Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,661
- 46,349
Naona baadhi ya watu wanashangilia kama jambo jema na kubwa sana kwamba kuna kijana wa miaka 44 kutoka chama cha upinzani huko Senegal anakaribia kutwaa madaraka ya Urais baada ya kupigiwa kura nyingi zaidi na raia wa huko.
Watu wanaoshangilia jambo hili wanasahau kwamba mojawapo ya matatizo makubwa ya watawala wa Africa ni kung'ang'ania madarakani kwa muda mrefu, na wengi wa ving'ang'anizi wa madaraka walianza kutawala wakiwa vijana wenye umri mdogo sana.
Unapomchagua mtu mwenye miaka 44 ina maana akitawala miaka 10 kama zilivyo katiba za nchi nyingi anatakiwa aondoke madarakani akiwa na miaka 54, sasa hapo ndipo sarakasi za kucheza na katiba huwa zinaanza kwa sababu inakuwa bado mapema mno kwake na kwa wapambe wake.
Marais katika nchi nyingi za Africa wanatakiwa waingie madarakani angalau na umri kuanzia miaka 65 ili akitawala miaka 10 inakuwa imefika 75 na anakuwa amechoka kuendelea kutawala na kufanya mapambano ya kisiasa, anamwachia mwingine. Vinginevyo kuwapa madaraka vijana kuna hatari ya kutawailia na mtu mmoja hata miaka 20 au 30 kama ilivyo katika nchi nyingi za Africa.
Zaidi naamini wazee wana uzoefu na busara zaidi za kuongoza katika nafasi kubwa kuliko vijana, pia hata inakuwa rahisi kuwafahamu kutokana na majukumu yao mbalimbali waliyokwisha kupitia.