Unaishauri vipi serikali kuhusu hizi picha.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaishauri vipi serikali kuhusu hizi picha..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Indume Yene, Jan 7, 2009.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nimekutana na hizi picha mtandaoni ambazo zimepigwa hapa nchini Tanzania. Hizi picha si za kuvijunia hata kidogo. Na hili suala si lazima mtu aende darasani kujua ni makosa kumruhusu mtoto kunywa kilevi cha aina yeyote kama hajafikia umri wa miaka 18.

  Katika hizi picha Mama mzazi wa huyu mtoto anaonekana kama kufurahia ustadi wa mwanae kufakamia bia.

  Wewe ndugu Mtanzania na mwanaJF una ushauri gani kwa serikali juu ya hizi picha. Ni hatua gania mbazo zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Mzazi wa huyu mtoto au mmiliki wa sehemu walipokuwa wanaburudika. Fungua hapo chini utaona hizo picha
   

  Attached Files:

 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huyu mwanamke anapaswa kufunguliwa mashtaka
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  [​IMG]
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Serikali ina lawama zake hata sisi wazazi tuna lawama. Japo sishauri kunywa pombe, lakini kuna sheria tunazivunja tukiona. Mfano, Serikali ina sheria ndogo ndogo za kuzuia kelele kama sauti za disko katika makazi ya watu, sababu ni usumbufu kwa wazee, watoto, wagonjwa hata kwa walio wazima (wenye afya) sababu ni usumbufu wanapopumzika. Lakini nani anazifuatilia hizi sheria, kila kona kuna vilabu vya pombe na mziki kwa kwenda mbele. Kuna wale wa kufanya matangazo ya biashara (promotion), siku hizi wanaweza weka kambi sehemu, tena katika makazi ya watu na kupiga mziki hadi asubuhi. Hivyo sheria nyingi tuliowapa dhamana ya kuzisimamia wala ni kama hawazioni.

  Upande wa sisi wazazi, siku hizi mfumo wa kulea mtoto kama wa jamii unaondoka. Zamani ilikuwa mtoto ni wa jamii, ukifanya kosa unapewa adabu na mtu mzima, na ukirudi nyumbani ukisema ama wenzako wakiripoti kuwa ulipewa adabu, unapata karipio linine toka kwa wazazi. Hata waalimu walikuwa na usemi mkubwa sana na kujua udhaifu wa kila mtoto na kujaribu kwa kila njia kumnyoosha. Lakini sasa ukiona mtoto anafanya kosa ukampa karipio, usishangae wazazi wake kukufuata na kukwambia "zaa wako umkaripie", "wakaripie wakwako" nk. Hata waalimu wakitoa adhabu hupata matatizo kwa wazazi. Hata wazazi kuambiana ukweli juu ya watoto nayo imepungua kwa sababu hizohizo, mzazi mwingine kuja kukwambia naona mwanao anapotea siku hizi ni nadra. Wazazi haohao wanaenda katika kumbi za starehe usiku mpaka majogoo na watoto wao,

  Hivyo, kwa Serikali ijaribu kufuata sheria tulizojiwekea, na sisi wazazi tujaribu kuwalea watoto wetu kijamii, mtoto wangu ni mtoto wa wanaJF, na watoto wa wanaJF ni wanangu.
   
 5. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Naamini Afande Kova au IGP Mwema wana mahudhurio mazuri hapa jamvini ingawa kwa kificho. Picha wanaziona, wanachotakiwa ni kumshughulikia huyu Mama kwa mujibu wa sheria.
   
 6. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Mie naona kama ni geresha tu, maana kweli the child is as mlevi as he seem to be tena in public then nashangaa ni kwa nini bado vijana wa saidi mwema hawajamsomba mzazi wa mtoto huyo au yeyote aliyekuwa responsible na mtoto huyo. Ingawa huenda hata serikali haina sheria yeyote ya kuwa protect watoto na ulevi assuming kuwa watoto hawanywi pombe. Of what irritates me in kuonesha hadharani, wengine lukuki watadaka hiyo kuanza kuwa wabwia ngano. TOBA!!
   
 7. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ndiyo madhara ya kusherehekea sikukuu, huyu mama alifanya makosa na naamini hata yeye mwenyewe alikuwa kalewa. Kwa mzazi mwenye busara huwezi kufanya ujinga wa namna hiyo.
   
 8. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kosa si kusherekea sikukuu bali kumwachia mtoto na kuserebuka na kilevi. Kusherekea sikukuu si lazima upate kilaji, tatizo ni jinsi unavyoitumia nafasi kama hizo kufanya madudu.
  Huyu Mama anatakiwa hata kunyang'anywa huyo mtoto na kumpeleka Ustawi wa Jamii. Anaweza akawa anachekelea kumuona mwanae anabwia unga kama aliona kawaida kwa Mwanae kuserebuka na kilevi.

  Hii tabia tusiiruhusu katika jamii zetu. Najua kwa nchi za wengine kama Europe na US huyu mama angekiona cha moto kwa tabia yake hiyo ya kumwachia mwanaye kufanya hivyo.
   
 9. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa hapa chini naye ameweka ulabu kwenye chupa ya mtoto ya kunyonyea maziwa. Huyo mtoto naye ana chupa ya bia, ila sijui kilichopo ndani yake (maybe yamo maziwa !!). Hebu waangalie wote na ulinganishe. Sasa tusemaje, tuhoji hivyo "vyupa" walivyoshika au vimiminika vilivyomo ndani yake?

  [​IMG][​IMG]
   
  Last edited: Jan 7, 2009
 10. Modereta

  Modereta Senior Member

  #10
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Labda tuangalie ni nani mwenye jukumu la kwanza, tukikumbuka methali ya kiswahili "asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu" hivyo ni baada ya mama kushindwa ndio akina serikali watakuja. Hata ukimshika ukamfunga huyo mama au akalipa faini kama yeye mwenyewe anaamini kuwa yuko sawa basi atakachofanya ni kuhamisha mahali pa kufanyia hayo, ndio maana pamoja na serikali kuwa na sheria ya kuzuia kinywaji "kitamu" cha gongo, bado kinashamiri kwa vile wahusika hawajijali. Tuanze na kuwaelimisha Wazazi kuhusu malezi maana ndipo tunapanga maisha yetu ya kesho, huwezi kupanda ndimu uvune machungwa, walimu wanalazimishwa kutengeneza mazezeta (mwezi Octoba 2008, mwalimu mmoja alimfinya mtoto wa kigogo mmoja asubuhi ya saa 4, saa 11 baba kaja chukua kabomu kake kakuta kanalia, kisa!!!!!!!! mwalimu kanikata na kisu, WAPI???? (maana alipokatwa hapaonekani) anaonyesha mahali hata alama ya ukucha hakuna, kesho yake asubuhi Baba na mama wakafunga safari kwa mwalimu mkuu, "nionyeshe huyu mwalimu, utakosa kazi, nitamfundisha adabu huyu mwalimu..........." bahati nzuri huyu mwalimu mkuu ni sawasawa, akamwambia sitakuonyesha na kama hutaki mtoto wako aguswe hata akikosa sasa hivi mchukue mtoto wako sasa hivi peleka huko kunamkomfaa...... Wakatoka mkuku na mtoto wao wakaenda polisi, nako wakaulizwa alama ya kukatwa iko wapi "ilikuwepo jana" inabidi ucheke lakini NI SISI WAZAZI WA SASA NDIO MABOMU, Tufanyeje?????????
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu mama atakuwa Mnyalu au Mbena kule ndo zao hiki kitu ni cha kawaida sana mpaka vichanga vinanyweshwa ulanzi au comoni au msabe vilale usingizi au wavichangamshe lengo lao kuu mala nyingi iwa linakuwa walale ili walime sana wazazi au wafanye shughuli sana.
  Mkoani Iringa kitu hiki si cha kushangaa saaaaaaaaaaana ni kawaida tu mtoto kushtua homone.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kuna ka imani ka ki-albinoalbino hivi kwamba watoto wakionja pombe katika umri huo ukubwani hazitawasumbua!
  Pili, mbona mambo haya yanafanyika tangu zamani kwenye pombe za kienyeji? Au wengi wenu humu mmezaliwa WODINI?
   
 13. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Mambo ya teknolojia hayo .... kila kitu "digital" kwa hiyo ni rahisi kupiga picha na kui-upload bila wasiwasi. Huko nyuma hizi picha hatukuziona kwa maana ukishanunua "mkanda" (film??) wako, unahesabu ngapi zimebaki kabla ya kupiga picha za kihasara hasara kama hizi hapa!!!
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mkubwa unamaanisha nini katika hiyo red? Nadhani umetoka nje ya uungwana na ni vema ukaomba radhi kwa kupotoka katika lugha uliyotumia
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  really? kuna watoto 4 wamelipuwa bomu kule moshi, 19 wamekufa Tabora...
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu anamaanisha kuwa ni imani potofu ndilo lengo lake na si vingine.
  Yaani kama ilivyo kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi watu wana imani potofu.
  Lakini watoto wanayweshwa sana pombe za kienyeji vijijini na ni jambo la kawaida sana la halishangazi.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kamanda kumbe upo???
  Mi nilifikiri umekubwa na dhoruba kali ukatoweka gafla kama ilivyo kawaida hapa JF.Tunauliza cheche vp mbona kimya?
  Naona hata CCM nao wanataka kukuiga wanatoa cha EPA .
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unamzungumzia mama gani? Huyo aliyeshika chupa za bia? kama ni huyo mimi sioni kosa lake kisheria.
  Au unamhusisha na mtoto anayekata kilaji? kama ni hivyo, basi ni vema ukatueleza kinagaubaga kuwa huyo mama ana uhusianao na tendo la mtoto kunywa bia kwa maana picha hazionyeshi uhusiano huo
   
 19. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Waafrica ndivyo tulivyo, madhara hatuyaoni kwani hatuko makini kabisa. Watoto hawawekewi mazingira ya kupambanua mazingira ya hapo baadaye. Tumekuwa too much globalized hata kushinda wale walioasisi globalization wenyewe maana haya huko kwao huwezi kuyaona.

  Ulevi na mwana.JPG
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  SIFA ZA KIJINGA!
   
Loading...