Chadema ni chama kilichoanzishwa kwa mfumo wa kibepari. Kwahiyo Msingi mkuu wa chadema ni ubepari.
Mwanzilishi wa Chadema ni Mzee Mtei ambaye alitofautiana na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Tofauti yao ni kuhusu sera za IMF Mtei alikuwa anaunga mkono bali Nyerere alikataa sera za kibepari.
Kwahiyo Sera za kibepari msingi wake mkuu ni mtaji (Pesa).
Kimekuwa kikipata misaada ya chini chini kutoka katika nchi za magharibi kama Uholanzi na zingine, kitendo ambocho kinanipa mashaka kuwa vipi pesa hizo zitalipwa. Ninadhani kuna makubaliano ya chini kwa chini ambayo watu wengi hatuyajui.
CHADEMA kimejitahidi sana kuwafundisha wanachama wake kutohoji mapato na matumzi ya chama. Hii ni mbinu ambayo imetumiwa na CHADEMA kuwaaminisha wanachama dhidi ya viongozi kuwa wao hawana doa.
Kaka/Dada, hapo kwenye Kijani, CCM kilianzishwa kama chama cha wakulima na wafanyakzi, leo waweza sema the same, kumbuka hotuba ya JK kwa wazee wa Dar, mwezi May, 2010, alisema kabisa, hazitaki kura za wafanyakazi.
Kwenye Red, hiv unakumbuka Nyerere kabla hajafa aliwahi kukifagilia CHADEMA kwamba ndio chama chenye sera zinazoeleweka, tena huyo Mtei unaye msema ndiye alikuwa ndiye mwenyekiti na Bob Makani katibu (RIP) kama walitofautiana kihivyo, basi asingefagilia chama cha adui yake.
Kwenye Blue, kama kumbukumbu zangu zitakuwa sahihi, CDM ndio chama pekee nchini kilicho toa mahesabu yake mapema kwa msajiri wa vyama mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, sina hakika kama magamba na wakeze walifanya hivyo hadi leo, mwenye records tofauti naomba anisahihishe.
Kuhusu ubepari, hivi aliye uza nchi kwa wazungu waliokuwa maadui wa Nyerere, yaani makaburu ni nani? nadhani we ni mtoto, rejea historia ya miaka 70-80 Nyerere na uhusiano wake na SA (South Africa), nyinyiem ni wanafiki wakubwa, wanahubiri ujamaa while wanacheza Kibepari.