Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Umesema sahihi mtoa mada, Vijana wajitahidi kujenga kabla hawajafika huo umri

Of course huo ni umri wa mtu kupumzika na kusubiria kifo tu

Suala la kujenga, kusomesha linapaswa uwe ulishamaliza kabla ya 55

Jambo la kuzingatia kwa Wazee wenzangu ni kutofanya kosa la kuzalisha katika umri huo

Huo ni umri wa kucheza na Wajukuu sio kuanza kusomesha watoto wako eti wakiwa shule ya msingi 🙌
Kuna wengine kwenye umri huo wanafukuzia teuzi, unawashauri nini?
 
Kuna wengine kwenye umri huo wanafukuzia teuzi, unawashauri nini?
Hao ni wavivu wa kufikiri

Wanaamini maisha bora yanapatikana kwenye teuzi

Kumbe unaweza kupambana kufanya uwekezaji wako kwenye biashara n.k ukiwa na miaka 35, ukija kufika hiyo 65 tayari unakuta na biashara ina matawi Miko yote Tanzania Bara na Nchi za jirani
 
Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k

Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri?

Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji.

Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?
Jenga chini brother
 
Back
Top Bottom