Unaweza kudhani ni habari za kutunga

Unaweza kudhani ni habari za kutunga

Kwani yaliyowasilishwa kwenye hiyo mada ndiyo mawazo ya wapinzani. Nini kinakufanya wewe uamini hivyo?

Na wapinzani wapi hasa, au unawazungumzia CHADEMA?
Sijaona mwakilishi yeyote wa CHADEMA aliyedai usahihi wa hayo yaliyoelezwa ndani ya andiko.

Hayo uliyoandika huko chini wewe mwenyewe, ni nadhalia tu isiyokuwa na tofauti na ya huyu aliyewasilisha ya kwake hapo juu.
Kwenye hii nchi ukionekana tu unapingana au kuzikosoa baadhi ya sera za serikali ya ccm, hata kama si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa! Utaaambiwa wewe ni CHADEMA!
 
Kugawanyika kwa CCM na vyombo vya dola ni hadithi ya kila msimu wa uchaguzi. Kila ifikapo miaka ya uchaguzi mkuu huwa tunapewa hizi scenarios lakini ikifika siku ya wao kufanya wizi wao kwenye kura huwa wanakunywa kikombe kimoja cha chai na kuwa kitu kimoja.
Saiv sio mda wa uchaguzi uchaguzi umepita miez kadhaa tu nyuma hapo.
 
Mwandishi kumbukeni ni coin kwahiyo hapo kaja kupima upepo.Double agent
 
Labda uniambie kuna kitu kipya kabisa safari hii ambacho hatujawahi kukiona miaka ya nyuma. Maana tuliona mipasuko mikubwa zaidi ya kina Lowassa na bado kikombe cha chai kilinywewa!

Hiyo strong backward pressure huwa inaishia tu kwenye korido za madaraka, lakini ikifika siku yenyewe, huwa wanajua jinsi ya kuorganize na kila mtu anarudi kwenye mstari.
Picha unayojaribu kuijenga hapa na pengine ndiyo iliyo ktk akili yako ni kuwa kwa wewe unajua na kuamini kwamba, kila siku ni alhamisi...

Unadhani kwamba, kwa kuwa jana ilikuwa hivi, basi na leo itakuwa hivyo hivyo. Unajidanganya..!

Mimi nakuambia hivi👇

Ilikuwa hivyo wakati huo, ilishapita hiyo...

Lakini haitakuwa hivyo kesho wala keshokutwa...

Kesho au keshokutwa itakuja na yake..

Unaweza kupenda au usipende...

Hakuna aliyewahi kudhani kuwa ipo siku Watanganyika wangekuja kuandamana na kugomea zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu unaoitishwa nchini...!!

Lakini ilitokea hivyo 29/10/2025 na CCM hawakuamini na hawaamini mpaka leo. Nawe u miongoni mwao bila shaka...!

Hakuna aliyewahi kudhani kuwa ipo siku itatokea serikali iliyochini ya CCM ingeua maelfu ya raia watoto, kinamama, kinababa, kinadada na kinakaka wasio na hatia kwa risasi za moto kama wanyama ili tu kupata madaraka ya urais, ubunge au udiwani...

Samia Suluhu Hassan na genge lake la CCM lilifanya hivyo 29/10/2025...

Sio kila siku ni alhamisi...!

Kila nyakati na majira huja na mambo yake...

Kuna wakati wa kufa na kushindwa pia...

Huu umeshaipata CCM...

Unakuja wakati wa ukiri na kuamini kwako kuwa, NI KWELI ILISEMWA..!
 
Mnyeramba anaamini ni zamu ya Wakristo - Walutheri, baada ya Rais Muislam kustaafu. Zipo jitihada kadhaa zimefanywa ndani ya Kanisa na wanasiasa wa kilutheri.
Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo.
Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa. Wapo pia wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa upinzani, ambao ni waumini wa KKKT wanaounga mkono juhudi za Myera
Thread 'Askofu Malasusa ameigeuza KKKT kuwa jumuiya ya CCM' Askofu Malasusa ameigeuza KKKT kuwa jumuiya ya CCM
 
Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo.
Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa
Iko wazi
 
Picha unayojaribu kuijenga hapa na pengine ndiyo iliyo ktk akili yako ni kuwa kwa wewe unajua na kuamini kwamba, kila siku ni alhamisi...

Unadhani kwamba, kwa kuwa jana ilikuwa hivi, basi na leo itakuwa hivyo hivyo. Unajidanganya..!

Mimi nakuambia hivi👇

Ilikuwa hivyo wakati huo, ilishapita hiyo...

Lakini haitakuwa hivyo kesho wala keshokutwa...

Kesho au keshokutwa itakuja na yake..

Unaweza kupenda au usipende...

Hakuna aliyewahi kudhani kuwa ipo siku Watanganyika wangekuja kuandamana na kugomea zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu unaoitishwa nchini...!!

Lakini ilitokea hivyo 29/10/2025 na CCM hawakuamini na hawaamini mpaka leo. Nawe u miongoni mwao bila shaka...!

Hakuna aliyewahi kudhani kuwa ipo siku itatokea serikali iliyochini ya CCM ingeua maelfu ya raia watoto, kinamama, kinababa, kinadada na kinakaka wasio na hatia kwa risasi za moto kama wanyama ili tu kupata madaraka ya urais, ubunge au udiwani...

Samia Suluhu Hassan na genge lake la CCM lilifanya hivyo 29/10/2025...

Sio kila siku ni alhamisi...!

Kila nyakati na majira huja na mambo yake...

Kuna wakati wa kufa na kushindwa pia...

Huu umeshaipata CCM...

Unakuja wakati wa ukiri na kuamini kwako kuwa, NI KWELI ILISEMWA..!
Hakuna aliyewahi kudhani kuwa ipo siku itatokea serikali iliyochini ya CCM ingeua maelfu ya raia watoto, kinamama, kinababa, kinadada na kinakaka wasio na hatia kwa risasi za moto kama wanyama ili tu kupata madaraka ya urais, ubunge au udiwani...😭😭😭
 
Hana ubavu sema analazimisha huyu siasa zake ni kama za lipumba zinaamka kwa msimu
Sasa hivi anajitahidi ku play low key kumbe nyuma pazia ndiye mkandarasi wa maujinga mengi
 
2030 ni mbali kidogo.

Tutaona mengi.
Ila Emma ni mpole machoni, nyuma ya pazia ana watu wake na mtandao wake.

Magufuli aliona mbali ndio maana akamtupa Brazil na kumfungia asigombee uongoz ndan ya CCM kwa miaka 4. 2017-2021.
We Ni yule mbunge wa Zanzibar eti
 
Unaweza ukahisi ni habari za kutunga, au wale wenzangu na mimi wanasema ni 'drama' za CCM...
Au na Polepole alikuwa anafanya drama?

Anyway!
Huu mtanange una sura nyingi na inabidi utulize kichwa kwelijweli. Ondoa hisia na mihemko ya kisiasa, kiimani na ushabiki wa aina nyingine.

1. Kuna sura ya mbio za Urais; Mngoni vs Mnyeramba

Mweusi anachagua njia ya 'kushawishi na kupendwa na watu' ndio maana kauli zake ni Katiba mpya, Haki, Umoja wa kitaifa...akiamini ndio njia itakayompa nguvu dhidi ya washindani wake.

Mnyeramba anachagua njia ya kutawala kwa mtindo uliopo. Kuendeleza ubabe, kulazimisha madaraka kwa njia yoyote bila kujali watu wanasema nini au wanataka nini.

Mnyeramba ni mtoto wa utawala uliopo na anataka hali ibaki hivyo.
Ndio maana hutamsikia akizungumza maneno kama Katiba Mpya, na hawezi kutamka hadharani kupinga matukio ya utekaji na kuumiza wapinzani, kwa sababu hayo ni sehemu ya 'Modus Operandi' ya utawala uliopo.

2. Ukatoliki vs Ulutheri
Katiba haisemi Rais anatakiwa awe wa dini gani. Lakini kuna utamaduni akitoka Mkristo anafuata Muislam.

Marais wote wakristo wamekuwa Wakatoliki; Nyerere, Mkapa, JPM. Na wote wameshakufa. Mnyeramba anaamini ni zamu ya Wakristo - Walutheri, baada ya Rais Muislam kustaafu. Zipo jitihada kadhaa zimefanywa ndani ya Kanisa na wanasiasa wa kilutheri.
Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo.
Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa. Wapo pia wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa upinzani, ambao ni waumini wa KKKT wanaounga mkono juhudi za Myeramba.

Kwa upande wake mngoni, yeye ni mtoto pendwa wa Kanisa Katoliki. Baadhi ya matamko yake amekuwa akiyatoa akiwa Kanisani. Na matamko hayo yanafanana na matamako ya mapadre na maaskofu wa kanisa Katoliki; Key Words; Haki, Uwajibikaji.

Kwa kukazia hisia za udini katika mbio za urais, Mngoni amewahi kusema; hatuhitaji Rais Mkatoliki au Mlutheri, au Muislam. Akimaanisha tunahitaji Rais anayefaa kwa Watanzania wote.

3. Umakamu vs Uwaziri Mkuu.
Kwa utamaduni wa CCM sio Rais kwa Makamu au Waziri Mkuu kuwa Rais.
Lakini Makamu yupo karibu zaidi na Urais kuliko Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Mngoni anajua; akisubiri 2030 kibarua kitakuwa kigumu kwa sababu utawala uliopo una nafasi kubwa ya ya kuteua mgombea, ambaye hawezi kuwa yeye kwa sababu ya tofauti zilizopo na zisizorekebika.

Vilevile, Mnyeramba ana nguvu kubwa ya pesa alizoiba kwa miaka mingi akiwa serikalini na chamani. Kwa asili ya wajumbe wa CCM, pesa ndio inaamua.

Kwahiyo, Karata kubwa ya Mngoni ni kuwa Rais wa kurithi. Hiyo ndio njia ya haraka kwake, lakini ngumu kwelikweli. Je! Tamaa ya Urais ya Mngoni ni kubwa kiasi cha kuchagua njia yoyote ile, au ni mtu aliyejiwekea mipaka ambayo hawezi kuvuka? Hapo sijui chochote.

4. Uungwaji mkono ndani ya CCM na dola.
CCM imegawanyika, na dola limegawanyika.
Mngoni anaungwa mkono na wazee wa Nyerere, na wanasiasa waliopoteza ulaji wakati huu, ambao pia humuona Rais aliye madarakani, '.hana uwezo wa kuongoza nchi'.

Mnyeramba anaungwa mkono na watawala, vijana wake na marafiki zake (wale wanosema 'thi' badala ya 'si' ) wenye maono yanayofanana.

Yakiwemo maono ya kuumiza watu kwa sababu ya fedha na madaraka.
Huko kwenye vyombo vya dola tunahitaji muda zaidi..

Mwisho!
Rais wangu ni Tundu Lissu.

Nawasilisha!
Dr. Christopher CyriloView attachment 3644312View attachment 3644313
Mbona sie tunajua raisi wetu ni TAL tunampambania atoke Jela tumsimike tu!
 
Back
Top Bottom