Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Nitoe kisa kimoja cha kweli kilitokea zamani kidogo mwaka 1993 kipindi ndio simu zinaanza kuingia enzi hizo zilikuwa ni mobitel tu na tritel.Mtoto mmoja wa waziri wizara flani hapa nchini alikuwa anaoa.Vile baba yake alikuwa mtu mkubwa sana kwa vyovyote harusi ilikuwa kubwa na walipata zawadi nyingi sana na mikufu ya dhahabu.
Dogo alikuwa anakaa nyumba alijenga baba yake Kunduchi yenye flat moja.Walivorudi usiku na mkewe mpya wakiwa juu usiku wa manane mishale ya saa tisa kwa chini wakaona kuna kundi la majambazi wana mapanga yanawaka waka.Dogo akajua kimenuka.Alimpigia simu baba yake yeye alikuwa anaishi sio mbali sana na hapo baba yake akaenda polisi wakaja na defender ikiwa na kundi lenye maaskari na vya moja.
Ila landrove ilivyofika kwa fujo sana maaskari wakashuka majambazi wakajua kimenuka wakakimbilia porini.
Swali je baba yake angezima simu kingetokea nini?
Aiseeee,alinusurika
 
kuna miaka ya nyuma kidogo nilikiwa namiliki kibasi cha abiria simu ikipigwa usiku gari imearibika duu nishatoka na pensi la kulalia nakajikuta niko ubungo hapo ndio nilipoona umuhimu wa kuzima simu usiku napatatizo nayajua asubuhi tu
Pole Sana,Ila Anza kuiwasha
 
watu wenye mawazo ambayo ni mafupi huwa kila kitu wanaishia kusema ilishapangwa au mipango ya mungu.Majambazi wenye mapanga yanataka kuvunja geti waingie kwako una jirani yako ambaye ana bunduki kiasi kwamba unajua fika ukimpigia akiipiga bunduki tu juu jamaa wanakimbia sasa ukute amezima simu na hapo utasema mipango ya mungu.
Ni muhimu boss kuacha simu on,uko sawa
 
Ile line kwa ajili ya kazi ikifika saa mbili tu naizima.

But familia na wadau muhimu wanaifahamu line yangu nyingine hiyo inapatikana muda wote.

Kuna watu wengine hawana mipaka na privacy za wenzao mtu anakuletea maswala ya kazi saa nne usiku ukiwa umetulia nyumbani.

Zamani nilipokua kijana nilifurahia kuwa busy muda wote.

Ila kadri navyokuwa mzee naona umuhimu wa kupata some quality time at home.
Umeanza kuzeeka,hahahaaa
 
Uzime usizime simu ilipangwa hivyo pindi tu tangu uzaliwe. Kwa iyo siyo eti kwasabab usizime simu usiku. Hata huko kuzima simu usiku na gari kupaki na kuwasha taa ilishapangwa long time time pindi tu ulipozaliwa. Chochote ufanyacho kilipangwa. Hata wewe kuandika hii sreedi leo ilishapangwa long time.
Hizi dhana za ilipangwa wakati mwingine yafaa tuzikae kabisa mawazoni mwetu.
Ina maana waafrika ilipangwa tuwe masikini tu
 
Type kisa basi Demi
Kuna kipindi mwanangu alikuwa kwa bibi yake kwa muda, akawa anatokea huko kuelekea shule. Kuna siku ikatokea kaenda shule hakurudi na school bus imepita.
Nilitafutwa hiyo jioni na usiku wote sikupatikana, na mimi pekee ndio nina contacts za shule.
Kesho yake nakuja kupatikana kupewa taarifa nilikaribia kuzimia.

Tangu siku hiyo sizimi simu kabisa tena naweka volume kubwa
 
Kila Jambo Lina Mungu,nakubali kabisa
 
Kuna kipindi mwanangu alikuwa kwa bibi yake kwa muda, akawa anatokea huko kuelekea shule. Kuna siku ikatokea kaenda shule hakurudi na school bus imepita.
Nilitafutwa hiyo jioni na usiku wote sikupatikana, na mimi pekee ndio nina contacts za shule.
Kesho yake nakuja kupatikana kupewa taarifa nilikaribia kuzimia.

Tangu siku hiyo sizimi simu kabisa tena naweka volume kubwa
Pole Sana,dogo alienda wapi? Hawa wanetu hawa!
 
Mimi nikishalewaga mimi na simu yangu wote tunazima. Tunakuja kuamshana asubuhi atakayemwahi mwenzake kama ni mimi au alarm.
Punguza basi pombe,au uache kabisa
 
Unaweza arrange namna ya kuondoka kabla hujaenda kazini, kuna pesa nk, wanaweza fika hospitali dawa zikakosekana wakahitaji pesa ili utatue changamoto hiyo.
Unawaza kwa MAKALIO
Mambo ni mengi mno
 
kaaah yaan watu wanakupigia simu kisa tu gari imepark nje na wakati uko pembezoni mwa barabara,, aaah huo kwangu ni usumbufu kabisa yaani majirani wa tabia izo siwataki kabisa...........,, kuna siku weekend niko OFF nimeamua kupumzika ilanmekuja pigiwa simu saa kumi na moja alfajiri ata sijaamka aseeh napokea uku macho yanauma naambiwa kuna paka getini kwangu daah kwakweli nilichukia sana,, Tangia apo naweza silent kuepuka usumbufu
Paka!!Kali hiyo
 
Kama nimekusoma umesema wanafunzi wanakupigia simu usiku, mimi boss wangu hawezi kunipigia simu usiku wala sina mwanafunzi.anipigiae usiku.Siku moja moja napiga simu huko kwenye asili yetu teeena mwisho saa tatu baada ya hapo simu ipo kimya ukiona sms ujue tigo au voda na matangazo yao mkuu.Na simu ya usiku ujue zaidi ya 3 au 4 ujue ni janga la haja siyo mchezo
Nimekuelewa mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom