Unapompinga Rais Magufuli, unapinga yafuatayo

Unapompinga Rais Magufuli, unapinga yafuatayo

Ungelikua umeelimika ungefahamu tofauti kati ya majukumu ya raisi na majukumu ya serikali? huwezi kuisifia serikali inajenga fly over, au inajenga barabara hayo ndo majukumu ya serikali, raisi apingwe asipingwe hivyo vitu vinatakiwa kutekelezwa cha ajabu 98% wana akili kama zako kidhani kwamba serikali kutekeleza majukumu yake ni kama favour au fadhila...

Ni kweli ila sasa lazima watu wasifu kunpokuwa na outstanding records, zinazoambatana na utendaji wa Serikali ya Magufuli. Kwa mfano, mtoto aliyefaulu kwenda kusoma shule nzuri ila ni ya bure, halafu baba akiamua kumpeleka kwenye shule nyingine ya kulipia tena kwa gharama kubwa, hiyo ni outstanding recoord kwa maana kuwa huyu mtoto kwa kiasi kikubwa inabidi amsifu baba pamoja na kuwa ni jukumu la baba kumsomesha mtoto wake
 
Mimi simpingi kwenye haya, ila kwenye uhuru wa habari na mitandao bado kuna kasoro, pia ajaribu kufanya yale ya maana kwanza kuliko kuonekana mlaini kwenye mambo fulani lakini mgumu kwenye lingine lilol dhahiri lianze..
Bado kelele za vyama vya Upinzani zinarindima, aliangalie hili, upinzani ni chachu ya maendeleo, sisemi wakivunja sheria wasishughulikiwe ila nasema kunaoenekana kuna kutumia nguvu za dola na siyo za hoja kwenye hili..
Unakula mitandao??

Ingekuwa mitandao imefungiwa ungekuwa unatype hapa?
 
Uchaguzi wa Tanzania mwaka 2015 uliacha historia kwa sababu ulikuwa uchaguzi wa mabadiliko. Wagombea wote waliimba mabadiliko na wananchi tuliimba mabadiliko.

Naam, kila aombacho mtu ndio hupewa uchaguzi uliisha na mabadiliko yalipita.
Baada ya uchaguzi kuisha na Magufuli kutangazwa mshindi limetokea wimbi la kupinga kila kitu.
Hadi mabadiliko waliyoyalilia na kuzungusha mikono wanayapinga.!!!

Kumpinga Rais Magufuli ni kupinga yafuatayo.

1. Elimu bure. Hao wapingaji hawataki watoto wasome bure kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari.

2. Machinga kufanya biashara kwa uhuru. Kabla ya rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa adhabu ,kupigwa na kuibiwa mali ilikuwa ndio maisha ya machinga.

3. Ujenzi wa flyover kila kona.
4. Kupanda kwa makusanyo ya mapato.
5.Maelfu ya wanafunzi kupata mikopo.
6.Nidhamu na uwajibikaji wa watendaji wa serikali kuongezeka.
7. Serikali kuhamia dodoma.

8. Vita ya rushwa na ufisadi na wakwepa kodi wa billicanas na bandarini.
9. Kodi kufutwa
10. Wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wanafukuzwa kama mbwa sasa wanatajirika .

Anayeyapinga hayo hawezi kushinda uchaguzi ndio maana kwenye kata zote wanaishia kushinda kata moja tu.

Dhambi ya kupinga kila kitu haitawaacha salama.
Tuanze na elimu bure. Ni shule gani inatoa elimu nipeleke mtoto wangu?
 
Unakula mitandao?? Ingekuwa mitandao imefungiwa ungekuwa unatype hapa?
Siyo jibu zuri kama kweli wataka kujenga hoja, ila sishangai, kukosolewa siyo kupingwa, hili likiingia kwenye vichwa hasa kwa wale wanaofikiri wao ni CCM zaidi kuliko wenzao wanakosea, ila majibu kama hayo tayari yanakuweka katika hali ya kutokutaka kuchambuwa mambo..Napenda Polepole anavyojibu hoja, tukimuiga mbona discussion na debate zitakuwa na afya zaidi kuliko kujibu kwa mihemko..
 
Nina wasiwasi na kiwango chako cha kufikiri wewe mwenye post. Kwenye namba 9 unasema 'kodi kufutwa'. Hivi kweli Tanzania imefikia point ya kufuta kodi, sasa serikali itajiendeshaje bila watu wake kulipa kodi? Mtoa post are you serious or you are just joking?

Namba 7, unasema 'serikali kuhamia Dodoma'....so what? Unataka nini nishawishike kwa hili hadi niukubali utawala huu wa awamu ya 5? Je, kuhamia Dodoma kuna-affect vipi maisha ya Mtanzania ya kila siku?

Namba 3, unasema 'ujenzi wa fly-over kila kona'...hivi unajua maana ya 'kila kona'? fly-over ya TAZARA inayojengwa sasa na ingine ambayo bado haijaanza rasmi pale Ubungo ndizo fly-over pekee kujengwa Tanzania nzima. Sasa hii phrase ya 'kila kona' umeitoa wapi? Unajua kuna vitu unaweza kudhani unamsifia kumbe unamdhihaki!!

Hatukatai kumsifia, ila msimpe sifa asizostahili. Kumbuka kusifusifu sana ni dalili kubwa ya unafiki na wala hautakusaidia kitu. Mungu pekee ndiye anastahili kusifiwa kwa kila jambo, na wala si mwanadamu kama wewe na mimi. Kumbuka, sisi wote ni wadhaifu hakuna kati yetu aliyekamilika. Hata mimi nina madhaifu yangu, sijakamilika. Hata wewe ni dhaifu una mapungufu yako haujakamilika. Hata muanzilishi wa JamiiForums ana madhaifu yake hajakamilika hiyo ndiyo sifa ya mwanadamu.
 
Naona hujui mambo wewe kati ya awamu ya nne na awamu ya tano ni wapi wanufaika wengi wa mkopo walinufaika?Vipi unaunga mkono kuzui bunge live mkutano ya baba jesca live huku akiongea uongo uliotukuka? Mfano sukari 1kg kwa 5000 wapi na mwaka gan?
 
Naona hujui mambo wewe kati ya awamu ya nne na awamu ya tano ni wapi wanufaika wengi wa mkopo walinufaika?Vipi unaunga mkono kuzui bunge live mkutano ya baba jesca live huku akiongea uongo uliotukuka? Mfano sukari 1kg kwa 5000 wapi na mwaka gan?
Unakula bunge live?
 
ndg wana jf mtanzania mzarendo n yule mwny kupongeza na kukosoa jambo fulan lakn kupongeza Mara nyng kunakua moyon it means hakuna asiyejua baadh ya kaz ngum alzofanya MKUU lakn kukosoa kunakua mkonon ili kumfanya mkosaj kujrekebxha mapema xo tucpenfe kucfu xana kla jambo maana kunaweza kumbwetexha MTU akasahau majukumu yake
Hiyo ni lugha gani mkuu
 
Buguruni pia lipo. Na huku kwetu Ngopyolo pia limejengwa. Hatupiti tena kwenye fiteputepu (yale madaraja yajengwao kienyeji, yananesaje!!)
We jamaa utakuwa mnyakyusa fiteputepu hahaha nimecheka kwa sauti
 
Back
Top Bottom