Ubepari tatizo lake ni kwamba mwenyenacho ndie anayepata na siye nacho ataendelea kuwa mnyonge.
Ni tofauti kabisa na mfumo wa kijamaa.
Jaribu kujikumbusha Uraia au siasa darasa la tatu shule ya msingi.
Yes theoretically that's how it's. Is so practically na kwa mazingira ya Tanzania? CCM inajinadi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kinafuata ujamaa.Hivi kivitendo ndivyo ilivyo na hali waliua Azimio la Arusha ambalo lilikuwa linahubiri utu kuwa ni marufuku mtu mmoja (mwenye nacho) kumnyonya mtu mwingine (asiyenacho) kwa njia nyingi kama kumfanyisha kazi kwa malipo duni au bila malipo. Azimio limetupwa na aliyeliahsisi kabla hajafa alisema kulitamka Azimio la Arusha unahitaji roho ngumu kama mwendawazimu.
CCM ndiyo ya kusitikitia ambayo inaishi katika unafiki na uongo wa kuogopwa maana inaendesha mambo kibepari kwa kumilikisha raslimali zetu kwa wageni na huku imejificha chini ya kivuli cha ujamaa. Quite pathetic ukiona tasisi inashindwa kusimama kwa miguu yake miwili na kuwa wazi inaendesha mambo kwa falsafa ya popo huku anataka kuwa mnyama (ujamaa) huku ndege (ubebari). Hypocricy at work