Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,140
- 859,420
Unaweza ukahisi ni habari za kutunga, au wale wenzangu na mimi wanasema ni 'drama' za CCM...
Au na Polepole alikuwa anafanya drama?
Anyway!
Huu mtanange una sura nyingi na inabidi utulize kichwa kwelijweli. Ondoa hisia na mihemko ya kisiasa, kiimani na ushabiki wa aina nyingine.
1. Kuna sura ya mbio za Urais; Mngoni vs Mnyeramba
Mweusi anachagua njia ya 'kushawishi na kupendwa na watu' ndio maana kauli zake ni Katiba mpya, Haki, Umoja wa kitaifa...akiamini ndio njia itakayompa nguvu dhidi ya washindani wake.
Mnyeramba anachagua njia ya kutawala kwa mtindo uliopo. Kuendeleza ubabe, kulazimisha madaraka kwa njia yoyote bila kujali watu wanasema nini au wanataka nini.
Mnyeramba ni mtoto wa utawala uliopo na anataka hali ibaki hivyo.
Ndio maana hutamsikia akizungumza maneno kama Katiba Mpya, na hawezi kutamka hadharani kupinga matukio ya utekaji na kuumiza wapinzani, kwa sababu hayo ni sehemu ya 'Modus Operandi' ya utawala uliopo.
2. Ukatoliki vs Ulutheri
Katiba haisemi Rais anatakiwa awe wa dini gani. Lakini kuna utamaduni akitoka Mkristo anafuata Muislam.
Marais wote wakristo wamekuwa Wakatoliki; Nyerere, Mkapa, JPM. Na wote wameshakufa. Mnyeramba anaamini ni zamu ya Wakristo - Walutheri, baada ya Rais Muislam kustaafu. Zipo jitihada kadhaa zimefanywa ndani ya Kanisa na wanasiasa wa kilutheri.
Waliofuatilia kwa jicho la kijasusi uchaguzi wa Askofu Mkuu wa KKKT wanafahamu vema picha ilivyo.
Na baadhi ya viomgozi wa KKKT wamekuwa na mahusiano mazuri na utawala uliopo, na hata kusababisha mgogoro ndani ya Kanisa. Wapo pia wanasiasa wakubwa, wakiwemo wa upinzani, ambao ni waumini wa KKKT wanaounga mkono juhudi za Myeramba.
Kwa upande wake mngoni, yeye ni mtoto pendwa wa Kanisa Katoliki. Baadhi ya matamko yake amekuwa akiyatoa akiwa Kanisani. Na matamko hayo yanafanana na matamako ya mapadre na maaskofu wa kanisa Katoliki; Key Words; Haki, Uwajibikaji.
Kwa kukazia hisia za udini katika mbio za urais, Mngoni amewahi kusema; hatuhitaji Rais Mkatoliki au Mlutheri, au Muislam. Akimaanisha tunahitaji Rais anayefaa kwa Watanzania wote.
3. Umakamu vs Uwaziri Mkuu.
Kwa utamaduni wa CCM sio Rais kwa Makamu au Waziri Mkuu kuwa Rais.
Lakini Makamu yupo karibu zaidi na Urais kuliko Waziri Mkuu.
Hata hivyo, Mngoni anajua; akisubiri 2030 kibarua kitakuwa kigumu kwa sababu utawala uliopo una nafasi kubwa ya ya kuteua mgombea, ambaye hawezi kuwa yeye kwa sababu ya tofauti zilizopo na zisizorekebika.
Vilevile, Mnyeramba ana nguvu kubwa ya pesa alizoiba kwa miaka mingi akiwa serikalini na chamani. Kwa asili ya wajumbe wa CCM, pesa ndio inaamua.
Kwahiyo, Karata kubwa ya Mngoni ni kuwa Rais wa kurithi. Hiyo ndio njia ya haraka kwake, lakini ngumu kwelikweli. Je! Tamaa ya Urais ya Mngoni ni kubwa kiasi cha kuchagua njia yoyote ile, au ni mtu aliyejiwekea mipaka ambayo hawezi kuvuka? Hapo sijui chochote.
4. Uungwaji mkono ndani ya CCM na dola.
CCM imegawanyika, na dola limegawanyika.
Mngoni anaungwa mkono na wazee wa Nyerere, na wanasiasa waliopoteza ulaji wakati huu, ambao pia humuona Rais aliye madarakani, '.hana uwezo wa kuongoza nchi'.
Mnyeramba anaungwa mkono na watawala, vijana wake na marafiki zake (wale wanosema 'thi' badala ya 'si' ) wenye maono yanayofanana.
Yakiwemo maono ya kuumiza watu kwa sababu ya fedha na madaraka.
Huko kwenye vyombo vya dola tunahitaji muda zaidi..
Mwisho!
Rais wangu ni Tundu Lissu.
Nawasilisha!
Dr. Christopher Cyrilo