Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,890
Habari wakuu? Ni mwisho wa mwaka. Tutafakari usomaji wetu wa mwaka huu. Vitabu vingi nimevijua kupitia michango ya members humu.
Mi nimesoma vitabu vichache tu, sikuwa na usomaji mzuri.
1. Screw business as usual cha Richard Branson.
Anaeleza jinsi biashara zinaweza kubadilika na kuweka jamii kwanza badala ya faida kwanza. Anasema biashara zinazoweka faida mbele zitapotea. Anaeleza pia jinsi misaada inavyopaswa kubadilika na kulenga ujasiriamali unaotatua matatizo ya kijamii badala ya kuwapa tu watu vitu. Kina mifano mingi kutoka Africa. Nilienjoy kukisoma.
2. Surveillance valley: The secret military history of the internet cha Yasha Levine.
Kitabu kizuri sana. Kinaeleza jinsi internet ilivyoanza na jinsi toka mwanzo ilikuwa ni chombo cha upelelezi.
3. David and Goliath cha Malcom Gladwell. Hiki sikukimaliza. Kilikuwa kimepondwa sana kwenye reviews lakini nilienjoy mpaka nilipofikia. Anazungumza mambo yanayofanya underdogs wa-shine.
4. The country of the blind cha HG Wells.
Jamaa anaenda nchi ya vipofu watupu.
5. The pearl cha John Steinbeck.
Jamaa masikini anapata lulu kubwa sana.
6. Hichhiker guides to the galaxy. Bado nasoma hii series ya vichekesho. PAULA unamkumbuka Bowerick wowbagger the infinitely prolonged?
7. Adili na Nduguze cha Shaaban Robert. Nimeisoma tena hii hadithi.
8. Njama cha Musiba.
9. Naandika Novel ipo kama 90%. Naona kama iko poa sana.
Vipi wewe, umesoma vitabu gani mwaka 2020?