DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 544
- 558
Kwa mantiki hiyo unataka utuaminishe kuwa wanaohombea wasiwekewe sharti ya elimu wala umri. Alafu hapohapo wanaopiga kura wawe kuanzia miaka 18+..!? Hhahahhhaa sasa hizo zitakua hesabu za wapi bwa shee??Kwa nini liwe taifa la wendawazimu kuruhusu kila mtu kugombea bila kujali vyeti wala umri?
Kuweka vigezo vya umri na vyeti ni ubaguzi unaoashiria walioweka vigezo hivyo hawaamini uwezo wa wapiga kura kufanya maamuzi sahihi pale wanapopelekewa mgombea kijana asiye na vyeti na yule mzee mwenye vyeti. Kama ni kweli wapiga kura sisi hatuwezi kutanabahisha mgombea anayefaa mpaka Katiba ituchagulie, huyo msomi mzee anashindwa nini kuja kutushawishi tumchague?
Naamini wapiga kura ni watu wazima (miaka 18+) na ni wenye akili timamu, wenye uwezo wa kujua ni yupi mgombea sahihi wa kupewa kura.
Tumebarikiwa akili na utashi kiasi ili maisha yetu yaende vizuri tuweze kupangilia mambo. Na ndio tukawekewa utaratibu kuwa kila jambo lina Wenye. Sasa hii wenye hii ndio hizo qualifications and qualities