Unataka kuijua CHADEMA? Angalia hapa

mtoa maada umetumia kigezo kipi kuja na hii thread? au umelewa ndio ukaingia hapa? tuliza ubongo ndio ulete maada

Kwanza hii sio maada ni mada sawa! kigezo ni mimi ni member wa jf basi sawa mheshimiwa?
 
Chadema ni chama kilichoanzishwa kwa mfumo wa kibepari. Kwahiyo Msingi mkuu wa chadema ni ubepari.
Mwanzilishi wa Chadema ni Mzee Mtei ambaye alitofautiana na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Tofauti yao ni kuhusu sera za IMF Mtei alikuwa anaunga mkono bali Nyerere alikataa sera za kibepari.

Kwahiyo Sera za kibepari msingi wake mkuu ni mtaji (Pesa).
Kimekuwa kikipata misaada ya chini chini kutoka katika nchi za magharibi kama Uholanzi na zingine, kitendo ambocho kinanipa mashaka kuwa vipi pesa hizo zitalipwa. Ninadhani kuna makubaliano ya chini kwa chini ambayo watu wengi hatuyajui.

CHADEMA kimejitahidi sana kuwafundisha wanachama wake kutohoji mapato na matumzi ya chama. Hii ni mbinu ambayo imetumiwa na CHADEMA kuwaaminisha wanachama dhidi ya viongozi kuwa wao hawana doa.

na hii ni hatari sana.
Kweli CDM inawanyima usingizi, mnajaribu kubuni mbinu kila angle za kutowaimanisha wananchi waone CDM sio mkombozi wao, lakini wapi. Huu ukombozi unaletwa na Mungu kupitia CDM, hakuna wa kuuzuia, Wana wa Tanganyika wameteseka kwa miaka mingi sana ndani ya nchi yao aliyowapa Mwenyezi Mungu yenye neema lukuki.
Fanya uchunguzi kwanza kwenye chama chako mnachosema kitatawala milele, bado ni chama cha ujamaa ikiwa na maana ya chama cha wakulima na wafanyakazi? na msingi wenu sio pesa ni kilimo?
Mapato na matumizi ya chama chako unayajua?
Ungejua kiasi kikubwa cha mapato ya chama cha majambazi (ccm) wanachofuja kinatoka wapi, usingetamani kuishi dunia hii!
 
Ubepari tatizo lake ni kwamba mwenyenacho ndie anayepata na siye nacho ataendelea kuwa mnyonge.

Ni tofauti kabisa na mfumo wa kijamaa.
Jaribu kujikumbusha Uraia au siasa darasa la tatu shule ya msingi.
Wako sawa maana hata Azimio la Arusha ambalo ni la CCM kwa ujumla linasema hivi;
"Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini si nchi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
ikapanuka na kuenea"
Sasa tangu limewekwa huoni kuwa ni wakati misingi ienee kisawasawa?.
 
Sasa unipa wasi wasi na ufahamu wako maan wewe unasema mmeanza kurudi kwenye enzi zenu pale mlipozaliwa toka Tanu na asp, sasa hapa unakana kwamba wewe sio ccm, sasa wewe ni chama Gani? au wewe uliwahi kuwaliza Chadema maswali unayouliza hapa JF? Acha unafiki na kama wewe ni mzalendo kama unavyojiita vaa gwanda, ili tubadili mfumo mzima wa serikali, Mfumo hauwezi kubadilishwa na mtu mmoja bali kwa wazalendo wa kweli kushirikiana kwa pamoja, ccm washindwa na sasa meli ya ukombozi ni Chadema ukiwa mzalendo wa kweili Panda Meli hii.

Wewe tatizo lako nini hasa umesoma maelezo yangu yote. Je unahoja ya kujitetea niliyo yatoa?
 
Signature yako na ulichokiandika vinarandana kabisa sasa sijui tukusaidieje maana hata ukibebwa hubebeki umekosea kujiunga JF tafuta mtandao mwingine hapa sipo pahala pake... Pole sana ndugu!!
 
Naunga mkono hii hoja kwa asilimia mia moja.
Juzi kwenye mkutano wa CHADEMA Jangwani, kulikuwa na mamluki ambao hata mimi niliwatilia shaka. Walikuwa wamekaribishwa na walikaa kama vile nao ni wenyeji (Watz). Najiuliza, hawa ndo washauri wa CHADEMA? au wamekuja kungalia pesa wanayotoa inatumikaje? Au wana agenda gani ya siri na CHADEMA?

CHADEMA wanarejesha ukoloni Tz, wanatupiga bei kabla hata hawajakamata dola.

View attachment 56234

Hatuwapi kura hawa maana hiki chama ni biashara ya watu furani wa nje. Ni For profit organization.
 
mtu mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu pamoja na ngano upumbavu wake haumtoki
 
Chadema ni chama kilichoanzishwa kwa mfumo wa kibepari. Kwahiyo Msingi mkuu wa chadema ni ubepari.
Mwanzilishi wa Chadema ni Mzee Mtei ambaye alitofautiana na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Tofauti yao ni kuhusu sera za IMF Mtei alikuwa anaunga mkono bali Nyerere alikataa sera za kibepari.

Kwahiyo Sera za kibepari msingi wake mkuu ni mtaji (Pesa).
Kimekuwa kikipata misaada ya chini chini kutoka katika nchi za magharibi kama Uholanzi na zingine, kitendo ambocho kinanipa mashaka kuwa vipi pesa hizo zitalipwa. Ninadhani kuna makubaliano ya chini kwa chini ambayo watu wengi hatuyajui.

CHADEMA kimejitahidi sana kuwafundisha wanachama wake kutohoji mapato na matumzi ya chama. Hii ni mbinu ambayo imetumiwa na CHADEMA kuwaaminisha wanachama dhidi ya viongozi kuwa wao hawana doa.

na hii ni hatari sana.
umesau UDINI naokikumba Chama hichi
 
Soma kila kitu ndio upost. Mimi sija sema CCM ni wajamaa. ila walijikwaa kutoka kwenye ujamaa na sasa wanajirekebisha.
Huelewi nini sasa?
Wanajirekebisha...! ujamaa unaufahamu au unausikia tu!
Wameanzia wapi ndugu yangu
Kumbe wewe bado unaifahhamu CCM ya wakulima na Wafanyakazi.
Looo! siku hizi ni ya Mabepari bwana. Wala hauhitaji kuwaza ili kujua hilo.
 
  • Labda utusaidie makubaliano ya chini kwa chini maanake nini? halafu lile fundisho kuwa hawapaswi kuhoja mambo ya mkwanja yalitolewa wapi? Tupe data ili nasi tuelimike na kama unadanganya ufe mwaka huu kwa ajali ya kujitakia
 
Chadema ni chama kilichoanzishwa kwa mfumo wa kibepari. Kwahiyo Msingi mkuu wa chadema ni ubepari.

Khaaa, kwani kuna ubaya gani? ,Mbona mfumo tulionao sasa hivi ni ubepari tayari, wewe bado unadanganyika na sera ya ujamaa ya CCM? UNAFIKI.

Mwanzilishi wa Chadema ni Mzee Mtei ambaye alitofautiana na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwani Nyerere ni Mungu ambaye mawazo yake hayapingwi?

Tofauti yao ni kuhusu sera za IMF Mtei alikuwa anaunga mkono bali Nyerere alikataa sera za kibepari.

Mbona sasa hizo sera ndizo tunazozitekeleza, licha ya kwamba Mtei hakuwahi kuwa Rais wetu.

Kwahiyo Sera za kibepari msingi wake mkuu ni mtaji (Pesa).

Offcourse!!!

Kimekuwa kikipata misaada ya chini chini kutoka katika nchi za magharibi kama Uholanzi na zingine

Si afadhali ya hawa kuliko Chi Chi EM iliyotuibia pesa zetu za EPA.

kitendo ambocho kinanipa mashaka kuwa vipi pesa hizo zitalipwa. Ninadhani kuna makubaliano ya chini kwa chini ambayo watu wengi hatuyajui

Mbona hujahoji ni vipi Chi Chi EM watalipa pesa za wavuja jasho wa Tanzania.

CHADEMA kimejitahidi sana kuwafundisha wanachama wake kutohoji mapato na matumzi ya chama. Hii ni mbinu ambayo imetumiwa na CHADEMA kuwaaminisha wanachama dhidi ya viongozi kuwa wao hawana doa.

Hatuna muda wa kupoteza kuwahoji viongozi wa CHADEMA huku tukijua ADUI yetu ni CCM!
 
Signature yako na ulichokiandika vinarandana kabisa sasa sijui tukusaidieje maana hata ukibebwa hubebeki umekosea kujiunga JF tafuta mtandao mwingine hapa sipo pahala pake... Pole sana ndugu!!

Mama sikiliza kama kunakosa liseme sio kusema nimekosea kujiunga JF naomba unijibu kwanini?
 
Chadema ni chama cha kidemokrasia? Mbona wachina ama nchi nyingine hamshangai? Je? hao rafiki zao wa Democratic Parts wakiwamo akina obama na akina fulani conservative hamuwajui? Mamluki hawezi akajichanganya wazi vile, kitu kizuri hakifanyiki kizani?Hiyo ndio CDM, usingeishia kuwapiga picha tu ungejua wanatokea mbali? Ongeeni hoja za Msingi Kama zile za kusafirisha twiga na madawa ya kulevya, uuzaji wa ardhi na binadamu pamoja?
 
Yan katika watu wana openda kutafuta maneno we unaongoza!
Kwa hiyo nyiemu ni chama cha kijimaa?
Yan sikuhizi we unafanya kazi ya kuichafua cdm.

Narudia tena,hatuyumbishwi na maneno ya kizushi na yasiyo na msingi kutoka kwa watu wepesi kama wewe.
 
Sisi Watanzania "SIO CHADEMA" hatutaki ubepari pili tunataka tuelewe historia ya CHADEMA na kwanini ilianzishwa tatu Mtupe maelezo ya kutosha kwanini Mtei ashindwane na Nyerere? Na nchi ya Uholanzi inafadhili chadema kwa misingi ipi?

Kuhusu CCM nani asiye jua Historia yake? Ni muungano wa vyama viwili TANU na ASP ili kuimarisha muungano.

Acheni kuongea tu LAZIMA MKIELEWE CHAMA CHENU VIZURI SIO KUPELEKWA.

umejitaidi kupoteza muda kwa kumwaga pumba, wewe unafuata mfumo upi baada ya ujamaa kuzikwa? Chengeism, Rostaism, au Lowasism. maana ndio wenye chama nyie ni maboya tu. Hata hivyo chama chako gambas au chukua chako mapema mfumo huu wameukubali kwa kuwa wamechuna wamechuma, madini yote kwa kumtumia Mr. Safi, kutukiwa na kutumeremeta na nchi kubaki mashimo.
 
Ndugu Anael, waweza kunisaidia sasa hivi chini ya utawala wa CCM Nchi hii tunafuata mfumo gani?
 
Khaaa, kwani kuna ubaya gani? ,Mbona mfumo tulionao sasa hivi ni ubepari tayari, wewe bado unadanganyika na sera ya ujamaa ya CCM? UNAFIKI.

Kwani Nyerere ni Mungu ambaye mawazo yake hayapingwi?

Mbona sasa hizo sera ndizo tunazozitekeleza, licha ya kwamba Mtei hakuwahi kuwa Rais wetu.

Offcourse!!!

Si afadhali ya hawa kuliko Chi Chi EM iliyotuibia pesa zetu za EPA.

Mbona hujahoji ni vipi Chi Chi EM watalipa pesa za wavuja jasho wa Tanzania.

Hatuna muda wa kupoteza kuwahoji viongozi wa CHADEMA huku tukijua ADUI yetu ni CCM!

Hapa siongelei CCM wiki ijayo nina anza na CCM subiri
 
Back
Top Bottom