Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Huwa nazima simu usiku kwasababu sipendi usumbufu usiku,usiku ni muda wa kulala na kuipumzisha akili,nitafute mchana kutwa lakini si usiku.

Suala la mama kuumwa usiku hiyo ni emergency ambayo haikutarajiwa,hata kama simu ikiwa on halafu akaumwa usiku na mnakaa mikoa tofauti,utafanya nini?,mwanadamu tumeumbwa na tulipewa akili ya kupambanua mambo,mama yako anaumwa na anajua uko mbali inapaswa ajiongeze kwa watu wa karibu yake au majirani,sidhani kama mama yako hana hata ndugu anayeishi naye!.

Huwa nazima simu usiku kwa kuepusha habari mbaya za ghafla zitakazopelekea kukosa usingizi,kama tujuavyo usingizi ni muhimu na ndiyo maana tukapewa masaa 24,yaani 12 kupiga kazi na 12 kupumzika!,kama kutakuwa na taarifa mbaya ni bora nikutane nayo asubuhi nikishaamka maana akili itakuwa fresh!.

Kwangu mimi kuzima simu usiku ni jambo zuri kuliko kuiacha on.

Ya kwamba una hofia majambazi?,hebu jiulize kwa jiografia ya nchi yetu hii na mikoa tunayoishi,umepata tatizo la kuvamiwa na majambazi usiku ukapiga simu polisi watafika kwa wakati huo?,hii nchi tunajuana sana na wala tusidanganyane,umpigie uenda jirani yako atakusaidia nini na wazee wana mijegeje mikononi?.

Kwa kifupi hatuzimi simu usiku ili itulinde,bali tunazima simu usiku ili kuepusha usumbufu na kupata muda mzuri wa kupumzisha akili.
Hapo Sasa!

luckyline Mama yako Yuko mbali na wewe, akiumwa usiku simu itamponya?.

Hivi wale watalamu wa mionzi wanasemaje kuhusu kulala na simu zikiwa on kitandani.

Japo na Mimi Huwa sizimi simu,Lengo ni kuangalia muda ninaposhituka usiku na mwanga ikitokea umeme umekata.
 
Unaweza arrange namna ya kuondoka kabla hujaenda kazini, kuna pesa nk, wanaweza fika hospitali dawa zikakosekana wakahitaji pesa ili utatue changamoto hiyo.
Unawaza kwa MAKALIO
 
Unaona jinsi ulivyo okoka endapo ungepigiwa na kupatikana ukatonywa kinachoendelea nje ungetoka na kuharibu dili za watu na ingewezekana wangekushambulia
 
Nimefurahi unavyompenda mama,Safi boss
Wewe acha tu kuna wakati nawaza mengi mpaka nasemms mungu akismua kuchukua basi anichukuwe mimi
Wewe na Mama yako... . Msogeze uishi nae tuu awe karibu na wewe.
Anakujaga na kurudi, mwezi mmoja tu anarudi.ingawa hawezagi maliza huo mwezi ila hata mimi siwezi muruhusu amalize zaidi ya mwezi mjini.
Mjini ni kukaa ndani hana kazi so anakosa mazoezi anaweza develop magonjwa ya uzembe.
Ila kijijini ni full mazoezi anakimbizana na wafanyakazi wake mashambani, mara kanisani, mara kwenye hisa, mara mifugo yake siku nzima yupo busy hayo ndo mazoezi yenyewe.
 
Ile line kwa ajili ya kazi ikifika saa mbili tu naizima.

But familia na wadau muhimu wanaifahamu line yangu nyingine hiyo inapatikana muda wote.

Kuna watu wengine hawana mipaka na privacy za wenzao mtu anakuletea maswala ya kazi saa nne usiku ukiwa umetulia nyumbani.

Zamani nilipokua kijana nilifurahia kuwa busy muda wote.

Ila kadri navyokuwa mzee naona umuhimu wa kupata some quality time at home.
 
Uzime usizime simu ilipangwa hivyo pindi tu tangu uzaliwe. Kwa iyo siyo eti kwasabab usizime simu usiku. Hata huko kuzima simu usiku na gari kupaki na kuwasha taa ilishapangwa long time time pindi tu ulipozaliwa. Chochote ufanyacho kilipangwa. Hata wewe kuandika hii sreedi leo ilishapangwa long time.
watu wenye mawazo ambayo ni mafupi huwa kila kitu wanaishia kusema ilishapangwa au mipango ya mungu.Majambazi wenye mapanga yanataka kuvunja geti waingie kwako una jirani yako ambaye ana bunduki kiasi kwamba unajua fika ukimpigia akiipiga bunduki tu juu jamaa wanakimbia sasa ukute amezima simu na hapo utasema mipango ya mungu.
 
Nitoe kisa kimoja cha kweli kilitokea zamani kidogo mwaka 1993 kipindi ndio simu zinaanza kuingia enzi hizo zilikuwa ni mobitel tu na tritel.Mtoto mmoja wa waziri wizara flani hapa nchini alikuwa anaoa.Vile baba yake alikuwa mtu mkubwa sana kwa vyovyote harusi ilikuwa kubwa na walipata zawadi nyingi sana na mikufu ya dhahabu.
Dogo alikuwa anakaa nyumba alijenga baba yake Kunduchi yenye flat moja.Walivorudi usiku na mkewe mpya wakiwa juu usiku wa manane mishale ya saa tisa kwa chini wakaona kuna kundi la majambazi wana mapanga yanawaka waka.Dogo akajua kimenuka.Alimpigia simu baba yake yeye alikuwa anaishi sio mbali sana na hapo baba yake akaenda polisi wakaja na defender ikiwa na kundi lenye maaskari na vya moja.
Ila landrove ilivyofika kwa fujo sana maaskari wakashuka majambazi wakajua kimenuka wakakimbilia porini.
Swali je baba yake angezima simu kingetokea nini?
 
Binafsi sizimi simu usiku, nikiona namba ngeni sipokei ikikata napiga mimi chap, ili kudominate maongezi. Hata nipigiwe saa usiku nitaamka, siweki silent mode hata siku moja, nitaweka sauti lkn nitapunguza kiasi kwamba mtu akipiga lazima nitasikia tu.
 
Unaweza kuta una jamaa yako au mtoto wako kapata ajali mbaya anahitaji umuongezee damu maana group lake ni adimu sana la AB(-) wewe baba yake ndio pekee mji mzima mwenye damu hiyo na lazima ipatikane usiku huo ikifika asubuhi mtoto wako atapoteza maisha.Unapigiwa simu umeizima.
Unadhani kitakachotokea ni nini? RIP utajua maisha yako yote.

Mnaosema mnazima simu za kazini mwenu kumbuka hata kupanda vyeo pia kujitoa muda wa ziada ni moja ya sifa kuu.Unapigiwa simu kuwa umesahau kufunga koki ya maji ofisini kwako na mlinzi na yale maji yakitoka yatachuruzika mwishowe yataingia store ambapo kuna kemikali ambazo zikikutana na maji zinalipuka na zikilipuka kiwanda kitawaka moto.
Unapigiwa simu umezima matokeo yake kiwanda kinaungua jibu ni kwamba 1.Uzembe kwa kutokuwa mwangalifu 2.Kazi itakuwa imeisha sababu kiwanda kimeungua.........................''Akili zako changanya na akili za kuambiwa'' ..........nukuu ya mhe flani raisi mstaafu hapa ndio mahali pake.
 
zamani ni zamani bro maisha yanakwenda kasi sana.Nikupe mfano mbona zamani kulikuwa hakuna magari na watu walikuwa wanasafiri,Jibu ni kwamba walikuwa wanachukua muda mrefu sana na walikuwa hawa feel ila jaribu wewe uone ile feeling itakuumiza sana.Mambo yanakwenda kwa kuji adjust.
 
Wewe acha tu kuna wakati nawaza mengi mpaka nasemms mungu akismua kuchukua basi anichukuwe mimi

Anakujaga na kurudi, mwezi mmoja tu anarudi.ingawa hawezagi maliza huo mwezi ila hata mimi siwezi muruhusu amalize zaidi ya mwezi mjini.
Mjini ni kukaa ndani hana kazi so anakosa mazoezi anaweza develop magonjwa ya uzembe.
Ila kijijini ni full mazoezi anakimbizana na wafanyakazi wake mashambani, mara kanisani, mara kwenye hisa, mara mifugo yake siku nzima yupo busy hayo ndo mazoezi yenyewe.
Safi sana
 
Unaweza kuta una jamaa yako au mtoto wako kapata ajali mbaya anahitaji umuongezee damu maana group lake ni adimu sana la AB(-) wewe baba yake ndio pekee mji mzima mwenye damu hiyo na lazima ipatikane usiku huo ikifika asubuhi mtoto wako atapoteza maisha.Unapigiwa simu umeizima.
Unadhani kitakachotokea ni nini? RIP utajua maisha yako yote.

Mnaosema mnazima simu za kazini mwenu kumbuka hata kupanda vyeo pia kujitoa muda wa ziada ni moja ya sifa kuu.Unapigiwa simu kuwa umesahau kufunga koki ya maji ofisini kwako na mlinzi na yale maji yakitoka yatachuruzika mwishowe yataingia store ambapo kuna kemikali ambazo zikikutana na maji zinalipuka na zikilipuka kiwanda kitawaka moto.
Unapigiwa simu umezima matokeo yake kiwanda kinaungua jibu ni kwamba 1.Uzembe kwa kutokuwa mwangalifu 2.Kazi itakuwa imeisha sababu kiwanda kimeungua.........................''Akili zako changanya na akili za kuambiwa'' ..........nukuu ya mhe flani raisi mstaafu hapa ndio mahali pake.
Umeelezea haswa boss
 
Binafsi sizimi simu usiku, nikiona namba ngeni sipokei ikikata napiga mimi chap, ili kudominate maongezi. Hata nipigiwe saa usiku nitaamka, siweki silent mode hata siku moja, nitaweka sauti lkn nitapunguza kiasi kwamba mtu akipiga lazima nitasikia tu.
Safi kiongozi
 
kuna miaka ya nyuma kidogo nilikiwa namiliki kibasi cha abiria simu ikipigwa usiku gari imearibika duu nishatoka na pensi la kulalia nakajikuta niko ubungo hapo ndio nilipoona umuhimu wa kuzima simu usiku napatatizo nayajua asubuhi tu
Salaam wana jukwaa,Kuna hii tabia ya kuzima simu usiku mwa kuepuka usumbufu wa calls na sms.

Je, ulishawahi kuzima simu usiku then ukajutia? Tujitahidi kuacha simu zetu on kila wakati.

Mimi Kuna siku nilizima simu usiku then nikalala,kumbe usiku wa Kama saa sita Kuna gari ilikuja ikapaki barabarani,karibu na nyumba yangu,(Mimi naishi pembezoni mwa barabara,Tena kilimani).

Sasa majirani zangu wanaokaa bondeni kidogo wakaiona ile gari,imewasha taa,Ila haiondoki wakajaribu kunipigia wakakuta simu iko off.

Ashukuriwe Mungu baada ya muda gari ikaondoka.

Asubuhi ndo wananiuliza kwanini ulizima simu?

Km wenye gari walikuwa na lengo baya ungesaidikaje?

Nami nikajifunza kitu,ikiwezekana acha simu yako on usiku.

Kazi iendelee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom