Unadhani kwanini Watanzania wengi wanamkubali Rais Samia?

Unadhani kwanini Watanzania wengi wanamkubali Rais Samia?

kama mihemko na wivu vinakusaidia ongeza juhudi zaidi,
ila kaa ukijua Dr.Samia Suluhu Hassan ndio habari ya mioyoni mwa waTanzania wengi šŸ’
Watu wanadhani hii kazi yako ni rahisi, waambie na wao wajaribu kuwa chawa waone kama wataweza
 
kua
Watanzania wapi mjombaa...maana huku chini walala hoi hatumpendi,tena kina mama wezake ndo wanaongoza kutompenda.sasa sijui unawasemea watanzania gani?
kuanzia watoto wa chekechea hadi vyuo vikuu, wapiga kura na wasio wapiga kura wote wanamkubali mno kwa upendo mkubwa sana Dr Samia Suluhu Hassan šŸ’
 
Tukuulize wewe na familia yako , maana mnamkubali sio watz
Yes,
ni mimi pamoja na sehemu kubwa sana ya familia ya waTanzania ikiwemo ya humu JF tunampenda na tunamkubali sana Dr Samia suluhu Hassan bila mbambamba za wengineo mathalani wenye mihemko na ghadhabu ambazo hazina maana yoyote šŸ’
 
Nipo kwenye mwendokasi apa..nikawa nasoma vichwa vya mada nikakutana na hii yako nikatukana tusi kubwa kimoyomoyo naona watu wananishangaa kumbe nimetukana kwa sauti .... mkuu kwanini mnapenda kuwasababishia watu zambi za makusud
si ndicho kilichokujaa moyoni na akilini mwako na ndicho unachoweza kufanya...
kama mihemko hiyo inakusaidia komaa nayo utatoboa gentleman šŸ’

Lakini ndio hivyo tena waTanzania wengi wanashow love kubwa sana kwa Dr.Samia Suluhu Hassan bila mbambamba yoyote, right?šŸ’
 
Daah

Machawa mnatumia nguvu nyingi sana ila moyon mnajua kuwa mnafanya unafiki
 
Ni kwasababu ya makusudi, haja na nia yake thabiti, ya wazi na njema ya kutaka kuibadili tanzania kiuchumi, kijamii na kusiasa?

Au ni kwasababu ya umadhubuti wa sera, mipango, mikakati, jitihada, bidii na umahiri wake katika kutekeleza kwa weledi sana na kwa ufasisi mkubwa mno miradi mtambuka ya maendeleo inayogusa mojakwamoja maisha ya watanzania kama vile maji, afya, elimu, kilimo, viwanda, uvuvi, miundombinu, usafirishaji N.K?

Au ni kwasababu ya amani liliyopo, ulinzi, usalama, uhuru, haki, utulivu, usawa, uwazi na uwajibikaji wake katika kuongoza nchi kwa misingi ya utawala wa sheria na kwa kuzingatia katiba ya nchi?

Au ni kwasababu ya matumani makubwa waliyo nayo Watanzania kwake, kwamba ndie pekee kiongozi wa kisiasa nchini, anae weza kutimiza ndoto na matarajio yao, ya maisha bora?

Kwa maoni yako, unadhani ni kwanini Samia Suluhu Hassan, anapendwa na kuaminika kiasi hiki, kitaifa na kimataifa?
hata samia akiona huu uzi wako atastaajab sana yaan unamsifia kwa vitu hajawai kuvifanya yaan hata yye atakukana,, umeshindwa kabisa kuwa chawa mkuu umekua mnafki kabisa

NONSENSE!
 
Mheshimiwa mbunge ,kiongozi na msemaji wa matatizo ya wananchi wa jimbo lako duh😁😁😁😁😁, umeshindaje mkuu?
Namshukuru Mungu sana kwa Neema na Baraka anazonijalia nina afya na nguvu tele, kwa ujumla each and everything are under full control na tunasonga kifua mbele, wanainchi wanakubali na kuunga mkono yanayoendelea mjengoni na field jimboni...

na kwakweli matumani ya kufanya vizuri zaidi huko mbeleni yapo juu sana, na Imani na mapendo makubwa ya waTanzania wengi ni kwa Dr Samia Suluhu Hassan,

Lakini kama Jimbo matumani ya wananchi bado ni makubwa mno kwa kiongozi wao mchapakazi hodari, makini asiechoka wala kukata tamaa Tlaatlaah ..haijaisha mpka iishe šŸ’

Natumai hujambo na unasonga mbele kwa amani...
Mungu Ibariki Tanzania..
 
Daah

Machawa mnatumia nguvu nyingi sana ila moyon mnajua kuwa mnafanya unafiki
huna haja kughadhabishwa na upendo wa waTanzania kwa Dr Samia Suluhu Hassan kwasabb ni upendo wa dhati usio pimika mkuu šŸ’
 
Humu JF hakuna Rais aliyewahi kukubalika na kupendwa. Tokea JF ianzishwe sijawahi kuona Rais aliyeko madarakani akipendwa. Hata hivyo kila uchaguzi hakuna Rais aliyeshindwa, wote walishinda kwa kishindo.
Hata huyo Samia H, naye atashinda tu tena kwa kishindo.
 
unaelewa kuna mambo ukiskia hata kama ulikua umekata tamaa unapata faraja na nguvu mpya, Ari na bidii ya kitofauti kukamilisha ndoto zako za maisha,

waTanzania wengi wakimskiza tu Dr Samia Suluhu Hassan wanapata nguvu ya ajabu kwamba ndoto na matarajio yao yanakwenda kufikiwa aisee!!? šŸ’
Mbona unahangaika sana Bro?fanya uchunguzi mdogo tu kama nilioufanya hapa nimeupitisha huu uzi wako hapa kibaruani kwangu kiukweli,hakuna kijana hata mmoja aliekiri kuwa ni kweli ulisemalo tafadhali muwe mnajipanga mnavyoleta uzushi haikusaidii lolote kama Mtanzania kuandika jambo ambalo unajua wazi sio la kweli hivi mnajua kuna maisha baada ya Mama yenu?kama wewe ni chawa huna haja ya kusumbua watu ita familia yako waambie haya mapambio mnawasababishia watu matatizo tukisema ukweli mnatuteka kama anapendwa mnahangaika nini kupandisha nyuzi humu yaani mpaka inakua kero please behave guys uchawa ni usenge
 
Ni kwasababu ya makusudi, haja na nia yake thabiti, ya wazi na njema ya kutaka kuibadili tanzania kiuchumi, kijamii na kusiasa?

Au ni kwasababu ya umadhubuti wa sera, mipango, mikakati, jitihada, bidii na umahiri wake katika kutekeleza kwa weledi sana na kwa ufasisi mkubwa mno miradi mtambuka ya maendeleo inayogusa mojakwamoja maisha ya watanzania kama vile maji, afya, elimu, kilimo, viwanda, uvuvi, miundombinu, usafirishaji N.K?

Au ni kwasababu ya amani liliyopo, ulinzi, usalama, uhuru, haki, utulivu, usawa, uwazi na uwajibikaji wake katika kuongoza nchi kwa misingi ya utawala wa sheria na kwa kuzingatia katiba ya nchi?

Au ni kwasababu ya matumani makubwa waliyo nayo Watanzania kwake, kwamba ndie pekee kiongozi wa kisiasa nchini, anae weza kutimiza ndoto na matarajio yao, ya maisha bora?

Kwa maoni yako, unadhani ni kwanini Samia Suluhu Hassan, anapendwa na kuaminika kiasi hiki, kitaifa na kimataifa?
Acha propaganda wewe. Kwani nani anampenda samia? Huyu amekuja na sera ya kukabidhi nchi kwa fisadi? Huyu anauza nchi kwa wageni eti ndio uwekezaji? Wrwe hukusoma masharti yale ya mkataba wa bandari na dubai? Huyu samia mwenyewe ana tamaa ya kujitajirisha yeye na familia yake. Huyu mwenye kujijengea mahekalu ya kifahari? Huyu asiyeweza hata kumsikiliza mama mnyonge aliyetaka kumueleza shida yake?
Wananchi watamshukuru sana kama atahakikisha anarejesha uongozi kwa mzalendo aina ya magufuli. Mtu jasiri mwenye maona sahihi kwa mstakabali kiuchumi wa umma wa wananchi wa tanzania. Akifanya hivyo tutamkumbuka. Tunajua hakujitayarisha wala hakua na uwrzo kua rais. Limetokea kwa ajali.
 
Rais Samia anapendwa na kukubalika na mamillioni ya watanzania kwa sababu amekidhi matarajio ya watanzania na kukata kiu waliyokuwa nayo juu ya aina ya kiongozi waliyekuwa wanamuhitaji.

Kwa ufupi Mama yetu mpendwa na kipenzi cha watanzania ni jibu na jawabu kwa mahitaji ya watanzania.
Wewe ni walewale wenye tenda kumsifu mama bure kwa mapambio na nyimbo.
 
Endeleeni kumdanganya huyu Mama, na nadhani ccm hakuna uchaguzi watamwaga hela kama uchaguzi ujao, na wizi wa waziwazi wa kura.
 
Back
Top Bottom