Unajisikiaje mara ghafla mke wako anavyoanza kuonekana mkubwa zaidi kuliko wewe?

Sijui kwann mimi sinaga hii mitizamo. Miminyf akonde labda ndio nitashtuka. Akininenepa au kufumuka hata sioni tabu. Acha tu aishi anavyotaka maisha haya sio kilankitu cha kukijali muda woote uko makini kama nurse wa zam shift ya usiku..Mwache ajiachie..avae anavyotka ale anavyotaka afanye anavyotaka.. kuna muda maisha hayakupi hii option.
 
Mambo ya kuachana na Mke miaka 2 ndio hayo sasa, utofauti uanzie angalau miaka 7 kwenda juu.
Ahahahah... what is wrong with the age??? Mimi sijawah kuona shida hata.

Yf mimi alinipiga kamba wakat tunaanza relationship 2010 kuwa na yeye pia kazaliwa 1989 kumbe baadae nikaja kugundua kazaliwa mwaka 1988. 😂😂.

Bas unafikiri hata kuna shida naionaga kuhusu umri!? Walaaah!!. Age is just a number bwana. Tunaishi tu hata hatusumbuki na minor issues kama hizo. Kanizalia watoto wa4 na bado namuona yuko fiti tu
 
Tunzeni wake zenu wapendeze,ushamlaza kifua kimekuwa kama ndala za gesti halafu unasema kazeeka .

Mwanamke akishazaa basi mwili unafumuka kwa kasi na kadri anavyoendelea ,kama ni mnene angalia avae zile nguo ndefu jamii ya abaya na sio za mtumba ,tafuta angalau za bei mbaya zinapendeza kwa wanawake angalau 150k .

Manukato safi hata afike 50 utamuona kawaida ila kama humtunzi na hali za umaskini lazima awe kikongwe.
Manukato safi hata afike 50 utamuona kawaida ila kama humtunzi na hali za umaskini lazima awe kikongwe..

😄😄,
 
Ni matunzo tu..Wakati nchi zilizoendelea Wanawake wembamba ndio wanakimbiza soko la udangaji na kuolewa.huku bongo Mitukunyema yenye miswambwanda ETI ndo wanakimbiza Soko kiasi kwamba wanawake hawapati usingizi wanawaza kuongeza shape..!

Wengi hawajijali ni kusaka pesa na vicoba mwanzo mwisho..Gym inaonekana umalaya huku kwetu..Akishajifungua ndo kabisaa anajiona kashazeeka anaanza kujifunika na mavitenge na nguo za kushona..Hawazingatii Diet wala nini..Anaamka na mihogo analala na Ugali.mara chips kwa wingi hii yote ni mfumo wa maisha tuliyochagua

Kazi kwelikweli/ Job true true
 
Habari wana JF, Poleni na majukumu ya hapa na pale 🤝,
• Nimekuwa nikifikiria na kufuatilia hili kwa miezi kadhaa sasa, nimeona mke wangu si tena yule mrembo niliyemkuta na kumtongoza.


• Atafikisha miaka 35 hivi karibuni, na tumepata watoto wawili pamoja, Lakini ni kwa nini ghafla anaonekana kuzeeka zaidi ya umri huo, ndicho sikielewi.


• Nimeona wanawake na marafiki wa umri wake bado wanavyoendelea kuwa wabunifu na kufuata mtindo wa mitindo ya maisha, lakini mke wangu hafanyi bidii tena kuchukulia mitindo kwa uzito.


• Anavaa nguo yoyote ile, bila kujali tukio. Huenda hamtanielewa kuhusu hili, kwa sababu zamani alikuwa anazingatia haya kabla hatujapata mtoto wetu wa kwanza. Labda tuseme maisha magumu, sikweli, hapitii kwenye mazingira magumu, maisha yetu ni ya kutosha namlisha vizuri kila siku.


• Hivi ni nini kinachoendelea??
• Wanaume mlio oa, mnahisi hivi pia kama ninavyo hisi mimi?, Namaanisha wale waliooa kwa miaka 5-10 na zaidi.


........ Hadithi ya kijana aliyefunga ndoa miaka 11 iliyopita." 😎.
Sasa si umweleze yeye sisi unatueleza itakusaidia wewe nini😎
 
Back
Top Bottom