Unahitaji kuwa Afisa Usalama? Give it a try

Unahitaji kuwa Afisa Usalama? Give it a try

Nahitaji kuwa kwani nafikiri naweza tena napenda sana kushiiriki katika ujenzi wa taifa letu nikiwa na nafasi yangu kama msomi wa ngazi wa uzamivu na ninayetembelea mataifa mbalimbali. Najihusisha na sayansi ya asili na huku kwa kweli kunahitaji usalama na uzalendo sana kwani watanzania wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa taifa hudanganywa na watu wasio wazalendo kuhusu mambo ya maslahi ya taifa. Tafadhali nijulishe nifanye nini niweze kutoa mchango wangu kupitia usalama wa taifa. 0686997270

Kosa la kwanza ni kuweka namba yako hadharani.
 
Maofisa usalama huwa wanatafutwa bila wao kujitambua ni ngumu sana ukataka kuwa afisa usalama na ukaupata,hapa kwetu wengi waliajiriwa huko walienda sababu ndugu zao walikuwa wafanyakazi wa hiyo idara tofauti na wenzetu ambao huwa wanatangaza hizo kazi waziwazi kila mtu kama atakuwa na vigezo anaajiriwa.Baadhi ya watumishi kwenye idara za serikali ni maafisa usalama

1.Human Resources
Idara nyingi hawa ndio wanakuwa na taarifa zote za wafanyakazi kwenye ofisi,ukiomba kazi CV yako huwa inafika kwa HR na pia anakuwa na report ya mwenendo wako wote kipindi chote ulichofanya kazi kwenye hiyo ofisi pia ni rahisi yeye kuwasiliana na HR wa ofisi ulizofanya kazi zamani kabla ofisi yako ya sasa.Waajiri wengi kabla hawajaajiri mfanyakazi huuliza ofisa HR wa sehemu ambazo ulifanya kazi huko nyuma kama ulivyoandika kwenye CV yako


2.Dean of Students /Registration Officer
Hawa wanatumika vyuoni huwa wana taarifa nyingi za wanafunzi wote ikitokea mtu anahitajika wao ndio huandaa ripoti ya mhusika katika kipindi chote akiwa chuoni.Hutumiwa sana kupeleleza kama wanafunzi wanataka kugoma au kuangalia reaction ya wanafunzi kuhusu jambo fulani.Pia wanahusika kuandaa viongozi wa vyama vya wanafunzi


3.Registry Officers (Ofisa Masjala)
Idara ya masjala ni nyeti sana kwenye ofisi nyingi sana kwani wao ndio wanapokea na kutoa taarifa nyingi za kampuni kabla hazijafika kwa walengwa,wengi wao ni wasiri sana na hawapaswi kuwa waropokaji.Mfanyakazi anaweza akawa tayari ameandikiwa barua ya kufukuzwa kazi wiki moja kabla kukabidhiwa rasmi Registry Officer anafahamu lakini hawezi kuropoka


4.Viongozi wa Dini
Viongozi wa dini hutumiwa sana na idara ya usalama kazi yao inaweka karibu sana na wananchi na uadilifu na usiri walio nao,kuwatumia viongozi wa dini ni rahisi kupata taarifa za mtu yeyote au jambo lolote kiurahisi.

Wapo wengine kama madereva na ma-secretary ambao hutumiwa na idara ya usalama wa taifa kwenye mission mbalimbali
 
Back
Top Bottom