Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Ni mwisho wa mwaka. Kama kawaida tushirikishane vitabu tulivyosoma mwaka huu. Inasaidia kujua vitabu vizuri na kushirikishana maarifa. Mi nimesoma vitabu vifuatavyo, baadhi vilipendekezwa na members humu JF.
1. Bad Samaritans.
Kitabu hiki kinaelezea jinsi ambavyo mataifa tajiri yanavyoshauri, na kulazimisha mataifa masikini kufuata sera za kiuchumi ambazo haziwezi kuwatoa kwenye umaskini. Wanakuwa kama wanazisaidia lakini kumbe wanazididimiza zaidi, ndiyo maana kawaita wasamaria wabaya. Kitabu kizuri sana.
2. Shoe dog
Ni hadithi ya maisha ya muanzilishi wa kampuni ya Nike. Story nzuri sana, huwezi kukiweka chini ukikianza. Kuna muda unaona kabisa jamaa anaenda kufeli. Kitabu hiki ni ushahidi wa kauli "Fortune favors the bold."
3. The fortunes of Africa.
Ukitaka kujua historia ya bara la Africa kwa undani basi soma kitabu hiki. Historia ya kila nchi na kila kona ya Africa imezungumzwa humu. Mtazamo wangu juu ya Africa na watu wake umebadilika sana baada ya kusoma kitabu hiki. Kutokana na kitabu hiki nimeanza kusoma African origin of civilization cha Cheikh Anta Diop.
4. Silmarillion
Hii hadithi inazungumza habari za kabla ya The hobbit na Lord of the rings. Kinazungumza jinsi middle earth ilivyoanza. Ni kizuri kusoma kwa wapenda fantasy.
5. Prisoners of Geography.
Kitabu juu ya global geopolitics. Kitabu kizuri.
6. Mzingile
Mwaka huu nilinunua vitabu vitatu vya Kezilahabi. Hiki Ni moja ya vitabu vigumu kuwahi kukisoma, nahisi kama nimeelewa nusu. Ni kama anazungumzia juu ya dini, siasa, elimu(sayansi). Pengine jinsi sayansi itavyoua dini. Ni kitabu kizuri kama unapenda mambo tata.
7. Rosa Mistika
Riwaya nzuri, labda inahusu malezi ya watoto wakike. Japo binafsi sikubaliani na maoni ya muandishi.
8. Gamba la nyoka
Kitabu hiki kinazungumzia habari za ujamaa na uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa. Kizuri sana, pia kimetumia lugha ya kuvutia sana.
9. And then there were none.
Hadithi(mystery) nzuri ya Agatha Christie. Moja ya vitabu vilivyouza sana duniani.
Vitabu vingine ilibidi kuvisoma sababu tulikuwa tunavitafsiri na kuviedit ili kuviweka kwenye maktaba app(unaweza visoma bure humo). Hivi hapa chini.
10. Nchi ya wasioona(The country of the blind).
Humu jamaa alienda nchi ambayo watu wote ni vipofu, alichotarajia kitatokea kikawa kinyume chake.
11. Shamba la wanyama(The animal farm)
Dhihaka juu ya maisha ya kijamaa.
12. Tajiri wa Babeli(The richest man in Babylon)
Kitabu kizuri juu ya uchumi binafsi. Kuna uzi humu nilikiweka.
13. Sanaa ya vita(The art of war).
Kitabu cha kale cha kichina juu ya mbinu za vita.
14. Kiongozi(The prince)
Mbinu za uongozi na siasa. Kipo jukwaa la great thinkers
15. Lulu(The pearl)
Hadithi juu ya mtu aliyepata lulu bora kabisa na yaliyomtokea. Kuna uzi kipo
16. Hadithi ya Sungura aliyeitwa Peter(The tale of Peter rabbit).
Hadithi ya mafunzo kwa watoto juu ya utii.
17. Vazi jipya la mfalme. Jisomee mwenyewe hii hadithi fupi. Kuna uzi humu ipo
18. Kufikirika
Nafikiri kinazungumza juu ya elimu.
19. Kusadikika.----nchi iliyo kwa anga😀
20. Adili na nduguze. Adili alikuwa fala☹️☹️.
21. Maisha yangu na baada ya miaka 50. Simulizi la maisha ya Shaaban Robert. Kitabu safi sana.
22. Wasifu wa Siti binti Saad. Shaaban Robert anasimulia maisha ya mwanamuziki maarufu kutoka Zanzibar.
Na vitabu hivi vya adventures.
23. Mashimo ya mfalme Sulemani
24. Hadithi ya Allan Quartamainn
25. Kisiwa chenye hazina
Robinson Kruso na kisiwa chake.
26. Nyayo za binadamu wa kale. Historia fupi ya mwanadamu.
27. Hekaya za Abunuwasi na hadithi zingine
28. Alladin na taa ya ajabu
29. Safari saba za Sinbad
30. Alibaba na wezi arobaini.
Kwa sasa nasoma Black Genesis cha Robert Bauval.
Hiki kitabu kinaelezea mwanzo wa Egyptians civilization kabla ya mafarao. Kinaeleza kuwa chanzo cha ustaarabu wa Misri ni waafrika walioishi katika jangwa la sahara(kipindi lina maji). Anatoa ushahidi wake, hasa wa kinajimu. Kitabu kizuri.
Umesoma vitabu gani mwaka huu?
Kiranga Alisina Paula Paul My Next Thirty Years MALCOM LUMUMBA wadau wengi nimewasahau.
View attachment 20593
View attachment 20294