Chadema ilianzishwa kihalali kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ilikidhi vigezo vyote vya kisheria na kikatiba ndio maana vyombo vya serikali vinavyosimamia sheria za nchi yetu havina tatizo lolote na uwepo wa chama hiki, namna kinavyojiendesha wala mambo kinayodai kuyasimamia.
Unaposema sisi watanzania sio CHADEMA nadhani umejisahau kwamba mimi binafsi ni mtanzania, tena mtanzania kindaki ndaki na sio kama baadhi ya wana CCM wenzako wengi tu kama BASHE,KINANA,MUNGAI,n.k
Kuhusu ubepari unaonekana ni mtu usiyekuwa na uelewa wowote ule juu ya mifumo ya kiuchumi na namna inavyopata nafasi ya ushiriki kwenye Jamii tofauti tofauti, achilia mbali kwamba inaonyesha hauelewi serikali inayoongozwa na chama chako inafuata mfumo upi wa uchumi.
Kuhusu Kutoelewana kwa Mtei na Nyerere, labda tungeanza kuelezana ni nini kinafanya mimi na wewe tusielewane kwanza kabla ya kurukia mambo ya watu wengine, na kama wewe unaona ni makosa makubwa sana kwa mtu kukosana na nyerere basi tueleze pia hizi habari zinazodai kwamba aliyekuwa mwenyekiti wa chama chako anaelewa sababu za Kifo chake ambazo sisi hatuzijui zina ukweli gani.