Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,340
Reaction score
56,050
Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k

Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri?

Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji.

Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?
 
Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri? Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji. Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?​
This thread can be used to explain why you are still very poor mentally.
 
Uwezo kama unaona Jenga tu mkuu.
Ukifikiria Sana hauwezi kufanya lolote hapa Duniani.
Hebu Angalia, baada ya kuhangaika kote hapa Duniani ila mwisho wa siku unakufa tu unaacha Kila kitu.
Kwahiyo kama uwezo unao, Jenga, kama hauna uwezo wa kujenga siyo lazima
 
Uwezo kama unaona Jenga tu mkuu.
Ukifikiria Sana hauwezi kufanya lolote hapa Duniani.
Hebu Angalia, baada ya kuhangaika kote hapa Duniani ila mwisho wa siku unakufa tu unaacha Kila kitu.
Kwahiyo kama uwezo unao, Jenga, kama hauna uwezo wa kujenga siyo lazima
Na uzuri hata ukifa watu watutumia tu
 
Wewe jamaa either umesoma sana lakini unfortunately elimu yako hauifanyii kazi au haujasoma kabisa ndiyo maana kuna wakati unakuwa na uoni hafifu sana kwenye ishu ya makazi ambao kimantiki uoni huo ilibidi wawe nao watoto wadogo kama siyo wachanga.

Umesema nikiwa 65 natakiwa nisijenge nyumba ushauri wako nikalale nje chini ya mwembe?ok nikapange umejiuliza siku nikikosa kodi nani atanilipia hiyo kodi?je kama Mungu amenipa umri mrefu utanishauri tena nijiue kutokana na madhila ya kufukuzwa upangaji?wewe tulia tu kwenye hilo banda alilojenga mzee wako siku ndugu mligombanie ndiyo utajua ulikuwa unaandika vitu huvijui na nina uhakika utagombania mgao wako vile vile wakati wewe kujenga hutaki.
 
Hoja yako imekaa kibinafsi sana,

Ni sawa na kusema kua una umri wa miaka 65 unapanda mti wa matunda wa kazi gani?
Hata ukijenga Nyumba ukiwa na umri wa miaka 20 tu,unaweza kufa baada ya miezi kadhaa tu na Nyumba usiifaidi,

Kama uwezo wa kujenga upo,jenga tu haijalishi una umri gani,
kwani ukijenga Nyumba wakati una umri mdogo,una uhakika gani kua utaishi kwenye hiyo Nyumba yako kwa muda mrefu?

Love the life u live
Live the life u love.
 
Back
Top Bottom