Unatumia mbinu gani kuepuka kodi (tax avoidance) bila kuvunja sheria za nchi?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Tuwe wakweli hakuna kinachouma kama kulipa kodi na unalipa huku unajua kabisa pesa hizi haziendi kuleta maendeleo ya nchi, wanaenda kunufaika familia flani ukibisha hili soma ripoti ya CAG na angalia kinachoendelea TANESCO na sisi tunaofanya biashara za mazao huwa tunapita vijijini utakubali kuwa kodi hazifanyi kazi.

Pamoja na yote hayo kulipa kodi ni wajibu na wajibu huu upo kwa mujibu wa sheria za nchi, mimi binafsi ni mlipa kodi mzuri sana nalipa kodi kupitia ajira yangu ya uwalimu, nalipa kodi za magari yangu ya biashara, nalipa kodi za ardhi nalipa kodi za biashara za mazao nk nikipiga hesabu kiasi ambacho kinaenda serikalini na maendeleo ya nchi najikuta nipo bored sana, hivyo huwa nafikiria mbinu na marifa ya kukwepa kodi zaidi kwa sasa ili kukwepa kodi huwa nafanya haya.

1. Nasajili biashara kwa majina tofauti tofauti, mfano gari zipo tatu na nina mpango wa kuongeza nyingine , hizi nimesajili moja kwa jina la mjomba, nyingine mama na nyingine nimempa mfanyakazi wangu ukiniuliza kwa nini nafanya hivyo ni kwa sababu hawa jamaa wakiona jina lako huwa wananza kukufuata fuata kiboya na kuanza kuwekewa kodi za ajabu.

2. Nawekeza maeneo ambayo hayana kodi, nimeamua kuwekeza sana shambani, ukiwa na heka zaidi ya mia kwa nchi hii hulipi kodi, ila ukiwa na gunia hata 50 tu za mchele pale store pana kodi, so dawa nikuwekeza sana kwenye mashamba, kama una mbinu nyingine ya kukwepa kodi hapa share ili tuongeze marifa, tutakuwa huru kulipa kodi iwapo serikali itaonekana ipo serious kusimamia kodi zenyewe, share mbinu hata haramu ila tu isihushe kuwahonga wafanyakazi wa serikali hasa TRA, polisi na hawa watoza ushuru.
 
Hapi shamva unakwepaje kodi? Je mazao unaysuza reje reja ? Unayapitishaje mpaka mjini wakati kuna mageti ta ushuru?

Mfano Ukiuza msitu jwa mfanyabuasgara anakadiria na kodi kwenye bei hivyo anashusha pesa kufidia kodi, ukiuza mfugo hivyo hivyo, mazao hivyo hivyo labda kama una genge. Sasa kuna genge la kuuza mazao ta heka 10+ Eleza vizuri unakwepaje kodi kwenye shamba?

Ikimsoma R.Kiwasoki yeye ameshauri TAX DELAY, abasema chekews kulipa kodi ilibuizungushe hio hela sijajua kwa gaoa bongo jama wana cakculate % ya ku delay kulipa kodi.

MENEJA WA TRA ANAJENGA GHOROFA WAKATI MFANYABIASHARA ANAJENGA KIBANDA, badala ingekuwa viceversa. THIS IS AFRIKA! Poleni sana wafanya biashara
 
Mimi kwenye uhitaji wa miamala hasa kutoa pesa kwa wakala huwa natumia njia mbadala.
Nakuwa nimeepuka kodi na sio kukwepa.
 
Kichwa cha habari ni "kukwepa kodi" (Tax invasion) ila maelezo yako yamejikita kwenye dhana ya "kupanga kodi" (Tax avoidance).

Kukwepa kodi ni kukataa kulipa kodi halali kisheria na ni kosa la jinai.

Kupanga kodi ni kutumia mianya ya kisheria ili ulipe kodi kidogo. Mfano kusajili biashara kwa majina tofauti. Na hili siyo kosa
 
Kukwepa kodi ni kosa kubwa sana kisheria, sasa unasema unalipa kodi halafu huoni kazi yake au huoni maendeleo na ww ni mwalimu unalipwa mshahara kwa kutumia hela za mama yako? Hivi ni kweli huoni maendeleo yoyote? Acha siasa za kupinga kila kitu, sisi pia tuna macho na better education na tunaona kuna maendeleo walau yanafanyika mengi tu
 
Kichwa cha habari ni "kukwepa kodi" (Tax invasion) ila maelezo yako yamejikita kwenye dhana ya "kupanga kodi" (Tax avoidance).

Kukwepa kodi ni kukataa kulipa kodi halali kisheria na ni kosa la jinai.

Kupanga kodi ni kutumia mianya ya kisheria ili ulipe kodi kidogo. Mfano kusajili baishara kwa majina tofauti. Na hili siyo kosa
Ww ndo umeandika kisomi
 
Kukwepa kodi ni kosa kubwa sana kisheria, sasa unasema unalipa kodi halafu huoni kazi yake au huoni maendeleo na ww ni mwalimu unalipwa mshahara kwa kutumia hela za mama yako? Hivi ni kweli huoni maendeleo yoyote? Acha siasa za kupinga kila kitu, sisi pia tuna macho na better education na tunaona kuna maendeleo walau yanafanyika mengi tu
Acha ufala wewe,kwny salary yangu 1m ,laki 4 huwa inarudi tena Kwa anayenilipa hiyo salary, hapo naishi nyumba ya kupanga yenye Kodi na tozo ,maji nanunua,usafir nalipia Kodi.

Wakati mbunge analipwa 12m mpk 15m anapewa nyumba,gari,Hela ya Kila kikao,posho nk.
 
Honga maafisa wa TRA, ufanyiwe makadirio ya chini pia kwa msaada zaidi ongea na tax consultant watakupa maujanja kibao, hii nchi kulipa kodi ni kunufaisha mafisadi ya kijani.
Na hilo ndilo linalouma sana. Yaani unalipa kodi huku unajua kwamba zinangia kunufaisha mafisadi. Kukwepa kodi (evasion) ni kosa, ila kuepuka (avoidance) sio kosa. Tuendelee kuelimishana wadau
 
Back
Top Bottom