Unaweza kudhani ni habari za kutunga

Unaweza kudhani ni habari za kutunga

Kawaida hapajawahi kuwepo na Rais wa Tanzania Bara ambae alikuwa waziri mkuu mstaafu.

Huyo mnyiramba japo anatengenezewa mazingira na boss wake kama njia ya kulipa fadhila kwa kanisa la lutheran kumuunga mkono, lakini kazi naamini itakuwa kubwa kumpa huo urais.

Kwa upande mwingine, pia hapajawahi kutokea Rais ambae alikuea makamu kabla, kama yupo nikumbushwe.

So kiuhalisia mwisho wa siku sitashangaa nikiona wote wawili mnyiramba na mngoni wakitoswa CCM wakaja na jina lingine tofauti.
 
Unaweza ukahisi ni habari za kutunga, au wale wenzangu na mimi wanasema ni 'drama' za CCM...
Au na Polepole alikuwa anafanya drama?

Anyway!
Huu mtanange una sura nyingi na inabidi utulize kichwa kwelijweli. Ondoa hisia na mihemko ya kisiasa, kiimani na ushabiki wa aina nyingine.

1. Kuna sura ya mbio za Urais; Mngoni vs Mnyeramba

Mweusi anachagua njia ya 'kushawishi na kupendwa na watu' ndio maana kauli zake ni Katiba mpya, Haki, Umoja wa kitaifa...akiamini ndio njia itakayompa nguvu dhidi ya washindani wake.

Mnyeramba anachagua njia ya kutawala kwa mtindo uliopo. Kuendeleza ubabe, kulazimisha madaraka kwa njia yoyote bila kujali watu wanasema nini au wanataka nini. Mnyeramba ni mtoto wa utawala uliopo na anataka hali ibaki hivyo. Ndio maana hutamsikia akizungumza maneno kama Katiba Mpya, na hawezi kutamka hadharani kupinga matukio ya utekaji na kuumiza wapinzani, kwa sababu hayo ni sehemu ya 'Modus Operandi' ya utawala uliopo.

2. Ukatoliki vs Ulutheri
Katiba haisemi Rais anatakiwa awe wa dini gani. Lakini kuna utamaduni akitoka Mkristo anafuata Muislam. Marais wote wakristo wamekuwa Wakatoliki; Nyerere, Mkapa, JPM. Na wote wameshakufa. Mnyeramba anaamini ni zamu ya Wakristo - Walutheri, baada ya Rais Muislam kustaafu. Zipo jitihada kadhaa zimefanywa ndani ya Kanisa na wanasiasa wa kilutheri. Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo. Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa. Wapo pia wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa upinzani, ambao ni waumini wa KKKT wanaounga mkono juhudi za Myeramba.

Kwa upande wake mngoni, yeye ni mtoto pendwa wa Kanisa Katoliki. Baadhi ya matamko yake amekuwa akiyatoa akiwa Kanisani. Na matamko hayo yanafanana na matamako ya mapadre na maaskofu wa kanisa Katoliki; Key Words; Haki, Uwajibikaji.

Kwa kukazia hisia za udini katika mbio za urais, Mngoni amewahi kusema; hatuhitaji Rais Mkatoliki au Mlutheri, au Muislam. Akimaanisha tunahitaji Rais anayefaa kwa Watanzania wote.

3. Umakamu vs Uwaziri Mkuu.
Kwa utamaduni wa CCM sio Rais kwa Makamu au Waziri Mkuu kuwa Rais.
Lakini Makamu yupo karibu zaidi na Urais kuliko Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Mngoni anajua; akisubiri 2030 kibarua kitakuwa kigumu kwa sababu utawala uliopo una nafasi kubwa ya ya kuteua mgombea, ambaye hawezi kuwa yeye kwa sababu ya tofauti zilizopo na zisizorekebika. Vilevile, Mnyeramba ana nguvu kubwa ya pesa alizoiba kwa miaka mingi akiwa serikalini na chamani. Kwa asili ya wajumbe wa CCM, pesa ndio inaamua.

Kwahiyo, Karata kubwa ya Mngoni ni kuwa Rais wa kurithi. Hiyo ndio njia ya haraka kwake, lakini ngumu kwelikweli. Je! Tamaa ya Urais ya Mngoni ni kubwa kiasi cha kuchagua njia yoyote ile, au ni mtu aliyejiwekea mipaka ambayo hawezi kuvuka? Hapo sijui chochote.

4. Uungwaji mkono ndani ya CCM na dola.
CCM imegawanyika, na dola limegawanyika.
Mngoni anaungwa mkono na wazee wa Nyerere, na wanasiasa waliopoteza ulaji wakati huu, ambao pia humuona Rais aliye madarakani, '.hana uwezo wa kuongoza nchi'. Mnyeramba anaungwa mkono na watawala, vijana wake na marafiki zake (wale wanosema 'thi' badala ya 'si' ) wenye maono yanayofanana. Yakiwemo maono ya kuumiza watu kwa sababu ya fedha na madaraka.
Huko kwenye vyombo vya dola tunahitaji muda zaidi..

Mwisho!
Rais wangu ni Tundu Lissu.

Nawasilisha!
Dr. Christopher CyriloView attachment 3644312View attachment 3644313
Uchambuzi umekaa vizuri. Hata mimi ninamshauri asijiuzulu ili tuuone ukweli uliojificha kwa muda sasa.

Na uzuri Yuda ana historia yake ya 2015 pale alipoungana na wenzake wachache, na kujitokeza hadharani kupinga maamuzi ya Kamati kuu.
 
Ninachojuwa bila ya shaka yoyote, huu siyo mwandiko wa mleta mada. Kuna mtu kaazima jina.

Ni muhimu kulibainisha hili kabla ya mjadala wa mada yenyewe.

Kuhusu mada: Mgombea yeyote anayejiegemeza kwenye kundi la Genge na Samia Suluhu Hassan; hiyo ni sifa kuu inayomwondoa mhusika katika matarajio ya kuiongoza nchi hii.

Hizo sifa nyinginezo zinazojadiliwa humo ndani, kama hizo za kiimani ni za kipuuzi.
Tanzania haiwezi kutazama viongozi wake kwa misingi ya imani zao za kidini

Namtaka Nchimbi akomalie msimamo wake, asijiuzuru na akisha isalimisha CCM yake na pengine tukishapata fursa ya kurekebisha taratibu za kupata viongozi wetu kwa HAKI/HURU, akiwa tayari apambane na Tundu Lissu kwenye uchaguzi huru kabisa.
Ni kweli kabisa mkuu Kalamu Mimi nimeinakili kama ilivyo mpaka jina la mwandishi mwisho wa mada🙏🏿
 
Kawaida hapajawahi kuwepo na Rais wa Tanzania Bara ambae alikuwa waziri mkuu mstaafu.

Huyo mnyiramba japo anatengenezewa mazingira na boss wake kama njia ya kulipa fadhila kwa kanisa la lutheran kumuunga mkono, lakini kazi naamini itakuwa kubwa kumpa huo urais.

Kwa upande mwingine, pia hapajawahi kutokea Rais ambae alikuea makamu kabla, kama yupo nikumbushwe.

So kiuhalisia mwisho wa siku sitashangaa nikiona wote wawili mnyiramba na mngoni wakitoswa CCM wakaja na jina lingine tofauti.
 
Uchambuzi umekaa vizuri. Hata mimi ninamshauri asijiuzulu ili tuuone ukweli uliojificha kwa muda sasa.

Na uzuri Yuda ana historia yake ya 2015 pale alipoungana na wenzake wachache, na kujitokeza hadharani kupinga maamuzi ya Kamati kuu.
Ndio.
Historia hiyo ni muhimu pia isisahaulike; kwa sababu ni alama muhimu kumhusu yeye; kwamba hayumbiyumbi tu, bali kuna mambo anayoyaamini ndani ya dhamira yake.
Hicho ni kigezo muhimu kwa kiongozi yeyote.
 
Hapa ndipo tunasema wapinzani wa nchi hawana Agenda ya kudumu kuleta mabadiliko ya hii nchi si kwa mawazo ya kutengenezewa kama hayo, Hakuna ugomvi wala hizo drama kati ya hao uliowataja zaidi ya kuwapumbaza tu.
Kwani yaliyowasilishwa kwenye hiyo mada ndiyo mawazo ya wapinzani. Nini kinakufanya wewe uamini hivyo?

Na wapinzani wapi hasa, au unawazungumzia CHADEMA?
Sijaona mwakilishi yeyote wa CHADEMA aliyedai usahihi wa hayo yaliyoelezwa ndani ya andiko.

Hayo uliyoandika huko chini wewe mwenyewe, ni nadhalia tu isiyokuwa na tofauti na ya huyu aliyewasilisha ya kwake hapo juu.
 
Unaweza ukahisi ni habari za kutunga, au wale wenzangu na mimi wanasema ni 'drama' za CCM...
Au na Polepole alikuwa anafanya drama?

Anyway!
Huu mtanange una sura nyingi na inabidi utulize kichwa kwelijweli. Ondoa hisia na mihemko ya kisiasa, kiimani na ushabiki wa aina nyingine.

1. Kuna sura ya mbio za Urais; Mngoni vs Mnyeramba

Mweusi anachagua njia ya 'kushawishi na kupendwa na watu' ndio maana kauli zake ni Katiba mpya, Haki, Umoja wa kitaifa...akiamini ndio njia itakayompa nguvu dhidi ya washindani wake.

Mnyeramba anachagua njia ya kutawala kwa mtindo uliopo. Kuendeleza ubabe, kulazimisha madaraka kwa njia yoyote bila kujali watu wanasema nini au wanataka nini. Mnyeramba ni mtoto wa utawala uliopo na anataka hali ibaki hivyo. Ndio maana hutamsikia akizungumza maneno kama Katiba Mpya, na hawezi kutamka hadharani kupinga matukio ya utekaji na kuumiza wapinzani, kwa sababu hayo ni sehemu ya 'Modus Operandi' ya utawala uliopo.

2. Ukatoliki vs Ulutheri
Katiba haisemi Rais anatakiwa awe wa dini gani. Lakini kuna utamaduni akitoka Mkristo anafuata Muislam. Marais wote wakristo wamekuwa Wakatoliki; Nyerere, Mkapa, JPM. Na wote wameshakufa. Mnyeramba anaamini ni zamu ya Wakristo - Walutheri, baada ya Rais Muislam kustaafu. Zipo jitihada kadhaa zimefanywa ndani ya Kanisa na wanasiasa wa kilutheri. Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo. Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa. Wapo pia wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa upinzani, ambao ni waumini wa KKKT wanaounga mkono juhudi za Myeramba.

Kwa upande wake mngoni, yeye ni mtoto pendwa wa Kanisa Katoliki. Baadhi ya matamko yake amekuwa akiyatoa akiwa Kanisani. Na matamko hayo yanafanana na matamako ya mapadre na maaskofu wa kanisa Katoliki; Key Words; Haki, Uwajibikaji.

Kwa kukazia hisia za udini katika mbio za urais, Mngoni amewahi kusema; hatuhitaji Rais Mkatoliki au Mlutheri, au Muislam. Akimaanisha tunahitaji Rais anayefaa kwa Watanzania wote.

3. Umakamu vs Uwaziri Mkuu.
Kwa utamaduni wa CCM sio Rais kwa Makamu au Waziri Mkuu kuwa Rais.
Lakini Makamu yupo karibu zaidi na Urais kuliko Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Mngoni anajua; akisubiri 2030 kibarua kitakuwa kigumu kwa sababu utawala uliopo una nafasi kubwa ya ya kuteua mgombea, ambaye hawezi kuwa yeye kwa sababu ya tofauti zilizopo na zisizorekebika. Vilevile, Mnyeramba ana nguvu kubwa ya pesa alizoiba kwa miaka mingi akiwa serikalini na chamani. Kwa asili ya wajumbe wa CCM, pesa ndio inaamua.

Kwahiyo, Karata kubwa ya Mngoni ni kuwa Rais wa kurithi. Hiyo ndio njia ya haraka kwake, lakini ngumu kwelikweli. Je! Tamaa ya Urais ya Mngoni ni kubwa kiasi cha kuchagua njia yoyote ile, au ni mtu aliyejiwekea mipaka ambayo hawezi kuvuka? Hapo sijui chochote.

4. Uungwaji mkono ndani ya CCM na dola.
CCM imegawanyika, na dola limegawanyika.
Mngoni anaungwa mkono na wazee wa Nyerere, na wanasiasa waliopoteza ulaji wakati huu, ambao pia humuona Rais aliye madarakani, '.hana uwezo wa kuongoza nchi'. Mnyeramba anaungwa mkono na watawala, vijana wake na marafiki zake (wale wanosema 'thi' badala ya 'si' ) wenye maono yanayofanana. Yakiwemo maono ya kuumiza watu kwa sababu ya fedha na madaraka.
Huko kwenye vyombo vya dola tunahitaji muda zaidi..

Mwisho!
Rais wangu ni Tundu Lissu.

Nawasilisha!
Dr. Christopher CyriloView attachment 3644312View attachment 3644313
Mnyiramba hawezi tena tena asahau hiyo hiyo katiba iliopo inakataza kama umeshakuwa waziri mkuu hauwezi tena kushika nafasi kubwa zaidi ya hiyo ndani ya serikali labda ukiwa nje ya chama chako.kingine huyu mngoni magu mwenyewe alimwogopa yaani ana mguvu mno tena ccm kama wana akili wachutame tuu wasikurupuke kushindanana nae mama enu akubali tuu kuchutama zaidi ya hapoatoboi hata mwaka huu.
Kwa heshma atulie mngoni afanye siasa za kujijenga hivyo hivyo tu hadi mwisho wake uishe astaafu kwa heshma zaidi ya hapo mda si mrefu atahemea mdomo maana pumzi puani itakuwa ndogo
 
Kwani yaliyowasilishwa kwenye hiyo mada ndiyo mawazo ya wapinzani. Nini kinakufanya wewe uamini hivyo?

Na wapinzani wapi hasa, au unawazungumzia CHADEMA?
Sijaona mwakilishi yeyote wa CHADEMA aliyedai usahihi wa hayo yaliyoelezwa ndani ya andiko.

Hayo uliyoandika huko chini wewe mwenyewe, ni nadhalia tu isiyokuwa na tofauti na ya huyu aliyewasilisha ya kwake hapo juu.
Mlengo wa mleta mada ni upande wa upinzani licha ya kuifanya kuwa habari huru.
 
2030 ni mbali kidogo.

Tutaona mengi.
Ila Emma ni mpole machoni, nyuma ya pazia ana watu wake na mtandao wake.

Magufuli aliona mbali ndio maana akamtupa Brazil na kumfungia asigombee uongoz ndan ya CCM kwa miaka 4. 2017-2021.
Ni mwana comrade huyu . Atakuwa na mtandao wake mzito sana nyuma ya pazia.
 
Kawaida hapajawahi kuwepo na Rais wa Tanzania Bara ambae alikuwa waziri mkuu mstaafu.

Huyo mnyiramba japo anatengenezewa mazingira na boss wake kama njia ya kulipa fadhila kwa kanisa la lutheran kumuunga mkono, lakini kazi naamini itakuwa kubwa kumpa huo urais.

Kwa upande mwingine, pia hapajawahi kutokea Rais ambae alikuea makamu kabla, kama yupo nikumbushwe.

So kiuhalisia mwisho wa siku sitashangaa nikiona wote wawili mnyiramba na mngoni wakitoswa CCM wakaja na jina lingine tofauti.
SSH!
 
Kugawanyika kwa CCM na vyombo vya dola ni hadithi ya kila msimu wa uchaguzi. Kila ifikapo miaka ya uchaguzi mkuu huwa tunapewa hizi scenarios lakini ikifika siku ya wao kufanya wizi wao kwenye kura huwa wanakunywa kikombe kimoja cha chai na kuwa kitu kimoja.
Not this time..

They have pushed everything on the wall..

The backward pressure to sustain the reaction is very strong to hold...
 
Mnyiramba hawezi tena tena asahau hiyo hiyo katiba iliopo inakataza kama umeshakuwa waziri mkuu hauwezi tena kushika nafasi kubwa zaidi ya hiyo ndani ya serikali labda ukiwa nje ya chama chako.kingine huyu mngoni magu mwenyewe alimwogopa yaani ana mguvu mno tena ccm kama wana akili wachutame tuu wasikurupuke kushindanana nae mama enu akubali tuu kuchutama zaidi ya hapoatoboi hata mwaka huu.
Kwa heshma atulie mngoni afanye siasa za kujijenga hivyo hivyo tu hadi mwisho wake uishe astaafu kwa heshma zaidi ya hapo mda si mrefu atahemea mdomo maana pumzi puani itakuwa ndogo
Anatamani sana kutengeneza historia ya 3bila
 
Not this time..

They have pushed everything on the wall..

The backward pressure to sustain the reaction is very strong to hold...
Labda uniambie kuna kitu kipya kabisa safari hii ambacho hatujawahi kukiona miaka ya nyuma. Maana tuliona mipasuko mikubwa zaidi ya kina Lowassa na bado kikombe cha chai kilinywewa!

Hiyo strong backward pressure huwa inaishia tu kwenye korido za madaraka, lakini ikifika siku yenyewe, huwa wanajua jinsi ya kuorganize na kila mtu anarudi kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom