Nyaraka za Nangwanda Lawi Sijaona Moja ya Vielelezo Muhimu Vya Historia ya TAA na TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
NYARAKA ZA NANGWANDA LAWI SIJAONA MOJA YA VIELELEZO MUHIMU VYA HISTORIA YA TAA NA TANU

Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea kutoka kwa mtoto wa Lawi Sijaona, Sijali Sijaona, nyaraka moja baada ya nyingine, picha na wakati mwingine akiniandikia maelezo kunieleza yale ambayo siyajui kuhusu baba yake, nyaraka hizo na maelezo ya picha.

Naelemewa hata sijua nianzie wapi au nataka kusema nini.
Labda nianze vipi nilijuana na Sijali.

Sijali nilijulishwa kwake katika miaka ya 1970 sote tukiwa vijana wadogo na Abubakar Kirundu mtoto wa Ramadhani Omari Kirundu aliyepata kuwa Meya wa Dar es Salaam mwaka wa 1966.

Nimepata kuandika siku za nyuma kuhusu Nyaraka za Nangwanda Lawi Sijaona nikiamini kuwa nyaraka hizi za uhuru wa Tanganyika si za kusubiri Serikali au CCM itengeneze kavazi.

Sisi wenyewe kwa uchache na udogo wetu tunawajibika kuziweka na kuzianika hadharani ili Watanzania waijue historia yao kwa ithibati ya nyaraka na picha kuepuka kuwekewa historia za kutunga.

Huko tushatoka na tumepita tusirudi tena nyuma.
Mtu haumwi kwenye shimo moja la nyoka mara mbili.

Nimepata kusema maneno haya siku za nyuma:

‘’Sijali amenionyesha baadhi ya nyarakaza na picha za baba yake zinazokwenda nyuma hadi miaka ya1950.

Nimesisimkwa, nimepatwa na majonzi na halikadhalika nimefurahi.

Nimesisimkwa kwani kwa kupitia nyaraka hizi nimerudishwa miaka mingi nyuma kuanza kujifunza upya historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kusoma nyaraka na kuangalia picha.

Nimepata majonzi kwa kule kutambua kuwa wazalendo waliojitolea kupigania uhuru wa Tanganyika wengi hawatambuliki na ni suala la muda tu hizi nyaraka na picha za marehemu Mzee Lawi Nangwanda Sijaona zitapotea na nchi itabaki masikini wa historia yake.

Nimefurahi kwa sababu angalau hizi kumbukumbu zimehifadhiwa mahali ingawa si pake khasa lakini tukizitaka zitapatikana na zikipatikana labda wahusika wa historia ya urithi wetu watachukua hatua ya kuzihifadhi kwa manufaa ya kizazi kijacho.’’

Sijali katika siku mbili hizi kaniletea nyaraka ambayo sikupata kuiona hata katika Nyaraka za Sykes – ‘’Kanuni na Sheria za Chama Cha Watu wa Afrika.’’

Kaniletea vilevile picha ambazo hakika ni hazina kubwa na kaniandikia maelezo ya picha hizo.

Picha hizi zimepigwa Lindi wakati wa Kura Tatu mwaka wa 1958:

''Kushoto kwenda kulia waliosimama ni Shyam Thanki ambae alikuwa na mchango wake katika harakati za mapambano ya Uhuru Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amenibeba, Mbutta Milando huyu alikuwa Katibu Mkuu wa TANU.

Waliokaa kutoka kushoto ni Mrs. Veronica Sijaona ambae ni Mama yangu Mzazi, Mzee Julias Kambarage Nyerere akiwa amempakata Evans Kulaga Sijaona ambae ni second born wa Lawi Nangwanda Sijaona na mwisho ni Mrs Ester Sijaona ambae ni Mke Mdogo wa Lawi Nangwanda Sijaona.

1696444608067.png

1696444748591.png

1696444805958.png




 
Nafikri sasa tuweke mkakati wa kuwa na Mohamed Said Digital Archive....
 
Nilisoma na jamaa anaitwa LAWI SIJAONA sijui ana uhusiano Gani na huyo MZEE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom