Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Mimi sizimi simu na pia naweka antitheft active yani simu ikibebwa tu inaanza kupiga mikelele .....hii ni baada ya wezi kunichapa pc, na simu zangu usiku mimi nikiwa bize kucheki mpila
Pole Sana boss
 
ushukuru ulizima Mana hawakujua waende nyumba ipi kwani GPS iligoma kuonyesha upendo

Ulivofatilia ulitambua walitaka nn
 
Daa watu mna mawazo mazuri sana asee but kwenye hayo mawazo yenu sioni positive thinking za uoande wa pili, kila mtu sizimi sizimi.

Haya umelala simu ipo on na jamaa wapo mlangoni, dirishani inshort mwingine tayari yupo ndani jirani anakupigia, what next?.

Haya usiku 0430hrs unapigiwa kafariki au njoo ofisini na huna usafiri what next?.

Hizi ni just a story tu ila kwenye real issues haiwezi kuwa hivyo, hata wezi wanajua hayo yote maana kwenye vikao vya mtaani nawao huwa wapo na wanatoa mawazo mazuri tu 😁!.
Hahaaaass
 
kaaah yaan watu wanakupigia simu kisa tu gari imepark nje na wakati uko pembezoni mwa barabara,, aaah huo kwangu ni usumbufu kabisa yaani majirani wa tabia izo siwataki kabisa...........,, kuna siku weekend niko OFF nimeamua kupumzika ilanmekuja pigiwa simu saa kumi na moja alfajiri ata sijaamka aseeh napokea uku macho yanauma naambiwa kuna paka getini kwangu daah kwakweli nilichukia sana,, Tangia apo naweza silent kuepuka usumbufu
 
Binafsi sipendi kuzima simu ..na sipendagi simu za usiku Jamani🤔
 
Huwa nazima simu usiku kwasababu sipendi usumbufu usiku,usiku ni muda wa kulala na kuipumzisha akili,nitafute mchana kutwa lakini si usiku.

Suala la mama kuumwa usiku hiyo ni emergency ambayo haikutarajiwa,hata kama simu ikiwa on halafu akaumwa usiku na mnakaa mikoa tofauti,utafanya nini?,mwanadamu tumeumbwa na tulipewa akili ya kupambanua mambo,mama yako anaumwa na anajua uko mbali inapaswa ajiongeze kwa watu wa karibu yake au majirani,sidhani kama mama yako hana hata ndugu anayeishi naye!.

Huwa nazima simu usiku kwa kuepusha habari mbaya za ghafla zitakazopelekea kukosa usingizi,kama tujuavyo usingizi ni muhimu na ndiyo maana tukapewa masaa 24,yaani 12 kupiga kazi na 12 kupumzika!,kama kutakuwa na taarifa mbaya ni bora nikutane nayo asubuhi nikishaamka maana akili itakuwa fresh!.

Kwangu mimi kuzima simu usiku ni jambo zuri kuliko kuiacha on.

Ya kwamba una hofia majambazi?,hebu jiulize kwa jiografia ya nchi yetu hii na mikoa tunayoishi,umepata tatizo la kuvamiwa na majambazi usiku ukapiga simu polisi watafika kwa wakati huo?,hii nchi tunajuana sana na wala tusidanganyane,umpigie uenda jirani yako atakusaidia nini na wazee wana mijegeje mikononi?.

Kwa kifupi hatuzimi simu usiku ili itulinde,bali tunazima simu usiku ili kuepusha usumbufu na kupata muda mzuri wa kupumzisha akili.
 
Uzime usizime simu ilipangwa hivyo pindi tu tangu uzaliwe. Kwa iyo siyo eti kwasabab usizime simu usiku. Hata huko kuzima simu usiku na gari kupaki na kuwasha taa ilishapangwa long time time pindi tu ulipozaliwa. Chochote ufanyacho kilipangwa. Hata wewe kuandika hii sreedi leo ilishapangwa long time.
"Wewe ni mpumbavu"
Hata hii kukutukana ilishapangwa toka nazaliwa🤬🤗
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom