambalo anaweza akajisikia vibaya......Pia kuna jamaa alionana na demu wake eti alivyomuona hakumvumilia kabisa akamwambia kwamba smelling man sasa hiyo ni sawa kweli wadau kumwita binadamu mwenzako hiyo lugha kwamba ananuka??Unajuwa nilimmaind sana yaani sema mambo yao yalikuwa hayanihusu lakini ningemwambia ukweli yule dada sio vizuri kumuita mtu ananuka kwa nini hakusema kwa lugha nyingine???Jaribu tuangalie sana midomo yetu ndio inatuponza sana na baadae unakuja kujuta tu
 
Aisee hili ni jambo sensitive sana. Fikiria wewe ndio unaambiwa unanuka....utajisikiaje?

swali zuri sana NN, wangapi Ughaibuni weshakumbana na dhahma ya kuambiwa "you Stinks!"... Inauma kwakweli :( ni sawa na discrimination fulani, itafutwe lugha 'laini' kumfahamisha kistaarabu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom