mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,468
- 6,016
No Ninapinga utekaji na uuaji usio na hurumba kwa wapinzaniUchaguzi wa Tanzania mwaka 2015 uliacha historia kwa sababu ulikuwa uchaguzi wa mabadiliko. Wagombea wote waliimba mabadiliko na wananchi tuliimba mabadiliko.
Naam, kila aombacho mtu ndio hupewa uchaguzi uliisha na mabadiliko yalipita.
Baada ya uchaguzi kuisha na Magufuli kutangazwa mshindi limetokea wimbi la kupinga kila kitu.
Hadi mabadiliko waliyoyalilia na kuzungusha mikono wanayapinga.!!!
Kumpinga Rais Magufuli ni kupinga yafuatayo.
1. Elimu bure. Hao wapingaji hawataki watoto wasome bure kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari.
2. Machinga kufanya biashara kwa uhuru. Kabla ya rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa adhabu ,kupigwa na kuibiwa mali ilikuwa ndio maisha ya machinga.
3. Ujenzi wa flyover kila kona.
4. Kupanda kwa makusanyo ya mapato.
5.Maelfu ya wanafunzi kupata mikopo.
6.Nidhamu na uwajibikaji wa watendaji wa serikali kuongezeka.
7. Serikali kuhamia dodoma.
8. Vita ya rushwa na ufisadi na wakwepa kodi wa billicanas na bandarini.
9. Kodi kufutwa
10. Wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wanafukuzwa kama mbwa sasa wanatajirika .
Anayeyapinga hayo hawezi kushinda uchaguzi ndio maana kwenye kata zote wanaishia kushinda kata moja tu.
Dhambi ya kupinga kila kitu haitawaacha salama.
Ninapinga ufisadi mpya wa kuiba fedha za umma ili kuharibu utawala bora na demokrasia. Ni ufisadi usiovumilika wenye kichefu chefu. Wizi mwingine wowote pamoja na ubaya wake unaishia kuleta maendeleo angalau kwa wachache! Lakini huu unaoishia kuharibu demokrasia na utawala bora!! ni unyama