Unalijua eneo la siri zaidi duniani Area 51?

Unalijua eneo la siri zaidi duniani Area 51?

Ni vigumu kumtenganisha binadamu na ushirikina naona dunia nzima imeathirika na hii kitu.kule wanaita aliens huku vibwengo
 
Kama ni hivo basi lile season la 'V' , muvi la Avengers na Guardians of the Galaxy yana ukweli ndani yake
 
Mambo ya ma allien na mambo ya uchawi wa matunguli ni vitu ambavyo nitakuwa wa mwisho kuviamini baada ya dunia nzima kuamini
Yap UFO huko ulaya ni sawa nyungo, fisi, na matunguli ya huku Africa, wakati wachawi wa Africa wanaweza kupanda ungo tu na kuzunguka ndani ya kijiji wenzetu ulaya wanapanda UFO na kupaa ata nje ya dunia
 
Haya mataifa makubwa yana siri nzito sana, Movie hasa za Marekani sikuzote zina akisi kitu kilichopo au kilicho katika utafiti.. Wana vifaa vya ajabu Sana ambavyo nchi zetu tutasubiri miaka billion 1000 kuja kuvitengeneza
Kabisa mkuu we angalia limuvi kama Avengers na Guardians of Galaxy na pia lile season la Vs, inaendana kabisa na yanayosemwa hapa
 
Niliwahi kusoma historia flani ya zamani kuwa...
Aliens, wakiwa ni viumbe wa angani wenye akili na teknolojia kuliko binadamu wote walishaishi kwenye baadhi ya sayari lakini hali ya hewa haikuwa sufficient kwao.

Kuanzia miaka ya 1200's Aliens walianza kuwa na uhusiano na Binadamu wa sayari hii ya Earth ili wapate makazi duniani.

Viumbe hao + jamii ndogo sana ya kabila la dogon huko mali ndio waliotengeneza kaburi la Farao Khufu na wake zake.

Teknolojia yao iko juu sana na ndio siri ya teknolojia ya wamarekani na waingereza, hata ugunduzi wa ndege, rockets, computer una mchango wa asilimia kubwa sana kutoka kwao.
Zamani nilisoma kitabu cha George Adamski; "Inside a Flying Saucer". Kinaeleza jinsi huyu bwana alivyokutana uso kwa uso na viumbe hao. Ana kitabu kingine aliandika ila sikubahatika kukisoma "The Flying Saucer has Landed". Raymond Drake, mwanahistoria wa Uingereza naye ameandika sana juu ya haya katika vitabu vyake: "God and Spacemen in the Ancient East" na "Gods from the Outer Space". Huyo Adamski anaeleza juu ya mkutano wake na Orthon kutoka Mars. Baada ya muda kadhaa George Adamski "alitoweka". Inasemekana alienda kuishi huko kwao Orthon.
 
UFOs ni vyombo vinavyoundiwa hapahapa duniani..kufichwa kwa habari zake hapa duniani ni ili watu wazidi kujua kuwa ni kweli kuna aliens waishio katika sayari zingine kitu ambacho ni bullshit nonesense...hao aliens ni majini ila wanasayansi hawataki kuwataja kwa majina yao halisi bali hutuzuga kwa kuwaita aliens ili wawe tofauti na maandiko ya kidini...
kuna videos za UFOs zikizinduliwa na binadamu katika you tube tafuta kuhusu flying saucer...hii ni story ya kweli kabsa siyo kitu cha kuutungwa...flying saucer zilikuepo tokea enzi za zamani sana.katka vita vya dunia..cha hatari kuhusu hivi vyombo vya anga ni kwamba vina spidi ya ajabu...vipo kama nyuki kinaweza simama angani na kutoweka ghafla...
 
Ukweli Ni kua nchi za wenzetu washaendelea hawaoni tabu ku invest katika hizo tafit za kufikirika ..haijawai kusibitishwa kua kuna viumbe nje ya dunia..alieumba ulimwengu kasema tuko sisi Na majini basi.ila wazungu hawataki huo ukweli
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nachunga mbuzi na kondoo kijijini!!
Nilipokuwa nachunga kuna kipindi nilikuwa naona maruwe ruwe angani!!
Yaaan vitu vya ajabu vinatembea kwa spid ya hatari
Nakumbuka kuna kimoja kilitua jiran nilipo kwa vile nikiuwa na akili za kitt (7yrs)
Nikabaki nashangaaaa but nilijificha nyuma ya majan na vimiti
Bhas vikatokea viumbe vifupiiiiiii na vya ajabu yaan hata hawaeleweki maumbo yao! Nilikuwa sijuh kuhesabu(sikuwa naenda shule nashinda porini)
Lakin kwa kusika now nadhan walifika wa 3/4
Wale viumbe walikaa pale kwa muda wa dk kama 10!
Nakumbuka walifukua chini wakatoaa kitu na kuondoka!!

Kama kawaida nilipofika home nilimwambia mzaz lakin kutokana na mambo ya kijijini(mila zimetawala)
Wakasema.n mambo ya mizmu so wakanifanyia tambiko!
But..
Nitaendelea
 
Back
Top Bottom