Unahitaji kuwa Afisa Usalama? Give it a try

Unahitaji kuwa Afisa Usalama? Give it a try

Incident kama zile huwa zinaharibu taswira ya Idara yetu hii adhimu...

Lakini naamini ni makosa kama yanavyotokea sehemu nyingine za kazi.

and you are not one of them!???hahaha mkuu ukiongea sana 'utateleza tu'...
kazi njema huko kwenye 'idara yenu'.
 
Angalizo: Hiki ninachokiandika hapa ni mawazo yangu binafsi. Kwa namna yoyote ile isichukuliwe kama ndio msimamo rasmi wa Idara husika.

--------------



Sikuwa na nia ya kuweka uzi mpya ndani ya wiki mbili hizi kwa kuwa niko kwenye maandalizi ya msimu wa pili wa simulizi ya Vipepeo Weusi.

Lakini kuna swali nimekuwa nalipata sana mara nyingi PM na wengine wakinitumia jumbe za simu. Sijajua ni kwanini huwa naulizwa hili swali, lakini imekuwa common sasa kupata jumbe za.. "Nina passion ya kuwa afisa usalama, nisaidie broh.!"
Mara nyingi huwa sijibu hizi jumbe. Don't know why napata jumbe za namna hii...

Leo nimeona "nijaribu" kuadress hili suala japo kiduchu tu kwa kadiri ninavyofahamu.


Kwa muda sasa nimekuwa natamani kuandika kuhusu masuala ya dara ya Usalama wa Taifa lakini nimekuwa nasita kwa kuwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu tunaishi kwa kuzingatia desturi ya kufanya ni mwiko kuongelea hayo masuala.


Kuna makala ndefu nimeandika kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa (masuala muhimu ambayo naamini hujawahi kuyasikia) lakini sitaiweka public kwa sasa, natamani ifanyiwe uhakiki kupunguza "makali" yake (kama yamo) ili nisiwakwaze mtu yoyote.



Nisisitize tena, mimi binafsi sio (na sijawahi) kuwa huko (kwenye Idara), haya ninayoaandika ni kutokana na uzoefu wa yale niliyotafiti na kuyasikia.
Kwahiyo unaposoma hili andiko fupi na siku utakaposoma makala kamili nitakapo iweka ni muhimu kuzingatia hilo, am not one of them!
Nina uzoefu tu wa kusikia kutoka kwa wahusika na walio karibu nao na pia natafiti sana.




Sasa basi,


Ziko makala nyingi zilizochambua ni namna gani mtu anafikia hatua ya kuwa afisa usalama.
Lakini kitu nilichokiona kwenye makala hizi karibia zote zinaonyesha 'traditional ways' zinazotumiwa na Idara kupata maafisa wake.

Mfano, njia hii inayoongelewa sana ni kutoka kwenye depo za jeshi, polisi, vyuo vikuu na kadhalika. Kwamba 'mawakala' wanakuwepo huko ili kuangalia vijana wenye 'potential' ambao wanaweza kuwa watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Sasa njia hizi ni za bahati nasibu sana, na ni ngumu mno kwa mtu mwenye kutamani kuwa Afisa usalama kuweza kubahatika kuwarecruited.


Hii ndio sababu iliyonifanya niandike andiko hili fupi kuongelea machache yanayoweza kusaidia kukufanya uweze labda kuwashawishi "mawakala" wa usalama wa Taifa hapo ulipo wapendekeze uwe recruited kwenye Idara.


Nimesema "hapo ulipo" kwa kuwa ndio, wako hapo ulipo… kila mahali ulipo! Kwenye sekta yako ya ajira, kanisani, misikitini, mitandaoni, vijiweni n.k. (sio kila kijiwe na kila kanisa au msikiti)


Ndio maana mwaka jana, Mheshimiwa Rais alipo mteua Askofu wa kanisa kuwa Mkurugenzi wa Idara hii nyeti, wengi wakalalama kuwa kwanini amemchagua mtu ambaye "hana uzoefu wa Idara", pasipo kujua kuwa Mkurugenzi huyu mpya amekuwa afisa wa Idara tangu miaka ya 1980s. Hata kabla hajawa Askofu, hata kabla hajaenda Uingereza kusoma, hata kabla hajaajiriwa BOT.


Ndio maana nasema, nitaeleza machache yanayoweza kusaidia labda watu wa Idara kuvutiwa nawe.


Kabla sijaongea vitu hivyo vichache unavyoweza kuvifanya kuwashawishi "Vipepeo Weusi" wakufanye kuwa mmoja wao, ni vyema kujifahamu japo kwa uchache nadharia ya recruitment ya Idara za Usalama duniani kote na hasa hapa kwetu Tanzania.

Yaani kwanini Idara inafanya recruitment? Ni swali jepesi, lakini naomba nilizungumze..



Nadharia ya kwanza; Idara ni lazima iendelee kuwepo.

Hii ndio nadharia ambayo imetumika kwa miaka mingi sana... Kwamba "tuna Taifa tunalohitaji kulilinda, tuna Taifa tunalotakiwa kuhakikisha liko Salama!", hivyo lazima Idara iendelee kuwepo muda wote.

Hii nadharia ndio inazaa ile "traditional procedure" ya recruitment… yaani kuchukua vijana kutoka vyuoni, jeshini, polisi n.k.

Yaani kwamba, kuna maafisa wanastaafu kila mwaka, kufariki, kuacha/kuachishwa na kadhalika. Hivyo wanahitajika kuwa replaced… lakini pia Idara inahitajika kukua kwa maana ya kuongeza idadi ya maafisa ili kuendana na ukuaji wa population ya nchi na kuongezeka kwa changamoto mpya… hivyo lazima kufanya recruitment ya maafisa wapya.…

Yaani lazima Idara iendelee kuwepo, haijalishi nchi iko kwenye tishio au iko tulivu.! Idara lazima iwepo na ifanye kazi muda wote.




Nadharia ya pili; Uhitaji Maalumu.

Nadharia ya pili inayotumika kuamua kufanya recruitment katika Idara ni pale panapoibuka hitaji maalumu la kiusalama.
Uzuri (au ubaya) ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kukua kwa teknolojia, kuongezeka kwa idadi ya watu, kuendelea kwa utandawazi, kukua kwa uchumi wa nchi, na mwenendo wa Dunia, masuala haya ya "uhitaji maalumu" yamekuwa ni endless. Yanaibuka kila leo.

Inafika kipindi kwamba watu/maafisa wanaokuwa recruited kwa kazi maalumu wanakuwa wengi kuzidi hata wale wanaokuwa recruited in a traditional procedures.



Mara nyingi watu wanaokuwa recruited kwa shughuli maalumu huwa wanatumika kwa sababu maalumu na kwa muda maalumu. Lakini wapo "assets" kadhaa ambao baadae wanabahatika kuwa "Vipepeo Weusi" kamili.



Kwa kuzingatia kwamba nchi yetu haina mfumo au desturi ya kuweka wazi ajira za Idara Ya Usalama wa Taifa Kuombwa hivyo basi katika andiko hili nitatumia sana nadharia hii ya pili kujaribu kuonyesha ni mambo gani muhimu yanayoweza kukusaidia kuwashawishi Idara Ya Usalama kukufanya kuwa afisa wao.


2b3eaf77729e843fa9b0b9498734c95e.jpg




Nitoe tena angalizo,


Nimeandika andiko hili kwa kuzingatia kanuni na desturi ya usiri unaopaswa kulindwa kuhusu Idara hii nyeti.
Hivyo basi si lengo la makala hii kuongelea siri au taarifa zilizo "classified"!

Makala hii inalenga kutia moyo, na labda kufumbua macho vijana wenye matamanio ya kuwa Maafisa wa Idara ya Usalama, namna wanavyoweza kujiunga na Idara kutimiza ndoto zao.
Pia nimeamua kuandika andiko hili ili kuwatia moyo vijana hawa wenye matamanio haya, kwa kuwa naamini kiwango cha juu kabisa cha uzalendo ni kufanya utumishi kwa nchi yako.



Pia nisisitize kwamba kabla ya kukuza mno matamanio yako ya kutaka kuwa Afisa Usalama ni vyema kujitathimini kama kweli unatosha? Na njia nzuri zaidi ya kujitathimini ni kujiuliza kwanini unataka kuwa Afisa usalama!
Je unapenda tu ile haiba yao, mavazi ya Kaunda suti na waya sikioni? Au ni kweli kwa dhati kabisa una nia ya kujitoa nafsi yako kutetea na kulinda nchi yako?

Ukishajijibu, unaweza kughairi au kukuza zaidi matamanio yako..


Pia niseme kuwa haya nitakayo yaeleza sio guarantee kwamba utaajiriwa na Idara ya Usalama… isipokuwa yanakuweka kwenye nafasi nzuri endapo kukiwa na uhitaji wa kufanya recruitment.


Nitaeleza machache hayo.





1. JIFUNZE LUGHA NGUMU NA MAHUSUSI

Kadiri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo umuhimu wa ujasusi wa kimataifa unavyoongezeka. Utandawazi, teknolojia na kukua kwa uchumi kunachochea muingiliano wa nchi yetu na mataifa mengine. Hii inaongeza ulazima wa Idara Ya Usalama wa Taifa kuwa makini zaidi ili kutambua maadui na kuwajua vyema hata wale ambao tunawahesabu kama nchi "marafiki".


Moja ya changamoto kubwa ninayoiona katika Idara yetu ya Usalama wa Taifa, ni kutokuwa na maafisa wa kutosha wenye ufasihi katika 'mission-critical languages'.

Mfano upande wa magharibi mwa nchi yetu na kaskazini magharibi, tunazungukwa na nchi zenye kutumia Kifaransa kama lugha kuu ya mawasiliano.

Ubaya ni kwamba Kifaransa si lugha ngumu kujifunza na kama ikitokea Idara wanataka kuweka 'spy ring' kwenye nchi hizo, maafisa wanaopelekwa huko wana uwezo wa kujifunza Kifaransa kwa muda mchache.

Lakini kama utakuwa na ujuzi wa Kifaransa inakupa points za ziada.

Kifaransa, Kiarabu na Kihispaniola nazichukulia kama lugha adhimu (zinakupa points), lakini sio muhimu zaidi ndani ya Idara.


Ukitaka kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi, jifunze lugha ngumu kama vile Kichina, Kikorea na Kihindi.

Nchi yetu imekuwa na muingiliano na mfungamono mkubwa na mataifa ya India, China na Korea.
Kuna umuhimu na uhitaji mkubwa kuwa na maafisa wenye ufasahi katika kuzungumza na kuzielewa lugha hizi (hasa Kichina na Kikorea).

Haina maana kuweka 'spy ring' nchini china au Korea wakati majasusi wenyewe hawana ufasihi katika lugha hizo. Hawawezi kufanya espionage kwa ufanisi.
Hivyo uhitaji wa maafisa wenye kuzielewa lugha hizi ni mkubwa mno.


Pia lugha nyingine ambayo iko juu kwenye orodha ya 'mission-critical languages' ndani ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa nchinu, ni Indonesian.
Japokuwaa umuhimu wake hauwezi kufikia ule wa Kichina na Kikorea, lakini Indonesian ipo kwenye ngazi ya juu pia ya umuhimu.

Pia uzuri ni kwamba Indonesian ni lugha rahisi sana kujifunza. Ni moja ya lugha chache duniani ambayo muundo wake wa sentesi ni rahisi kiasi kwamba mfano binafsi nilishangaa nilipojifunza kukuta hii ni moja ya lugha ambayo haina uwingi (plurals), au tenses.

Ukiwa na ufasaha kwenye lugha hizi (au hata mojawapo) inakuweka katika nafasi nzuri zaidi.







2. JIPE 'EXPOSURE'

Moja wapo ya sifa zinazochochea mtu kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa ni kiwango chake cha 'exposure' katika mataifa mengine.

Hii inasaidia mtu huyu pale anapotakiwa kupandikizwa nchi nyingine ili afanye shughuli za clandestine, inakuwa rahisi kwake kunyumbuka na jamii husika ya nchi hiyo.

Kama haujawahi kufika ulaya, basi jipe exposure hata katika nchi zinazotuzunguka.
Uelewa wako kuhusu jamii za nchi nyingine, lugha zao, na tamaduni zao zinakupa sifa za ziada ikitokea Idara inataka kufanya recruitment mahali ulipo kwa shughuli maalumu.


3.UONGEZA UELEWA WAKO KUHUSU TEHAMA


Moja kati ya vitu critical zaidi ambavyo kila afisa usalama anapaswa kuwa na utaalamu navyo katika zama hizi ni utaalamu wa tehama. Japokuwa bado wapo maafisa wachache wakongwe ambao hawako vizuri na mambo ya tehama, lakini maafisa wapya wote wanaoajiriwa na Idara ya Usalama wa Taifa sasa hivi, wakiwa kwenye mafunzo katika kituo cha tiss lazima wapite kwenye kozi ya Tehama.


Hii inatokana na mwenendo wa ulimwengu ulivyo sasa. Dunia nzima iko kidigitali na kitehama.


Pengine ndio sababu ya Rais Kumteua Mkurugenzi wa Usalama msomi nguli wa masuala haya ya Sayansi ya Kompyuta.


Kama wewe ni expert katika mifumo ya Kompyuta inakuweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Lakini kama hujafikia hatua ya kuwa expert basi walau jifunze hata a, be, che kuhusu 'hacking' na masuala yanayorandana na hayo.


Hii itakuweka kwenye nafasi nzuri pia.




4. HAKIKISHA UNA REKODI NZURI YA MASUALA YA KIFEDHA


Afisa yeyeto kabla ya kuajiriwa ni lazima ahakikiwe kuhusu masuala yake ya kifedha, kwa maana ya vyanzo vya mapato, matumizi na madeni.

Rekodi ya masuala ya kifedha inaeleza Mengi kuhusu haiba ya mtu.

Kumekuwa na visanga vingi vya maafisa usalama kuingia matatani kutoa siri baada ya kuhongwa fedha. Kwahiyo rekodi yako ya fedha inaeleza mengi kuhusu wewe.

Mfano mtuwenye mkopo Finca, hapo hapo analipa mkopo mwingine NMB, na hapo hapo ana mkopo kwenye vikundi… huyu hawezi kuwa afisa muadilifu. Ana kilala dalili kuwa ni mtu mwenye kupenda na wanaweza kutokea maadui waka-exploit desperation yake ya kutaka kuondokana na madeni na kumfanya kibaraka.


Kwa hiyo kama una fikiria siku moja kuwa afisa Usalama, hakikisha rekodi yako ya kifedha iko vyema.

(Pia na rekodi yako kuhusu uhalifu... Japo hii ina exception na complicated kidogo ndio maana sijaiweka kwenye orodha)





5. KUWA BORA ZAIDI YA WENGINE MAHALI ULIPO

Kufanya kazi katika Idara ya Usalama wa Taifa ni fursa adhimu kwa walio wengi na nadra kuipata.
Pia shughuli hii inahitaji umakini wa hali ya juu mno.

Hii ndio sababu ya Idara kurecruit watu ambao ni bora zaidi katika sekta zao husika.

Kwenye kazi yoyote ambayo unaifanya sasa hakikisha kuwa siku zote unakuwa bora kuliko wengine. Kama wewe ni banker, mwalimu, polisi, hotelia, mjasiriamali n.k. kuwa bora zaidi ya wenzako mlipo kwenye sekta hiyo. Jitahidi kujenga competence ya hali ya juu katika hilo unalolifanya.

Idara ya Usalama wa Taifa ni mahali kwa watu "elites" (au inapswa kuwa hivyo).


Hii ni moja ya njia bora zaidi inayoweza kukufanya kwa haraka sana kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa.
Kwenye Idara kuna saikolojia kwamba, mtu yeyote aliye bora kwenye sekta fulani, anapaswa kuwa "asset" (au afisa kabisa) wa usalama wa Taifa.





6. UZALENDO

Hii nimeiweka mwishoni kabisa lakini ilipaswa kuwa ya kwanza.


Unapokuwa afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, unaaminiwa na siri nzito zaidi kuhusu Taifa hili. Unaaminiwa kujua mambo ambayo mamilioni wengine hawayajui. Unaaminiwa kufahamu siri ambazo maadui zetu wa Taifa hawalali wakizisaka.

Hivyo basi afisa yeyote ni lazima awe na kiwango cha hali ya juu cha uzalendo kwa Tanzania.

Kwahiyo kama una ndoto ya siku moja kuja kuingia Idarani, hakikisha matendo yako, maneno yako, misimamo yako, na mawazo yako yana akisi na kuonyesha dalili ya uzalendo iliyo ndani mwako.


Hii ndio sifa kuu ya kuweza kupata fursa ya kujiunga kuwa afisa wa usalama wa Taifa. Uzalendo. Kuweka nchi yako kwanza kuliko kingine chochote kile.


Pia...

Najua kuna hoja huwa inaongelewa sana kwamba ili upate fursa kwenye Idara ni lazima uwe na msimamo wa kisiasa unaoendana na chama fulani... Hoja hii ina ukweli na uongo.
Ukweli ni kwamba, labda kuna watu waliwahi kupatiwa fursa hii kutokana na misimamo yao ya kisiasa. Labda kuna hayo makosa yalikuwa ynafanyika huko nyuma.
Uongo ni kwa sababu hii sio kanuni ya Idara kupata maafisa wake. Kanuni rasmi ya Idara ni uzalendo, na kwa mujibu wa maadili rasmi kabisa ya Idara, afisa ambaye amekula kiapo hapaswi kufungamana na mlengo wowote wa kisiasa.


So I know all this talk about chama fulani cha siasa... But its half truth!
Na nasikia kuna juhudi kubwa sana ndani ya idara kuhakikisha hiki kiapo kinazingatiwa ipasavyo (nchi kwanza). No petty politics.



Kwa leo niishie hapa na nimalizie kwa kurudia kusema kwamba, jitathimini kama kweli unatosha kuwa afisa wa Usalama wa Taifa.

Kazi ya Usalama wa Taifa si sawa na kazi nyingine za kuingia ofisini saa mbili asubuhi na kutoka saa nane au kumi jioni.
Ni kazi ya long hours… kuna siku ambazo hautalala hata siku mbili nzima uko macho na unatakiwa kuwa active na makini kwa muda wote huo na utimize majukumu yako kwa ukamilifu na ufanisi wa hali ya juu bila chembe ya errors.


Ni kazi yenye mengi nyuma ya pazia kuzidi suti za kaunda na nyaya masikioni unazoziona na kuvutiwa nazo kwa maafisa walio kwenye Protection Unit.
Ni kazi ambayo shughuli zake zinatekelezwa kila siku kwa kiwango kikubwa cha 'urgency'!
Ni kazi ambayo maisha yako yanakuwa hatarini kila siku unayoishi.


Ni kazi ambayo ukitaka kuimudu kwa usahihi unapaswa kuwa na uzalendo haswa moyoni.




Ukijitathimini na kujiona unatosha… basi muombe Mungu, siku moja labda itakuwa!



"Kiwango cha juu zaidi cha uzalendo, ni kutoa utumishi kwa nchi yako"



THE BOLD
Sidhani kama sija kuelewa manaake na mimi ni kilaza sana.....
 
and you are not one of them!???hahaha mkuu ukiongea sana 'utateleza tu'...
kazi njema huko kwenye 'idara yenu'.
Hapo kavaa uhusika kama Mtanzania Mzalendo, ndio maana akatumia nafsi ya tatu wingi. Ila haikumaainisha kuwa ni mmoja wao.
 
Mkuu umeelezea vizuri,kwa utafiti wangu pia wa muda mrefu kuna kitu nataka kuongezea hapo ambacho labda hujakibaini na cha msingi zaidi nacho ni dhehebu la dini. Kwa huo utafiti wangu nimegundua kwamba wanapenda sana madhehebu ambayo ni asilia yaani kwa wakristo ni RC na waislamu ni hawa walio chini ya BAKWATA. Maana yake nini, hii kazi inahitaji watu loyal na sio wakaidi kama ilivyo madhehebu mengine(Protestants).Hilo kwa maoni yangu jaribu kufanyia kazi uone ukweli wake.
 
Kuna mwanajeshi mmoja aliwahi kuniambia"dogo usipende usichokijua".....sijui alikua na maana gani..mpaka Leo huwa natafakari sana!
 
The.bold hajawah kuniangusha hata siku 1 always anatoa vyuma vya reli zaidi anafata sheria tafaut ja wengne nmefurah kuona hata kabla ya makala kamil umeamua wahakiki wakemia wakuu isije kuwa shida ahsante sana upend maneno na kukwaza viongoz wa nchi.....

Ila ndugu mm makala yako ya vipepeo weusi nlishia episode ya 5 nkaktumia sms nitapaje muendelezo ukunijibu mpaka leo......

Nashukuru sana ndugu kwa matory yalokwenda Kwa mkemia vitu adimu sana hongera kwa kipaji chako ndugu tupo pamoja.....m

Vijana wengi wanataman kuwa usalama ila ukwel husiopingika hawajui ile kazi ni ya kujtoa sadaka roho yako sababu ya nchi yako.......

Utajsikiaje unaitumikia nchi yako kisha unadakwa nchi yako wanakukana we uko wala kichapo cha maana??? au kuuwawa je utakuwa tayari usitoe siri?????

ni uzalendo na heshma ya hali ya juu

Tujiangalie matendo yetu tu tunayoyafanya kabla ya kuifikiria Idara.........

Tujipime tu....

Wengi hawaipend Tz kila baya unakuta mtu anaipondea nchi yake hana mapenz kabsa yupo tyr asifie nchi nyingne na kuiponda yake had viongoz wake.....

Hufaiiii tafuta nyanya uuuze
 
Ila suala la kuwa mwanachama wa chama kile ndiyo namba moja japo ni hidden issue maana rafiki yangu hakufanikiwa kwa kuwa aliyekuwa anamwandaa alikufa ghafla.
Ila alimwambia awe na kadi ya chama chetu kile. Labda nikuulize inawezekana wakakutaka pasipo kujua wala kuomba?.
 
Ila suala la kuwa mwanachama wa chama kile ndiyo namba moja japo ni hidden issue maana rafiki yangu hakufanikiwa kwa kuwa aliyekuwa anamwandaa alikufa ghafla.
Ila alimwambia awe na kadi ya chama chetu kile. Labda nikuulize inawezekana wakakutaka pasipo kujua wala kuomba?.


Aiseeeeeh,
Pole Sana mkuu.

The bold ameandika wazi kuwa, kama wewe ni asset watakuchukua tu siku ikifika.
 
Hahahah!! Ok, here we go...



Unauliza nimeandika kwa maslahi ya nani??
Jibu: kwa maslahi ya vijana wote wenye matamanio ya kuingia katika huu utumishi... Matamanio yao ya kuitumikia nchi yao ni matamanio memo na yanapaswa kuchochewa...


Umeuliza kwa nini nimeandika hisia zangu??

Jibu: Nafahamu kuhusu nilichokiandika hapa zaidi ya maneno haya unayoyaona nimeandika hapa... Ila kwa kuzingatia sheria za nchi na tamaduni za usiri wa idara hiyo siwezi kuandika kila kitu...

Hakuna ubaya wa kuandika utashi wako (unaweza kuita hisia ukipenda)


Unasema ni kosa hiki nilichoandika??

Jibu: sidhani kama unaijua hata sheria ya kuanzishwa kwa idara ya usalama wa Taifa... Nenda kaisoma ndipi utajua nini ni siri na nini si siri... Kipi kinapswa kuzungumzwa na kipi hakipaswi kuzungumzwa...


Unasema nina lengo gani??

Jibu: unarudia swali lile lile kila baada ya aya moja. Nimekujibu hapo juu...


Unauliza wapi nimeambiwa kuna haja ya kuwapa watu somo.

Jibu: sidhani kama unatambua haki na wajibu wa mwananchi wa Tanzania kwa mujibu wa katiba. Nenda kasome.



Niko tayari kuwajibika kama itajenga "myth" kwenye jamii?

Jibu: mimi ni muwajibikaji tangu siku ya kwanza natoka kwenye tumbo la mama yangu.

Na kama andiko hili lingekuwa na shida yeyote... Wahusika wenyewe wangenitaarifu mpaka muda huu... They know me... Na si Mara moja au mbili wameniambia nisiandike kuhusu kitu Fulani... So tutayamaliza wenyewe...


Mwisho..

Najua watu wa dizaini yako, najua unachojaribu ku-insinuate... Najua unataka watu wakuoneje, najua unataka watu wakuhisi wewe ni nani...

You are not.. Stop pretending.... Its pathetic!!

If TISS has a problem with me they have my number... Tutamaliza kiutu uzima... Wataniambia niondoe Uzi na nitaondoa... sio hizi ngonjera unazoleta hapa...


Siku njema..
Jibu mubashara The bold
 
Kazi ya kindezi iyo .....zile movie za Hollywood za ki~espionage zinatudanganga aisseh ....bata huli khaaa
 
The Bold una kitu ndani yako ambacho ni muhimu sana kwa idara hii nyeti!
 
Mkuu nielekeze hiyo bar nami nikawasikie wakijitambulisha....toka nizaliwe sijawahi kumuona hata mmoja
Haaahaaa! Nimeandika 'nasikia' .... nikimaanisha kwenye vijiwe vyetu kuwa wakilewa wanajitambulisha... mwenyewe natamani kumwona hata mmoja, huko bar uwezo wa kufika. Sina mie yangu mataputapu pale kwa Mama Dan , Kolomije mjini
 
lazima ujue huo uhuru "uliozaliwa" nao haukuibuka tuu from thin air na usiuchukue tuu for granted. labda huyo uliemjibu alifanya uchaguzi mbaya wa maneno ila point ni kua kuna watu ambao hutokuja kuwajua kamwe ambao wanahakikisha "unazaliwa" na uhuru na wanaparangana kila siku usiishi kwenye failed state
Wapo wapumbavu flan ambao wanafanya kila kitu Tanzania ibaki hapa ilipo leo
 
Upande wa pili wa shilingi ya asset ni liability ni lini afisa anakuwa liability? Si alichukuliwa kuruta kama asset.

Je mtu au kitu gani kinakuwa asset ya kufuatiliwa nyendo zake?

Pale kitu au mtu anapotumiwa bila kujijua si inakuwa dhuluma maana kwa mfano mnatumia akili ya mtu kutimiza malengo yenu bila kumpa ujira hata bila kumjulisha. Ukiangalia kama huyu marehemu Ngosha (rip) akili na ubunifu wake katika uchoraji umetumiwa, nembo inaendelea kutumika yeye kafa maaskini kaambulia jeneza tu la maana na mazishi ya heshima.

Na washawasha!
Hili liko obviously sana kwa sababu haawa watu waanataka kila taaarifa
Hata tunavyosema hapa tayar tumetumika kutoa taarifa kwaa mahasimu wetu bila kujijua au tunajua lkn hamna namna lazima useme kama namna ya maisha
Huko mtaan tunasema tu kwa kila mtu mtaan juu ya jambo flan au rafiki ktk maisha kumbe anakutumia indirectly bila kujua
Hivyo tusiwe wepes kusema kila jambo pia kulalamika kutoka na eneo lako la kazi au shule or chuo kwa mtu yeyote bila kuzingatia ethically
 
Kitu chochote chenye usiri huongeza hamasa ya watu kukijua ama hata kuwa aehemu ya hiyo jamii.Lakini kiukweli hakuna lolote la maana..watu wanatamani kuwa miongoni mwa jamii ya freemason,usalama nk.Lakini hamna kitu.Kuna jamaa yangu alikuwa usalama na ameacha.Hakuna la maana,tafuteni pesa,acheni illusion..
Ni maisha mazuri ukiamua kuishi kama kasisi wa kikatoliki ktk idara hiyo lkn sio mazuri maisha hayo ukitaka kuishi kama mm au wewe
Kwa nn
Kasisi huiacha. Familia yake na huishi kama mtoto wa kanisa daima maisha yake yatategemea sadaka ili aishi na kusali na kutumwa kazi ya kanisa na jamii kichwan kwake haijui familia yake wala maisha yake yeye macho yake ni waamin na kanisa

Kama unaweza kuwa kasisi wa taifa karibu
Kama unataka kuwa superstarwa taifa kwa heri
 
Dah! Hii nimwandae mwanangu aje atumikie taifa lake
Was my only advice to all

It is mythical now to think about you in this

Panga upya juu ya kuwekeza
Kwa wanao au watoto
Ingekuwa vema ikawa hoja hapa ya kujifunZa mbinu za kuwekeza kwa watoto ktk jukwaa hili
The bold ni kuwafariji tu hapa kuwapa yote haya tutake another option
 
Back
Top Bottom