Waraka kwa serikali kuhusu waalimu, serikali iwajali walimu

Jabali Jiwwe

Member
Jul 28, 2022
6
8
WARAKA KWA SERIKALI KUHUSU WAALIMU, SERIKALI IWAJALI WALIMU


Ni muda sasa umepita kukiwa na manung'uniko kwa walimu katika nyanja nyingi zinazohusu maslahi yao ikiwemo mishahara yao, stahiki zao na kunyima haki na kuonewa na kuchukuliwa kama watu wa shida na kila kiongozi.

Kuna haja serikali kumwangalia mwalimu kwa jicho la tatu, walimu wanapitia wakati mgumu sana katika utendaji kazi wao. Nimejaribu kuorodhesha changamoto hizi ambazo kama serikali ikizitatua hasa katika bajeti ijayo, ili mwalimu naye aone faraja ya maisha.

Baadhi ya changamoto hizo ni;

MISHAHARA
Serikali ipitie a iboreshe kwa mapana mishahara ya walimu, suala hili limekuwa tatizo kwa muda mrefu ikiwa kuna manung'uniko makubwa juu ya mishahara kiduchu wanayopewa waalimu

Mara kwa mara tumekuwa tukisikia "mama anaupiga mwingu" kwenye Elimu, lakini ukichunguza kwa kina na kwa mapana na hata ukiwasikiliza wanaosema hivyo wanaishi kutaja vyumba vya madarasa na mabweni au katika miundombinu tu, huwezi kusikia kuhusu waalimu, hata angekuwa muumini wa kuweka miundombinu basi tungesikia hata idadi ya nyumba za walimu zilizojengwa, HAKUNA!

Mwalimu ndo kiungo chs kwanza hasa katika kuboresha elimu yetu, kuna haja ya kuboreshewa maisha ya mwalimu hasa mishahara ipandishwe!!

Ni katika ualimu pia unakuta ajira mpya anayeajiriwa sasa anamzidi mshahara mwalimu aliyeajiriwa miaka minne iliyopita "just imaging".

Waalimu walioajiriwa 2019 wote mpk sasa wapo daraja TGTSD1 huku wanaoajiriwa leo wanaanza na TGTSD3

utofauti huu unafanya kuwa "discourage" walimu na jambo hili lazima serikali iliangalie kwa mapana yake

Pamoja na hili la mishahara kuwa tofauti bado maslahi mengine mwalimu anaonekana kuwa nyuma ukilinganisha na kada zingine na mwalimu sasa anaonekana katika watumishi wote waajiriwa na serikali kuwa masikini pamoja na kwamba anafanya kazi kubwa na ngumu sana ukilinganisha na baadhi ya kada na hata katika posho imekuwa hivyo, hii inaonesha mshahara kuwa mdogo kwa walimu si jambo lililo kwa bahati mbaya bali viongozi wa juu wameridhia na kuona mwalimu hatakiwi kupata maslahi mazuri.

Hii inajionesha hata kwenye majukumu mengine yanayostahili posho kama kazi maalumu kwa walimu.

Posho za marking mitihani ya taifa
Katika hizi posho ni vichekesho sana na ni jambo la aibu mno, mwalimu anakaa nje ya kituo chake cha kazi kwa zaidi ya siku 14 na analipwa shilingi laki tatu can you imagine!

Imekuwa hivyo kwa muda sasa na pengine mambo yaliharibika zaidi kipindi cha mwendazake mpk kufikia kunyima hela za safari zile za kuamkia siku ya kazi (hela ya kituoni)

Sote tunajua ilivyo na umuhimu zaidi hasa mitihani ya taifa, nadhani ndo sehemu nyeti ya msingi ya kupata wataalamu na wasomi katika nyanja tofauti tofauti katika nchi yetu, lakini wanaofanya kazi hiyo ambayo hufanya kwa moyo na kwa moyo na ufanisi mkubwa zaidi wanalipwa laki tatu.

Mfano mitihani darasa la nne, saba,form four na form six miyihani hii ndo inabeba taswira halisi ya wasomi wa nchi hii, uwe daktari, mwanasheria mkuu,kina CAG, Majaji na wataalamu wote kwa wingi wao kama nchi wanapitia mitihani hii ambayo wanaornda kui "mark" wanalipwa laki tatu.

Kisa tu ni walimu ambao jamii sasa imeanza kuwachukulia poa kama si moja ya kada muhimu katika nchi kwa sababu hata serikali imewachukulia poa walimu!!, Kama nchi tujitafakari kwa kina katika hili jambo, serikali inao uwezo tena mkubwa na haishindwi kuja na maboresho ya maana na ya kuweka historia kwa walimu!!!

Posho za kusimamia mitihani yote ya kitaifa
Jambo hili nalo liangaliwe upya, mwalmu anaenda kusimamia mtihani wa kitaifa analipwa elfu 30000 kwa siku!
Hivi mshawahi kujiuliza waajiriwa wa TRA wanalipwaje katika vikao vyao wanavyokaa kujadili "elimu kwa mlipa kodi"?? Kuna ile wanaita "PER DIEM" mnajua wanajilipa ngapi? Mnajua elimu na namna ya kupambana na ugonjwa mpya wa "murbug" katika hizo semina wanalipwaje? Unajua kikao cha maafisa kilimo kata wanavyoelekezana jinsi ya kuzuia "gugu chawi" wanalipwaje? Wanazo semina ngapi kwa mwaka??

Sitaki niingie huko sana maana ni haki yao wapate semina na wajilipe vizuri ni haki yao kabisa na hata serikali huenda inajua ukubwa wa kazi hizo na ikaacha wajilipe hivo lakini shida yangu kwanini kwa MWALIMU ishindwe kumpa maslahi mazuri? Why mwalimu? Mwalimu anasimamia mitihani nyeti ya kitaifa, mitihani ya maisha ya ya watanzania, mituhani itakayotupa watallamu wa kuhudumia nchi! Mitihani ya maisha ya nchi hii, mwalimu anapewa elfu 30 kwa siku, haya ni maajabu mengine.

Extra duty allowance
Mmeshawahi kuona au kusikia kuhusu extra duty allowance!
Posho hii ni ya mhimu mno kwa mwalimu, kuna ofisi nyingi tu na kazi kibao katika hii nchi wanalipwa posho hii, kwa lipi? Jibu ni dogo tu wanalipwa kwa sababu wanafanya kazi kwa muda wa ziada nje na muda wao wa kazi! Kweli lazima walipwe ni haki yao lakini haki hii haipo kwa walimu, haipo na wala serikali inaona kama katika list ya wafanyakazi wanaostahili kupata posho hii na walimu wamo

Kwa uchache tu;
Mwalimu anashika zamu lazima ahakikishe wanafunzi wamekula mchana na jioni sa kumi na mbili hasa shule za bweni.
  • Ahakikishewanafunzi wameingia kusoma usiku
  • Ahakikishe wanafunzi wanakuwa na maadili mazuri
  • Analea watoto kwa ukaribu, wakiumwa wakiwa shule mwalimu anawapeleka hospital

Yote haya hapati hata mia ya serikali, serikali inamkata mwalimu na kodi
"Tuwaze wote hapa" ni kitu gani mwalimu akifanye aonekane basi kuwa ni mtumishi muhimu wa hii nchi pengine kuliko wengi tu walioko huko kwenye "system" anazidiwa nini mwalimu huyu na wanao lala bungeni wakisubiri posho ya siku laki 3 ambayo ndo mshahara wa mwalimu kwa mwezi 'ikiwezekana tutenge siku ya kulia tu sisi walimu huenda serikali itatusikia"

Waalimu nasi ni watu tunaona, tunasikia!! "TUMEMSIKIA CAG" juzi juzi, katika hela zilizoibiwa kwenye miradi, achaneni na mradi mmoja tu hilo helo iloibiwa "muitenge kwa walimu" kama mlivyotenga kwenye madarasa

Mwalimu anajiuliza leo, jinsi wabunge, mawaziri na wanaojiita

"machawa wa mama" wanaona bora madarasa kuliko mwalimu!?

Mama kaupiga mwingi kwenye madarasa

Huu wimbo bila shaka mnausikia sana, sisi walimu tunaona wimbo gani huu wenye ubeti moja tu!!??

Wimbo ulipaswa useme Mama kaupiga mwingi kwenye maslahi ya waalimu, walimu wengi (ajira) madarasa na mabweni na kibwagizo kiwe "elimu bora" yaani mliosoma fasihi mnaelewa kuanza na mtu kisha vitu afu matokeo chanya yataonekana.

Ni nani boss wa mwalimu?

Pamoja na kilio cha walimu kuhusu maslahi yapo pia manung'uniko yao makubwa kuhusu utitiri wa boss wa mwalimu

Waalimu wanao watu wengi tu wanaowasimamia na kila anayemsimamia ana jambo lake dhidi ya mwalimu, matamko na maelekezo ya kila anayefika shule dhidi ya mwalimu yupo MKURUGENZI ambaye ndiyo mwajiri wa mwalimu, wapo kina mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, maafsa elimu wote kuanzia kata hadi mkoa hao ni baadhi tu!! Yapo matukio mwalimu anashikishwa adabu na mtendaji kata huku akinyoshewa vidole na wajumbe wa nyumba kumi!!

Kuna haja ya kuweka limitation ni nani hasa mwenye mamlaka zaidi kwa mwalimu!! Mwalimu aachwe atimize majukumu yake bila kuingiliwa na utitiri wa viongozi wakijiita ndo maboss wa mwalimu!!

*Mwalimu apunguziwe makablasha

Hapa nazungumzia makablasha kibao, mwalimu ana jaza
Lesson plan
Scheme of work
OPRAS
KPI
Class journal

Kazi kubwa ya mwalimu ni kufundisha, ili afundishe mwalimu anatakiwa ajiandae kwa kuandaa document kibao kama "SUBJECT NOTES"

Hii ni kazi kubwa, mwalimu anaandaa hizi notes kwa umakini huku akifuata nini syllabus imemuelekeza afanye kipengele kwa kipengele..

Anayo kazi ya kutafuta teaching aids ikiwemo kuchora, videos tofauti tofauti kutokana na hasa maendeleo ya teknolojia!

Kazi hii ni kubwa na inahitaji muda wa kutosha na utulivu mkubwa!
Pamoja na kazi hiyo kubwa bado miongozo inamuhitaji mwalimu ajaze lesson plan, scheme of work, na sasa kuna KPI (Key perfomance Indicator) nisikitike kusema hizi makablasha hazina maana yoyote ni kumchosha tu mwalimu ili mradi achanganyikiwe tu!!

Jamii imheshimu mwalimu
Leo nchi tunajadili mmomonyoko wa maadili na imekuwa shida na ni kilio cha jamii zetu
Chanzo kimeanzia kwenye jamii kutoheshimu walimu, jamii haioni kama walezi wakubwa wa watoto wao ni waalimu

Yapo matukio mengi tu mwalimu anajadiliwa na jamii kisa eti ni mkali kwa watoto wao

Waalimu wanafanya kazi kubwa mno kurekebisha tabia na mienendo ya watoto mashuleni, kazi kubwa inafanywa, waalimu wanalea maadili yaliyo bora lakin hawapati ushirikiano mzuri kutoka kwa walezi wao au wazazi wao, hakuna mwalimu kichaa anayeweza kuchapa watoto bila sababu ingawa mifano ipo ya waalimu kutoa adhabu kali zilizovuka mipaka lakini yote hii ni harakati za kuwafanya watoto wawe na tabia njema

Kipindi cha nyuma wazazi waliheshimu nafasi ya mwalimu katika kulea na kufanya watoto wawe wema katika jamii.

Jamii irudi nyuma ione haja ya kuwapa walimu nafasi kubwa ya kulea, mfano katika shule za bweni wanafunzi hawaruhusiwi kwenda kumbi za starehe, kutumia kilevi au kumiliki simu lakini wakati huo mtoto akirudi likizo mzazi anamnunulia simu na anatumia vyovyote atakavyo, mtoto anaenda club na anaweza kunywa vilevi na mzazi asimuonye!! Hii si sawa katika kushikiriana kimalezi!! Lazima jamii itimize wajibu hapa!!

Mwisho kabisa serikali iweke mazingira mazuri yahusuyo waalimu, waone nao ni watumishi wa serikali wanaopambana kwa maslahi mapana ya nchi hii hasa kuboresha maslahi ya waalimu,
 
Back
Top Bottom