Rais Samia awamiminia vyakula wakazi wa Rufiji

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,435
Reaction score
26,159
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge amewamiminia mamia ya tani ya vyakula wakazi wa Rufiji walio athirika na mafuriko ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha na zinazotabiliwa kuendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini.

Ambapo Rais wetu amewapatia Tani 150 za unga wa mahindi,Tani 50 za maharage pamoja na mafuta ya kupikia lita 5000. Rais Samia ametoa msaada huo kwa kutambua kuwa wanarufiji wanahitaji misaada na mkono wa pole na faraja.

Siyo mara ya kwanza kwa Rais Samia kufanya hivi, maana amekuwa akifanya hivi mara nyingi kwa watu mbalimbali katika maeneo mbalimbali pale wanapokumbwa na Changamoto za aina yoyote ile.Rais samia ni kiongozi mwenye huruma na upendo mkubwa sana,ni kiongozi anayeguswa na shida za watu,ni kiongozi mwenye moyo wa ukarimu.

Kwa hakika ni mama wa Taifa,mama mlezi wa Taifa na mfariji wa Taifa letu.ni kiongozi mwenye moyo wa kujali na kujitoa sana .ni kiongozi anayestahili kuendelea kutuongoza Watanzania,kwa sababu ni kiongozi anayeguswa na mwenye uchungu na maisha yetu.

Rai yangu nawaomba viongozi wengine kuanzia mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya,wakurugenzi ,wabunge ,wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,wakuu wa taasisi,idara mbalimbali za serikali,taasisi binafsi, wawekezaji,wanamichezo ,vyama vya siasa na makundi mengine mbalimbali kumuunga mkono Mheshimiwa jemedari wetu kwa kutoa misaada na kwenda kuwapelekea wana Rufiji.

Amkeni na simameni kuonyesha upendo wenu kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na kubeba mlicho nacho mikononi mwenu kuwapelekea wanae na wajukuu zake kule Rufiji,ili kuwapa pole na faraja.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
IMG-20240410-WA0017.jpg
 
Hapo wahakikishe ndizi za kuiva na pilipili wanatembea nazo mfukoni, mambo ya msosi mama kamaliza
 
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2960519
well done madame president comrade Dr.Samia Suluhu Hassan,:KasugaYeah:

kazi kwa maarifa na bidii sana, utu wa watu na ubinadamu kwanza :ClapHD:
 
Lilikuwa suala la muda tu Mama Samia kuchukua hatua. Ni tabia ya Rais Samia kuguswa na shida za watu hasa kwenye majanga kama haya ya kiasili. Wakazi wa kijiji cha Kipwa hawatakaa wamsahau alivyowatendea baada ya kijiji chao kumezwa na maji ya ziwa Tanganyika. Mungu ambariki sana Mama Samia.
 
Back
Top Bottom