Unaishauri vipi serikali kuhusu hizi picha..

Huyu jamaa hapa chini naye ameweka ulabu kwenye chupa ya mtoto ya kunyonyea maziwa. Huyo mtoto naye ana chupa ya bia, ila sijui kilichopo ndani yake (maybe yamo maziwa !!). Hebu waangalie wote na ulinganishe. Sasa tusemaje, tuhoji hivyo "vyupa" walivyoshika au vimiminika vilivyomo ndani yake?

opaque-albums-op-pics-picture300-babu-ayubu.jpg
opaque-albums-op-pics-picture302-mtoto.jpg

Hata wakibadilishana hizo chupa bado kuna tatizo !!
 
Waafrica ndivyo tulivyo, madhara hatuyaoni kwani hatuko makini kabisa. Watoto hawawekewi mazingira ya kupambanua mazingira ya hapo baadaye. Tumekuwa too much globalized hata kushinda wale walioasisi globalization wenyewe maana haya huko kwao huwezi kuyaona.

Ulevi na mwana.JPG
 
Last edited:
Duu aibu sana jamani! na hapo huyo mama anajua kabisaaa kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!
 
Sijui huyu mama atashitakiwa kwa sheria ipi? (Wanaharakati/Wanasheria watusaidie) kwa tafrija nyingi nilizohudhuria ni jambo la "KAWAIDA" sana kuona wazazi au walezi wanawa-ONJESHA pombe watoto wao na sijwahi kusikia mtu akikemea hili! This has become a social norm and we are bound to accept it - either you agree or not it is there to stay!

Pakuanzia ni kufundisha jamii (INTENSIVELY) madhara or athari za vileo na kinachofuata ni kuzuia watoto kushiriki katika shughuli zenye "VILEO" na sio kuwakamata wazazi/walezi waowapa watoto vileo

**** Save water...drink beer *****
 
Kwa mtindo huu Serikali itabidi iongeze kiwanda kingine cha Bia,
 
Kwa mtindo huu Serikali itabidi iongeze kiwanda kingine cha Bia,

Naam inampango wa kujenga kingine mkoani Mbeya.Ndo bidhaa inayo lipatia taifa kodi kubwa hata madini hayaoni ndani.
 
Naamini Afande Kova au IGP Mwema wana mahudhurio mazuri hapa jamvini ingawa kwa kificho. Picha wanaziona, wanachotakiwa ni kumshughulikia huyu Mama kwa mujibu wa sheria.

Mkuu Indume Yene,si rahisi kwa polisi au vyombo vya umma kuingilia suala ambalo mtoto anaruhusiwa kunywa .Panapotokea fujo hapo dola ndo pake.
Hili ni tatizo la kijamii zaidi na ni kielelezo cha kuporomoka kwa maadili dhahiri ya kiafrika.
Nafikiri wale wanaomzunguka mtoto akinywa nao wanajukumu la kufanya, hivi wtu hawa wanapomwona mtoto kinda kabisa akinywa wanasemaje, aaah poa tu!
Basi hata polisi wakija hapo hakuna mashahidi.
 
Unamzungumzia mama gani? Huyo aliyeshika chupa za bia? kama ni huyo mimi sioni kosa lake kisheria.
Au unamhusisha na mtoto anayekata kilaji? kama ni hivyo, basi ni vema ukatueleza kinagaubaga kuwa huyo mama ana uhusianao na tendo la mtoto kunywa bia kwa maana picha hazionyeshi uhusiano huo

Inaaminika kuwa huyo Mama ndiye mzazi wa huyo mtoto. Inaaminika kuwa aliwaambia watu waliokuwa karibu naye kuwa wasishangae mwanane anaenda hadi chupa 2 na hazimdhuru kwa njia yoyote ile.
Hiki si kitendo cha kujivunia mbele ya familia na jamii kwa ujumla.
 
Hivi mnataka huyu mama achukuliwe hatua kwa sheria ipi?? wenzetu huku Europe mtoto anakuwa mali ya serikali kama wazazi wanaonekana kushindw akumlea vyema anachukuliwa na kutunzwa na serikali sasa sisi serikali yetu ya Tanzania inaashindwa kulea watoto kiasi kwamba wamezagaa mitaani huko kila kona, wasamaria wema wameamua kuchukua jukumu la kuanzisha vituo vya kulelea watoto yatima na wenye kuishi kwenye mazingira magumu misaada inatafunwa juu kwa juu, hebu jiulizeni lile saga la wale watoto wa mbagala kule liliishia wapi?? Dah ila huyo dogo mwenyewe anaonekana shujaa haswa maana ameshakomaa mapemaaa hebu cheki sura yake na muonekane wake.
 
Mkuu Indume Yene,si rahisi kwa polisi au vyombo vya umma kuingilia suala ambalo mtoto anaruhusiwa kunywa .Panapotokea fujo hapo dola ndo pake.
Hili ni tatizo la kijamii zaidi na ni kielelezo cha kuporomoka kwa maadili dhahiri ya kiafrika.
Nafikiri wale wanaomzunguka mtoto akinywa nao wanajukumu la kufanya, hivi wtu hawa wanapomwona mtoto kinda kabisa akinywa wanasemaje, aaah poa tu!
Basi hata polisi wakija hapo hakuna mashahidi.

Sina hakika kama kuna sheria inayomlinda mtoto dhidi ya ulevi wa aina hii. Kuna tofauti gani mtu anapomuingilia mtoto kimapenzi na kumpa mtoto kilevi? Kama hakuna sheria ya namna hii serikali kupitia wabunge wetu wanatakiwa kufikiria mara tatu tatu.
Kumlawiti au kumuingilia mtoto kimapenzi adhabu yake inatakiwa ilingane na hii ya kunywesha watoto vilevi kabla hata hawajafikisha miaka 18.
 
Jamani hebu tuuache huu Utamaduni wa Kuilaumu serikali kwa kila kitu hata kwa vitu vcisivyo na msingi. sasa hapo serikali inahusika nini? au unataka siziwekwe mtandaoni kwa kuwa zina sifa mbaya wakati ndio ukweli halisi?

watu wanamatatizo yao na raha zao na kila mmoja ana life style yake mimi sioni cha ajabu hapo.

Labda uulize Wazazi wa sasa tunaenda wapi ktk malezi ya watoto wetu? sio serikali jamani!
 
uchagani hata katoto kadogo kananyeshwa mbege!!!!
Avatar yako utata yaweekana mama mtoto ni meber humu kaona avatar yako kashaiwshika kumpa mtoto wake pombe tena kamuanzishia vibaya na SAFARI
 
Jamani hebu tuuache huu Utamaduni wa Kuilaumu serikali kwa kila kitu hata kwa vitu vcisivyo na msingi. sasa hapo serikali inahusika nini? au unataka siziwekwe mtandaoni kwa kuwa zina sifa mbaya wakati ndio ukweli halisi?

watu wanamatatizo yao na raha zao na kila mmoja ana life style yake mimi sioni cha ajabu hapo.

Labda uulize Wazazi wa sasa tunaenda wapi ktk malezi ya watoto wetu? sio serikali jamani!

Serikali ikiamua kuunda sheria ya kumlinda mtoto (Sijui kama ipo) dhidi ya tabia hii, mtu akampa kwa makusudi mtoto kilevi. Baadaye huyo mtu akafikishwa mbele ya sheria na kuhukumiwa. Je utasema utasema kuwa serikali imemuonea huyo mtu?
serikali inatakiwa itoe mwongozo wa kisheria dhidi ya baadhi ya mambo ya kijamii.
Mbona watu wamekuwa wakipiga kelele kuhusu kukeketwa kwa wanawake???? Kwa nini jamii isitumie staili hiyo hiyo kumlinda mtoto dhidi ya ulevi kabla hajafikisha miaka 18?

Kuna mifano mingi ambayo imepigiwa kelele dhidi ya unyanyasaji particularly kwa watoto. Tuliona hata huko Kongo, Liberia na hata Sudan jinsi watoto walivyokuwa wanatumiwa na vikosi vya kijeshi. Dunia ikapiga kelele na UN ikalizungumzia hili. Tanzania tuna baadhi ya sheria za kumlinda mtoto kama vile ulawiti n.k Kwa nini hili lisizungumziwe kwa mapana. Naelewa serikali hawezi kumfanyia mwananchi kila kitu especially kwa vitu ambavyo tunaweza fanya wenyewe. Lakini kama Serikali ikatoa mwongozo wa kulinda haki za mtoto kwa kuunda sheria, naamini watu wataweza kuwa na adabu na kuheshimu utu wa mtoto. Na cha jabu zaidi hilo tukio lilitokea kwenye Public.
 
Sina hakika kama kuna sheria inayomlinda mtoto dhidi ya ulevi wa aina hii. Kuna tofauti gani mtu anapomuingilia mtoto kimapenzi na kumpa mtoto kilevi? Kama hakuna sheria ya namna hii serikali kupitia wabunge wetu wanatakiwa kufikiria mara tatu tatu.
Kumlawiti au kumuingilia mtoto kimapenzi adhabu yake inatakiwa ilingane na hii ya kunywesha watoto vilevi kabla hata hawajafikisha miaka 18.
Mkuu Indume, nakubaliana kabisa na wewe, na pengine wale watu wazima wote walio karibu na watoto hao wakati wakinywa inabidi wachukuliwe hatua vilevile.Hili jambo lasikitisha sana.
 
Waungwana nafikiri kinachohitajika hasa ni elimu kwa wazazi wa aina hiyo juu ya swala zima la malezi na wajibu wao kwa watoto tunaotegemea wawe taifa la kosho. Magereza yamejaa kiasi huduma kwa hao waliomo ni finyu,nafasi zilizopo zisubiri mafisadi waliopo on line.
 
Hayaaa...! Mambo ya Si-Kuku-huyu...!

Harafu unategemea akiendelea hivyo baada ya miaka ishirini asiwe fisadi...!?
 
Waungwana nafikiri kinachohitajika hasa ni elimu kwa wazazi wa aina hiyo juu ya swala zima la malezi na wajibu wao kwa watoto tunaotegemea wawe taifa la kosho. Magereza yamejaa kiasi huduma kwa hao waliomo ni finyu,nafasi zilizopo zisubiri mafisadi waliopo on line.

I guess ulikuwa unamaanisha Taifa la Kesho na si Kosho.
 
Kuna ka imani ka ki-albinoalbino hivi kwamba watoto wakionja pombe katika umri huo ukubwani hazitawasumbua!
Pili, mbona mambo haya yanafanyika tangu zamani kwenye pombe za kienyeji? Au wengi wenu humu mmezaliwa WODINI?

Mmh ako ka-msemo kana utata kidogo ndugu yangu. Huwezi kutafuta neno lingine au kiswahili kina ku-Mwalusako(piga chenga)
 
Back
Top Bottom