Unahitaji kuwa Afisa Usalama? Give it a try

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457

Au bofya link hapa chini kunitumia ujumbe moja kwa moja whatsApp




Angalizo: Hiki ninachokiandika hapa ni mawazo yangu binafsi. Kwa namna yoyote ile isichukuliwe kama ndio msimamo rasmi wa Idara husika.
--------------
Sikuwa na nia ya kuweka uzi mpya ndani ya wiki mbili hizi kwa kuwa niko kwenye maandalizi ya msimu wa pili wa simulizi ya Vipepeo Weusi.

Lakini kuna swali nimekuwa nalipata sana mara nyingi PM na wengine wakinitumia jumbe za simu. Sijajua ni kwanini huwa naulizwa hili swali, lakini imekuwa common sasa kupata jumbe za.. "Nina passion ya kuwa afisa usalama, nisaidie broh.!"
Mara nyingi huwa sijibu hizi jumbe. Don't know why napata jumbe za namna hii.

Leo nimeona "nijaribu" kuadress hili suala japo kiduchu tu kwa kadiri ninavyofahamu.

Kwa muda sasa nimekuwa natamani kuandika kuhusu masuala ya dara ya Usalama wa Taifa lakini nimekuwa nasita kwa kuwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu tunaishi kwa kuzingatia desturi ya kufanya ni mwiko kuongelea hayo masuala.

Kuna makala ndefu nimeandika kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa (masuala muhimu ambayo naamini hujawahi kuyasikia) lakini sitaiweka public kwa sasa, natamani ifanyiwe uhakiki kupunguza "makali" yake (kama yamo) ili nisiwakwaze mtu yoyote.

Nisisitize tena, mimi binafsi sio (na sijawahi) kuwa huko (kwenye Idara), haya ninayoaandika ni kutokana na uzoefu wa yale niliyotafiti na kuyasikia.

Kwahiyo unaposoma hili andiko fupi na siku utakaposoma makala kamili nitakapo iweka ni muhimu kuzingatia hilo, I am not one of them! Nina uzoefu tu wa kusikia kutoka kwa wahusika na walio karibu nao na pia natafiti sana.

Sasa basi,,Ziko makala nyingi zilizochambua ni namna gani mtu anafikia hatua ya kuwa afisa usalama. Lakini kitu nilichokiona kwenye makala hizi karibia zote zinaonyesha 'traditional ways' zinazotumiwa na Idara kupata maafisa wake.

Mfano, njia hii inayoongelewa sana ni kutoka kwenye depo za jeshi, polisi, vyuo vikuu na kadhalika. Kwamba 'mawakala' wanakuwepo huko ili kuangalia vijana wenye 'potential' ambao wanaweza kuwa watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Sasa njia hizi ni za bahati nasibu sana, na ni ngumu mno kwa mtu mwenye kutamani kuwa Afisa usalama kuweza kubahatika kuwarecruited.

Hii ndio sababu iliyonifanya niandike andiko hili fupi kuongelea machache yanayoweza kusaidia kukufanya uweze labda kuwashawishi "mawakala" wa usalama wa Taifa hapo ulipo wapendekeze uwe recruited kwenye Idara.

Nimesema "hapo ulipo" kwa kuwa ndio, wako hapo ulipo… kila mahali ulipo! Kwenye sekta yako ya ajira, kanisani, misikitini, mitandaoni, vijiweni n.k. (sio kila kijiwe na kila kanisa au msikiti).

Ndio maana mwaka jana, Mheshimiwa Rais alipo mteua Askofu wa kanisa kuwa Mkurugenzi wa Idara hii nyeti, wengi wakalalama kuwa kwanini amemchagua mtu ambaye "hana uzoefu wa Idara", pasipo kujua kuwa Mkurugenzi huyu mpya amekuwa afisa wa Idara tangu miaka ya 1980s. Hata kabla hajawa Askofu, hata kabla hajaenda Uingereza kusoma, hata kabla hajaajiriwa BOT.

Ndio maana nasema, nitaeleza machache yanayoweza kusaidia labda watu wa Idara kuvutiwa nawe.

Kabla sijaongea vitu hivyo vichache unavyoweza kuvifanya kuwashawishi "Vipepeo Weusi" wakufanye kuwa mmoja wao, ni vyema kujifahamu japo kwa uchache nadharia ya recruitment ya Idara za Usalama duniani kote na hasa hapa kwetu Tanzania.

Yaani kwanini Idara inafanya recruitment? Ni swali jepesi, lakini naomba nilizungumze.

Nadharia ya kwanza; Idara ni lazima iendelee kuwepo.

Hii ndio nadharia ambayo imetumika kwa miaka mingi sana... Kwamba "tuna Taifa tunalohitaji kulilinda, tuna Taifa tunalotakiwa kuhakikisha liko Salama!", hivyo lazima Idara iendelee kuwepo muda wote.

Hii nadharia ndio inazaa ile "traditional procedure" ya recruitment… yaani kuchukua vijana kutoka vyuoni, jeshini, polisi n.k.

Yaani kwamba, kuna maafisa wanastaafu kila mwaka, kufariki, kuacha/kuachishwa na kadhalika. Hivyo wanahitajika kuwa replaced… lakini pia Idara inahitajika kukua kwa maana ya kuongeza idadi ya maafisa ili kuendana na ukuaji wa population ya nchi na kuongezeka kwa changamoto mpya… hivyo lazima kufanya recruitment ya maafisa wapya.…

Yaani lazima Idara iendelee kuwepo, haijalishi nchi iko kwenye tishio au iko tulivu.! Idara lazima iwepo na ifanye kazi muda wote.

Nadharia ya pili; Uhitaji Maalumu.

Nadharia ya pili inayotumika kuamua kufanya recruitment katika Idara ni pale panapoibuka hitaji maalumu la kiusalama. Uzuri (au ubaya) ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kukua kwa teknolojia, kuongezeka kwa idadi ya watu, kuendelea kwa utandawazi, kukua kwa uchumi wa nchi, na mwenendo wa Dunia, masuala haya ya "uhitaji maalumu" yamekuwa ni endless. Yanaibuka kila leo.

Inafika kipindi kwamba watu/maafisa wanaokuwa recruited kwa kazi maalumu wanakuwa wengi kuzidi hata wale wanaokuwa recruited in a traditional procedures.

Mara nyingi watu wanaokuwa recruited kwa shughuli maalumu huwa wanatumika kwa sababu maalumu na kwa muda maalumu. Lakini wapo "assets" kadhaa ambao baadae wanabahatika kuwa "Vipepeo Weusi" kamili.

Kwa kuzingatia kwamba nchi yetu haina mfumo au desturi ya kuweka wazi ajira za Idara Ya Usalama wa Taifa Kuombwa hivyo basi katika andiko hili nitatumia sana nadharia hii ya pili kujaribu kuonyesha ni mambo gani muhimu yanayoweza kukusaidia kuwashawishi Idara Ya Usalama kukufanya kuwa afisa wao.


2b3eaf77729e843fa9b0b9498734c95e.jpg


Nitoe tena angalizo,

Nimeandika andiko hili kwa kuzingatia kanuni na desturi ya usiri unaopaswa kulindwa kuhusu Idara hii nyeti.
Hivyo basi si lengo la makala hii kuongelea siri au taarifa zilizo "classified"!

Makala hii inalenga kutia moyo, na labda kufumbua macho vijana wenye matamanio ya kuwa Maafisa wa Idara ya Usalama, namna wanavyoweza kujiunga na Idara kutimiza ndoto zao.

Pia nimeamua kuandika andiko hili ili kuwatia moyo vijana hawa wenye matamanio haya, kwa kuwa naamini kiwango cha juu kabisa cha uzalendo ni kufanya utumishi kwa nchi yako.

Pia nisisitize kwamba kabla ya kukuza mno matamanio yako ya kutaka kuwa Afisa Usalama ni vyema kujitathimini kama kweli unatosha? Na njia nzuri zaidi ya kujitathimini ni kujiuliza kwanini unataka kuwa Afisa usalama!

Je unapenda tu ile haiba yao, mavazi ya Kaunda suti na waya sikioni? Au ni kweli kwa dhati kabisa una nia ya kujitoa nafsi yako kutetea na kulinda nchi yako?

Ukishajijibu, unaweza kughairi au kukuza zaidi matamanio yako.

Pia niseme kuwa haya nitakayo yaeleza sio guarantee kwamba utaajiriwa na Idara ya Usalama… isipokuwa yanakuweka kwenye nafasi nzuri endapo kukiwa na uhitaji wa kufanya recruitment.

Nitaeleza machache hayo.

1. JIFUNZE LUGHA NGUMU NA MAHUSUSI
Kadiri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo umuhimu wa ujasusi wa kimataifa unavyoongezeka. Utandawazi, teknolojia na kukua kwa uchumi kunachochea muingiliano wa nchi yetu na mataifa mengine. Hii inaongeza ulazima wa Idara Ya Usalama wa Taifa kuwa makini zaidi ili kutambua maadui na kuwajua vyema hata wale ambao tunawahesabu kama nchi "marafiki".

Moja ya changamoto kubwa ninayoiona katika Idara yetu ya Usalama wa Taifa, ni kutokuwa na maafisa wa kutosha wenye ufasihi katika 'mission-critical languages'.

Mfano upande wa magharibi mwa nchi yetu na kaskazini magharibi, tunazungukwa na nchi zenye kutumia Kifaransa kama lugha kuu ya mawasiliano.

Ubaya ni kwamba Kifaransa si lugha ngumu kujifunza na kama ikitokea Idara wanataka kuweka 'spy ring' kwenye nchi hizo, maafisa wanaopelekwa huko wana uwezo wa kujifunza Kifaransa kwa muda mchache.

Lakini kama utakuwa na ujuzi wa Kifaransa inakupa points za ziada.

Kifaransa, Kiarabu na Kihispaniola nazichukulia kama lugha adhimu (zinakupa points), lakini sio muhimu zaidi ndani ya Idara.

Ukitaka kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi, jifunze lugha ngumu kama vile Kichina, Kikorea na Kihindi.

Nchi yetu imekuwa na muingiliano na mfungamono mkubwa na mataifa ya India, China na Korea. Kuna umuhimu na uhitaji mkubwa kuwa na maafisa wenye ufasahi katika kuzungumza na kuzielewa lugha hizi (hasa Kichina na Kikorea).

Haina maana kuweka 'spy ring' nchini china au Korea wakati majasusi wenyewe hawana ufasihi katika lugha hizo. Hawawezi kufanya espionage kwa ufanisi. Hivyo uhitaji wa maafisa wenye kuzielewa lugha hizi ni mkubwa mno.

Pia lugha nyingine ambayo iko juu kwenye orodha ya 'mission-critical languages' ndani ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa nchinu, ni Indonesian. Japokuwaa umuhimu wake hauwezi kufikia ule wa Kichina na Kikorea, lakini Indonesian ipo kwenye ngazi ya juu pia ya umuhimu.

Pia uzuri ni kwamba Indonesian ni lugha rahisi sana kujifunza. Ni moja ya lugha chache duniani ambayo muundo wake wa sentesi ni rahisi kiasi kwamba mfano binafsi nilishangaa nilipojifunza kukuta hii ni moja ya lugha ambayo haina uwingi (plurals), au tenses.

Ukiwa na ufasaha kwenye lugha hizi (au hata mojawapo) inakuweka katika nafasi nzuri zaidi.

2. JIPE 'EXPOSURE
Moja wapo ya sifa zinazochochea mtu kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa ni kiwango chake cha 'exposure' katika mataifa mengine.

Hii inasaidia mtu huyu pale anapotakiwa kupandikizwa nchi nyingine ili afanye shughuli za clandestine, inakuwa rahisi kwake kunyumbuka na jamii husika ya nchi hiyo.

Kama haujawahi kufika ulaya, basi jipe exposure hata katika nchi zinazotuzunguka.
Uelewa wako kuhusu jamii za nchi nyingine, lugha zao, na tamaduni zao zinakupa sifa za ziada ikitokea Idara inataka kufanya recruitment mahali ulipo kwa shughuli maalumu.

3.UONGEZA UELEWA WAKO KUHUSU TEHAMA
Moja kati ya vitu critical zaidi ambavyo kila afisa usalama anapaswa kuwa na utaalamu navyo katika zama hizi ni utaalamu wa tehama. Japokuwa bado wapo maafisa wachache wakongwe ambao hawako vizuri na mambo ya tehama, lakini maafisa wapya wote wanaoajiriwa na Idara ya Usalama wa Taifa sasa hivi, wakiwa kwenye mafunzo katika kituo cha tiss lazima wapite kwenye kozi ya Tehama.

Hii inatokana na mwenendo wa ulimwengu ulivyo sasa. Dunia nzima iko kidigitali na kitehama.

Pengine ndio sababu ya Rais Kumteua Mkurugenzi wa Usalama msomi nguli wa masuala haya ya Sayansi ya Kompyuta.

Kama wewe ni expert katika mifumo ya Kompyuta inakuweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Lakini kama hujafikia hatua ya kuwa expert basi walau jifunze hata a, be, che kuhusu 'hacking' na masuala yanayorandana na hayo.

Hii itakuweka kwenye nafasi nzuri pia.

4. HAKIKISHA UNA REKODI NZURI YA MASUALA YA KIFEDHA
Afisa yeyeto kabla ya kuajiriwa ni lazima ahakikiwe kuhusu masuala yake ya kifedha, kwa maana ya vyanzo vya mapato, matumizi na madeni.

Rekodi ya masuala ya kifedha inaeleza Mengi kuhusu haiba ya mtu.

Kumekuwa na visanga vingi vya maafisa usalama kuingia matatani kutoa siri baada ya kuhongwa fedha. Kwahiyo rekodi yako ya fedha inaeleza mengi kuhusu wewe.

Mfano mtuwenye mkopo Finca, hapo hapo analipa mkopo mwingine NMB, na hapo hapo ana mkopo kwenye vikundi… huyu hawezi kuwa afisa muadilifu. Ana kilala dalili kuwa ni mtu mwenye kupenda na wanaweza kutokea maadui waka-exploit desperation yake ya kutaka kuondokana na madeni na kumfanya kibaraka.

Kwa hiyo kama una fikiria siku moja kuwa afisa Usalama, hakikisha rekodi yako ya kifedha iko vyema.

(Pia na rekodi yako kuhusu uhalifu... Japo hii ina exception na complicated kidogo ndio maana sijaiweka kwenye orodha)

5. KUWA BORA ZAIDI YA WENGINE MAHALI ULIPO

Kufanya kazi katika Idara ya Usalama wa Taifa ni fursa adhimu kwa walio wengi na nadra kuipata.
Pia shughuli hii inahitaji umakini wa hali ya juu mno.

Hii ndio sababu ya Idara kurecruit watu ambao ni bora zaidi katika sekta zao husika.

Kwenye kazi yoyote ambayo unaifanya sasa hakikisha kuwa siku zote unakuwa bora kuliko wengine. Kama wewe ni banker, mwalimu, polisi, hotelia, mjasiriamali n.k. kuwa bora zaidi ya wenzako mlipo kwenye sekta hiyo. Jitahidi kujenga competence ya hali ya juu katika hilo unalolifanya.

Idara ya Usalama wa Taifa ni mahali kwa watu "elites" (au inapswa kuwa hivyo).

Hii ni moja ya njia bora zaidi inayoweza kukufanya kwa haraka sana kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa.
Kwenye Idara kuna saikolojia kwamba, mtu yeyote aliye bora kwenye sekta fulani, anapaswa kuwa "asset" (au afisa kabisa) wa usalama wa Taifa.

6. UZALENDO

Hii nimeiweka mwishoni kabisa lakini ilipaswa kuwa ya kwanza.

Unapokuwa afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, unaaminiwa na siri nzito zaidi kuhusu Taifa hili. Unaaminiwa kujua mambo ambayo mamilioni wengine hawayajui. Unaaminiwa kufahamu siri ambazo maadui zetu wa Taifa hawalali wakizisaka.

Hivyo basi afisa yeyote ni lazima awe na kiwango cha hali ya juu cha uzalendo kwa Tanzania.

Kwahiyo kama una ndoto ya siku moja kuja kuingia Idarani, hakikisha matendo yako, maneno yako, misimamo yako, na mawazo yako yana akisi na kuonyesha dalili ya uzalendo iliyo ndani mwako.

Hii ndio sifa kuu ya kuweza kupata fursa ya kujiunga kuwa afisa wa usalama wa Taifa. Uzalendo. Kuweka nchi yako kwanza kuliko kingine chochote kile.

Pia...

Najua kuna hoja huwa inaongelewa sana kwamba ili upate fursa kwenye Idara ni lazima uwe na msimamo wa kisiasa unaoendana na chama fulani... Hoja hii ina ukweli na uongo.

Ukweli ni kwamba, labda kuna watu waliwahi kupatiwa fursa hii kutokana na misimamo yao ya kisiasa. Labda kuna hayo makosa yalikuwa ynafanyika huko nyuma.

Uongo ni kwa sababu hii sio kanuni ya Idara kupata maafisa wake. Kanuni rasmi ya Idara ni uzalendo, na kwa mujibu wa maadili rasmi kabisa ya Idara, afisa ambaye amekula kiapo hapaswi kufungamana na mlengo wowote wa kisiasa.

So I know all this talk about chama fulani cha siasa... But its half truth!
Na nasikia kuna juhudi kubwa sana ndani ya idara kuhakikisha hiki kiapo kinazingatiwa ipasavyo (nchi kwanza). No petty politics.

Kwa leo niishie hapa na nimalizie kwa kurudia kusema kwamba, jitathimini kama kweli unatosha kuwa afisa wa Usalama wa Taifa.

Kazi ya Usalama wa Taifa si sawa na kazi nyingine za kuingia ofisini saa mbili asubuhi na kutoka saa nane au kumi jioni.

Ni kazi ya long hours… kuna siku ambazo hautalala hata siku mbili nzima uko macho na unatakiwa kuwa active na makini kwa muda wote huo na utimize majukumu yako kwa ukamilifu na ufanisi wa hali ya juu bila chembe ya errors.

Ni kazi yenye mengi nyuma ya pazia kuzidi suti za kaunda na nyaya masikioni unazoziona na kuvutiwa nazo kwa maafisa walio kwenye Protection Unit.

Ni kazi ambayo shughuli zake zinatekelezwa kila siku kwa kiwango kikubwa cha 'urgency'!
Ni kazi ambayo maisha yako yanakuwa hatarini kila siku unayoishi.

Ni kazi ambayo ukitaka kuimudu kwa usahihi unapaswa kuwa na uzalendo haswa moyoni.

Ukijitathimini na kujiona unatosha… basi muombe Mungu, siku moja labda itakuwa!

"Kiwango cha juu zaidi cha uzalendo, ni kutoa utumishi kwa nchi yako"
 
1.kuna wanaosema unaweza kuwa spotted na kuwa recruited toka ukiwa mdogo kwa maana shule ya msingi au sekondari ukweli wa hili upoje?

2. Na vipi ikiwa hukupata fursa hiyo ukiwa mdogo lkn wakagundua kuwa wewe i potential ukiwa umri umeenda say 40 yrs and above?

3. Je unaweza kutumiwa na idara hii bila mwenyewe kujifahamu?..yaani unaweza kuwa nao na kuwafanyia kazi bila mwenyewe kujijua?
 
1.kuna wanaosema unaweza kuwa spotted na kuwa recruited toka ukiwa mdogo kwa maana shule ya msingi au sekondari ukweli wa hili upoje?

2. Na vipi ikiwa hukupata fursa hiyo ukiwa mdogo lkn wakagundua kuwa wewe i potential ukiwa umri umeenda say 40 yrs and above?

3. Je unaweza kutumiwa na idara hii bila mwenyewe kujifahamu?..yaani unaweza kuwa nao na kuwafanyia kazi bila mwenyewe kujijua?

1. Hii kitu hakipo sana siku hizi unaless kama kuna uhitaji maalumu sana wa shughuli fulani mahususi for the future... Ila hiki kitu sio common sana siku hizi
Na hata ikiwa hivyo mtoto mwenyewe hawezi kumbiwa nini kinaendelea... Mara nyingi tu mambo fulani fulani tu yanafanyika ili kumshape vile anatakiwa awe na kum-lure kwenye kusudi la Idara.

But as I said, hiki kitu sio common siku hizi, ni almost kama hakipo tena.


2. Mara nyingi ni ngumu kuwa recruited liwa afisa ukivuka 28 years... Lakini potentil ya mtu ndio kitu kikubwa zaidi... Na mara nyingi watu wanafanywa "assets" regardless of their age... Ila kwa miaka hii uliyotaja (40 years and above) kama akowa recruited basi ni kwa shughulo maalumu/mahususi kwa maoni yangu.


3. Kabisa inawezekana. Na kuna watu wengi sana wanatumikia/kutumiwa na Idara bila wenyewe kujijua. Kuna ofisi nyingi tu mabosi ni Vipepeo, so wafanyakazi wanafaaya kazi bila kujua boss wao halisi ni nani.
 
Nahitaji kuwa kwani nafikiri naweza tena napenda sana kushiiriki katika ujenzi wa taifa letu nikiwa na nafasi yangu kama msomi wa ngazi wa uzamivu na ninayetembelea mataifa mbalimbali. Najihusisha na sayansi ya asili na huku kwa kweli kunahitaji usalama na uzalendo sana kwani watanzania wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa taifa hudanganywa na watu wasio wazalendo kuhusu mambo ya maslahi ya taifa. Tafadhali nijulishe nifanye nini niweze kutoa mchango wangu kupitia usalama wa taifa.
 
Nahitaji kuwa kwani nafikiri naweza tena napenda sana kushiiriki katika ujenzi wa taifa letu nikiwa na nafasi yangu kama msomi wa ngazi wa uzamivu na ninayetembelea mataifa mbalimbali. Najihusisha na sayansi ya asili na huku kwa kweli kunahitaji usalama na uzalendo sana kwani watanzania wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa taifa hudanganywa na watu wasio wazalendo kuhusu mambo ya maslahi ya taifa. Tafadhali nijulishe nifanye nini niweze kutoa mchango wangu kupitia usalama wa taifa. 0686997270

Fazil,

Binafsi sina uwezo wa kufanya connection yoyote huko (wewe na Usalama)

Lakini naamimi wahusika wapo humu na kama wanaona inafaa basi watakutafuta kwa hiyo namba yako...


Lakini kuwa makini na matapeli.!!
 
Nahitaji kuwa kwani nafikiri naweza tena napenda sana kushiiriki katika ujenzi wa taifa letu nikiwa na nafasi yangu kama msomi wa ngazi wa uzamivu na ninayetembelea mataifa mbalimbali. Najihusisha na sayansi ya asili na huku kwa kweli kunahitaji usalama na uzalendo sana kwani watanzania wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa taifa hudanganywa na watu wasio wazalendo kuhusu mambo ya maslahi ya taifa. Tafadhali nijulishe nifanye nini niweze kutoa mchango wangu kupitia usalama wa taifa. 0686997270

We haufai mpaka hapo,, kirahisi rahisi tu umeweka na mawasiliano yako hadharani
 
Back
Top Bottom