Umesoma vitabu gani mwaka 2018?

List yangu ni kama ifuatavyo
1.The monk who sold his Ferrari-Robin Sharma
2.The Biggest secret-David Icke [kinaogopesha nimeishia nusu]
3.A new Earth-Eckhart Tolle
4.Lost book of the bible
6.Eat that frog-Brian Tracy
7.The 5 languages, the secret to love that last-Gary Chapman
8.Life is what you make it-Preeti Shenoy
9.Mars and Venus in the bedroom-John Gray
10.The book of Enoch
11.Master-George Leonard
12.The four Agreement-Don Miguel Ruiz
13.How to deal with emotion explosive people-Albert J. Bernstein
14.101 way to make money in Africa-Harnet Bokrezion
15.How to analyze people by sight- E.LBenedict & R.P Benedict
16.Chicken soup for the soul-Jack Canfiled
17.Gideon's spies the secret history of the Mossad-Gordon Thomas
18.A history of knowladge -Charles van Doren [Naendelea nacho sijakimaliza]
 
1: Sababu pekee za Kumuabudu Mungu ambazo ndizo wanazozitoa viumbe wa mbinguni kama kwa nini wanamuabudu Mungu ni MBILI i/ Muumbaji wa Vyote 2/ Tukio La Yesu Kufa Ili Kumpandisha hadhi mwanadamu atakayemuamini, Kutoka kuwa mdhambi asiye na Muelekeo wowote hadi Kuwa MTOTO wa Mungu Ambaye hamuiti tu Mungu bali ABBA yaani BABA. Sio tena Mungu na Mwanadamu Bali Baba na MTOTO aliyezungukwa na hatari.

2: Sabato ni Ishara pekee inayomtaka Mwanadamu Kumkumbuka Mungu kama Muumbaji wa Ulimwengu kwa siku (Lateral Days) Sita. Hii Itamlinda mwanadamu na nadharia zote potoshi juu ya Kazi na Uumbaji wa Mungu. Ndio Maana hata Yesu (Aliyeshiriki uumbaji) alisema Iliwekwa kwa ajili ya MWANADAMU sio MYAHUDI. Hapa kuna mitazamo mingi yenye utetezi mwingi kinzani ila kwangu mimi huu ndio sahihi kabisa

3: Nje ya mahusiano Binafsi (sio ya kikundi au kidini ) na Mungu, Juhudi zote za mwanadamu ni bure. Hiki ndio Kinapaswa kuwa kipaumbele namba moja cha Kila mwanadamu anayejitambua na hakizuii kufanya mambo mengine ya maendeleo.

4: Kuna Upotovu Mkubwa sana Katika Ulimwengu wa Imani dunia ya Sasa. Ila Wengi Hawajui. Hata wanaodhani wanajua wanajua kwa juujuu. Kuna kasi kubwa ya Modernization ya ancient paganism ambazo zinachanganywa katika imani subliminally.
Kilele cha mchanganyiko huu ambao unawaunganisha watu wa imani, wasio wa imani, atheists, scientists, wanasiasa, wanamichezo, wanadiplomasia, magicians, Vyama vya Siri, na wasio na hili wala lile ni UPINZANI WA WAZI KWA MAMLAKA YA MUNGU kwa ujanja na uficho wa kiwango cha juu. Ni wale tu ambao wataona haja ya Kujificha katika Vyumba vya sala peke yao binafsi Kumuomba Mungu, na Kusoma Neno la Mungu Kwa Bidii kubwa kama mchimbaji madini anavyosaka dhahabu ndio watakao kuwa Salama na Upotofu mkubwa ambao unaimomonyoa dunia kwa spidi kubwa. Ndio Pekee watakao kuwa watu wenye amani na furaha ya kweli hata kama hali ya nje ibadilike kutoka kuwa mbaya kwenda kuwa mbaya zaidi au nzuri kwenda kiwa nzuri zaidi.
Mzee hapa unazungumzia new age movements au Kuna kingine?ni Kama nimekuelewa hapa manake siku hizi no mambo ya vibe, universe, meditation, go vegan,aura na kuendelea au tumeelewana vibaya
 
Navipataje hasa hicho Cha enroute to global occupation manake kundalini yoga nahisi ninacho..
https://ia600609.us.archive.org/12/items/EnRouteToGlobalOccupation/EnRouteToGlobal.pdf
naona naatach kinagoma. download hapo.
New age movements ch 4 na ile ya NWO, muandishi Gary kagusia zaidi modenisation of ancient rituals. muhutasari wa maelezo yake kwa chati. Japo naamini Bibilia, nadharia za waandishi kama hawa huwa zinaongeza exposure japo sio vyema kuzinywa kama ni msaafu.
1545948716593.png
 
Mwaka mzima huu nilikuwa busy kufanya mtu Ila nimevisoma viwili tu
1.Uria Simango (um homem,uma causa)
2.Nada a perder (Edir Macedo,mwasisi Wa kanisa la universal)

Natumai mwakani nitaongeza vyengine
Nalog off
 
Unatumia mda gani mkuu kufikia lengo hivi..na huwa unaspecific genre au vitabu...ungetuwekea hata title inasaidia nasi kuviweka kwe reading liat yetu..asante

Asante kwa swali lako Mkuu, tuanze na audio books hizi ni rahisi coz muda wowote napokuwa free kama lunch tym, on the bus home, nikiwa gym, nikiwa napika etc. nasikiliza kwa simu via headphones na ujue mfano kitabu Chenye maneno average 80,000 hadi 120,000 na wastani ni maneno 150 kwa dakika kwa hiyo utaona kumaliza kitabu ni kama masaa 10 hadi 13. Kwa hiyo siku 2 zinatosha kumaliza kitabu kimoja with all your kazi zako zikiendelea kama kawaida. Na kama kitabu cha kawaida ni siku moja tu. Kwa mfano Mdogo kakitabu kama art of war au who moved my chease ni 70 minutes yaani unamaliza ukienda jogging na kurudi.

Kwa upande wa ebooks na hard copy nikushauri tu kwamba badilisha the way unavyosoma kwa kufanya mambo mawili cha kwanza weka target ya muda kwamba mfano leo nasoma kwa dk 120 la Pili usisome kitabu kimoja kwa wakati mmoja. Soma vitabu vitatu vya different genre kwa wakati mmoja yaani ni kama vile unaangalia series tatu kwa wakati mmoja unacheki episode moja ya shooter ikisha usiendelee ya pili unaancha unaamia empire episode moja ikiisha unaenda 24 then unarotate. Hii itakufanya usiboreke hivyo unasoma kitabu kwa dk 40 then unaweza pembeni unasoma kingine hapo brain inaamka tena then 40 minutes unasoma kingine.nakwambia utasoma vitabu vingi kwa muda mfupi.

pia kama una kindle or iPad its very simple as una soma ukichoka unaweka computer narative inakuvusha hadi chapter uliyojipangia siku hiyo.

Well kwa upande wa genres nasoma genres zote scifi, fantasy, romance, economy etc. nasoma genre zote coz reading is to get into the author’s mind kwa hiyo as long as u get into many people’s mind the more intelligent u become. Asante

Kuhusu list I will provide later.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakuu natamani sana kuanza upya utaratibu wa kusoma vitabu maana nilianza awali nkaishia kati kama sio kushindwa kabisa ....je nifanyaje ili nijue kipi kizuri na kinanifaa kwa wakati huo ...halafu vingi vilikua vya soft copy sasa vikawa vinanichosha sana ...msaada tafadhari


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sana man.

BTW hongera sana, nimeona list yako nikasema mimi siyo kabisa msomaji, wakati kwenye kundi langu jamaa wanaona mimi ndo msoma vitabu.

Noma sana, I need to pull up my socks.
Shukran.

Kila Jambo linawezekana, Msanii Nas anasema You can be anything in the World.

Nadhani Mpangilio wa Muda Ndio jambo kubwa na la Muhimu.

Japo kunausemi wa "Epuka Hitimisho la Jumuishi" lakini Wakati mwingine tunaivunja Manaake Hamna namna, Africa Wengi tunamuda Mwingi,mbaya zaiidi tunatumia kupiga majungu,fitna na Soga.

Taratibu kidogo ukitenga muda vizuri unasoma vitabu vingi.Pamoja na changamoto za Maisha za kila mwanadamu,Naamini kila mtu anachangomoto inaweza kuwa Afya,Uchumi,Mahusiano,nk lakini simbaya kuwa na muda nakusoma vitabu walau kwa uchache.

Nilikuwa napitia taarifa moja Wakidai kwamba Wayahudi ndio wanaongoza kwa Usomaji vitabu Kwa mwaka 64 Wastani mtu Mmoja,huku wakifatiwa na Japan vitabu 40 na USA vitabu 22.

Read more Learn More Change The Globe.

Sema Mimi simpenzi sana wa kusoma Fiction au Novel naona kama vile narudia kumsoma Eric au Irine Mwafumpe ndauka(Jamani babu kaju,Kipande cha Sabuni).

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom