Ukitumia ugonjwa kuombaomba fedha mtaani, adhabu ni jela miaka 3 au faini Milioni 5

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Machi 7, 2022 niliweka uzi hapa kuhusu watoto kuhusika katika biashara ya kuombaomba mitaani hasa kwenye miji mikubwa.

Justine Kaleb ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Mwandishi wa Vitabu vya Sheria, kutoka Kampuni ya Mawakili ya Moriah Law Chambers alifafanua kwa undani kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa watoto wanaofanya hizo shughuli.

Alifafanua kuhusu sheria zinazowabana watoto kufanya majukumu hayo ya kuombaomba na jinsi gani ambavyo mamlaka zinaweza kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria ndogondogo za Serikali za Mitaa ikiwemo Halmashari, Manispaa na Jiji.

Kwa ufafanuzi zaidi soma uzi huu hapa…
Watoto ombaomba ni halali kutolewa Mjini? Wakikamatwa Serikali inawapeleka wapi?

Wakili Justine Kaleb anasema kama ilivyo kwa watoto wanaofanya shughuli ya kuombaomba mitaani, sheria zinazozumika dhidi yao hazina tofauti sana, hata adhabu ni zinaendana.

Justine Kaleb anafafanua: “Kuna sheria tatu, ya kwanza ni ile ambao inamlenga mtoto zaidi japo mzazi na mlezi pia anahusika.

“Hapa mzazi au mlezi anatakiwa kuhakikisha mtoto anapata haki mbalimbali ikiwemo elimu, afya, matunzo, uangalizi, haki ya maoni…

“Ikitokea mzazi au mlezi ameshindwa kutimiza hayo kisha kumtumia mtoto katika shughuli za kuombaomba mitaani anaweza kukutana na mkono wa sheria.”

pic-wajanja-data.jpg


MZAZI/MLEZI ASIPOTIMIZA MAJUKUMU KWA MTOTO ANASHITAKIWA
“Mzazi anaweza kukumbana na adhabu ya faini au kifungo cha muda mfupi jela kama hatatimiza majukumu yake ya kumlea mtoto ambaye ni wajibu wake.

OMBAOMBA WAGONJWA MAKOSA YAO NI HAYA…
“Sheria ya pili ipo kwa ajili ya kila mtu, hii inahusu mamlaka za Serikali kuwa na mamlaka ya kuzuia na kuwaondoa wale wanaoenda kinyume na sheria zilizowekwa na Serikali za Mtaa.

“Unakuta kuna wale ombaomba ambao wana matatizo ya kiafya, wanatumia hali zao za kiafya kuombaomba mtaani hasa kwenye sehemu ambazo zina mpishano wa watu wengi kama vile kwenye mataa ya barabarani.

“Hao nao wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kwani suaa la afya zao wanatakiwa kufuata utaratibu maalum kama wanataka kuomba misaada barabarani.

“Mfano mtu ambaye ni mgonjwa na anataka kuomba msaada kutokana na afya yake kutokuwa sawa, anatakiwa kufuata taratibu za kuwa na nyaraka muhimu kutoka kwa wataalam wa afya kama vile hospitali ili kuonyesha anahitaji msaada wa kifedha.

“Japokuwa wamekuwa hawachukuliwi hatua na mamlaka lakini hiyo inamaanisha wapo sahihi kwa kuwa wanaumwa, wanafanya kinyume cha sheria wanaweza kukamatwa kwa mujibu wa sheria ndogondogo.

MZAZI/MLEZI AKIMTUMIA MTOTO NAYE KITANZINI
“Kuna wale wazazi au walezi ambao nao wanatumia watoto kuomba kwa kuwapeleka barabarani kisha wao wanajificha au wanakaa pembeni, wakibainika wanaweza kushtakiwa kwa sababu wanakiuka haki za mtoto kwa kuwatumikisha.

Sheria zilizopo hazirasimishi uwepo wa shughuli hiyo ya kuombaomba.
pic-wajanja-data (1).jpg

ADHABU NI KWENDA JELA
Adhabu mara nyingi inakuwa ni kifungo au faini au vyote viwili, bila kujali ni mgonjwa au la, lakini mara nyingi mamlaka huwa zinakuwa na kawaida ya kutumia busara katika kufanyamaamuzi, unakuta wale walemavu wanaondolewa na kupelekwa katika mikoa wanayotoka au kwenye taasisi walipokuwa awali.

“Kifungo chake kinaweza kuwa cha mwezi mmoja au wiki au siku kadhaa au faini ya fedha, huwa inategemea na mazIngiza na uhalisia wa tukio lilipofanyika na sheria ndogondogo zilizowekwa,” anasema Wakili Justine Kaleb.


Picha: Mtandaoni
 
Sasa hizo sheria zinafanya kazi muda gani, maana ombaomba wapo kila uchao na hatuoni wakipelekwa mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Mkubwa vipi kwa omba omba kama marais wa nchi za kiafrika wanaozungusha bakuli kule kwa mabeberu
 
Back
Top Bottom