Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Ni hatari sana huyu nyoka...,huuma hata mifugo kama ngombe,mbuzi,na hata punda..,hakufuati akushambulie.,ila ukimkanyaga ndio utajua...Sifa yake nyingine.,yeye akiuma haachi meno lazima atoke na nyama..,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi enzi hizo tulikuwa hatuwaui unatafuta tu gunia yale ya zamani unampakia humo mnabeba mnaenda naye mashamba ya mbali mnamtelekeza huko huko hana noma kabisa
 
unapona lakini lazima kuna mawili either utembee kama kilema, au mguu unaweza ukavimba au mkono usirudi katika hali yake ya kawaida, au ukatwe kabisa, manake sumu yake ni kama ina kansa huyu kifutu, na ukimuona tembea yake kama kinyonga hana haraka
Ni kweli kuna rafiki yangu aling'atwa tangu 2009 mpaka leo kidonda hakiponi,na huo mguu umepooza kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Black mamba ni nyoka asiyependa bughudha na usumbufu akikuona unamfuata kama alikuwa ametulia utamuona anaanza kuondoka ,

Hakuna nyoka duniani anayekimbiza ,nyoka wote wanamuogopa binaadamu kuliko binaadamu anavyomuogopa nyoka
Mmmh! Mkuu vp kuhusu chatu ambao wanakula kiumbe chochote.Usipotoshe umma aisee.Black mamba sina uhakika nae ila chatu hakuachi aisee hasa ukikutana naye sehemu tulivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijawahi muona nashukuru kwa elimu niliyopata kwenu
 
Kifutu ni hatari sana anaitwa puff adder sijui Kama spelling nimepatia . Akikuuma unaanza kuoza alipouma Kama ni kidole cha mguu kuoza kunaanzia pale kufuata mguu. Kiingereza ana damage tissue" wengi husema dawa ni kukata kiungo kilicho gongwa . Namwogopa kuliko nyoka wote yeye na koboko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu nyoka mpole sana wanapatikana sana maeneo ya baridi , siku moja nikiwa mafinga jkt nilitoroka mkesha nikaenda kulala porini nilikuwa na blanket nikiwa nmelala kumbe likaja likifutu na kuingia kwenye blanket asubuhi nashtuka linanitekenya...
Wala halikunidhuru
Kuwa serious Mkuu
 
Mimi na nyoka ni vitu viwili tofauti, awe mpole au mkali ila mimi NYOKA yoyote yule NINAUA.
 
na mm nasubiri jibu la swali hili maana ishawahi kunitokea huyu kifutu mida ya usiku alipita mbele yetu nikiwa na ba mdogo wangu tukafanikiwa kumuua tulipopiga hatua tena kadhaa tukakutana na mwingine anakatisha barabara tukamuua. kesho yake tukapokea taarifa mbaya ya msiba ndugu wawili wa familia moja kaka na dada wamefariki na walipishana masaa machache katika vifo vyao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Imani yako ipoje? Ushawahi kuomba Mungu juu ya kuua wachawi? Au ushawahi kwenda kwa waganga kufanyiwa matambiko ya kujikinga? Unaweza usiwe wewe ika huyo uliyeongozana nae.
 
hamna kitu naogopa kama nyoka,,kuna dawa za kupuliza home nyoka wasiwepo kabisa?
Kuna maua yake ukipanda huwa hafiki maeneo hayo. Ningekushauri umwage Petroli au Mafuta ya taa ila ndo hivyo ni gharama kisha sio dawa nzuri kuliko hayo maua.
 
Huyu yupo kwenye kundi la majoka yanayoitwa viper.
Zile njino mbili za juu zinaitwa fangs. Akikuchimba na yale meno huwa anasukuma na sumu hapohapo sumu hiyo huwa inaattack nerve system na kusababisha immobilization kwa victim.
Kutapika, uwezo wa kuona kupungua, na kushindwa kupumua ni miongoni mwa athari za kung'atwa na nyoka huyu.Ni miongoni mwa deadly creatures na pia ni miongoni mwa nyoka wenye sumu Kali sana.
Kuna kesi za watu waliogongwa na nyoka huyu kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu, wengine sehemu walizong'atwa zilioza.
Ni nyoka asiye mkorofi ila ukipita karibu yake anaweza kukung'ata
Huwa yuko faster kurusha kichwa ili akufikie kukung'ata hivo usimkaribie Sana pia ukimkanyaga lazima akutusue
 
Back
Top Bottom