Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Huyo nyoka ni noma akikung'ata usipotibiwa vizuri pale ulipong'atwa huwa panaoza kabisa.

-Ndumilakuwili-
hii nimewahi kusikia. Huyo nyoka kuna siku mbwa wangu alibweka sana usiku nilipotoka nikakuta ameingia getini kulikuwa na nafasi pembeni ilibidi niamshe wajirani tukamuua kwa kumrushia matofali baadae tukammwagia mafuta ya taa na kumpiga kiberiti alikuwa mkubwa sana kama kilo tatu hivi na alikuwa anafuata sauti ya vitoto vya mbwa vilikuwa vimezaliwa few days past
 
kweli huyu nyoka mpaka umkanyage, niliwahi kuchunga ng'ombe utotoni nikabanwa na haja kubwa porini, nilipomaliza kukata gogo natafuta jani nichambe, kumbe pale karibu kabisa na niliposhusha gogo alikuwa katulia ananichora tu, ilibidi niondoke taratibu, nikaenda chambia sehemu nyingine, kumsimulia babu akasema huyo sio swila, huyo mpaka umkanyage, ndio akung'ate, na vile vile inasadikika katika kabila langu ukiwakuta kwenye shamba lako la mihogo basi mihogo itanenepa kama lenyewe na inakuwa hivyo, hizo ni imani tu za wahenga
hahahah, nimecheka sana. mimi ngeenda kuchambia home kabisa😀😀
 
Inaonekana bado hujakutana na mziki wa Black mamba. Utabadilisha mtazamo wako tu kwa hiari au kwa lazima.

"A voice of one calling in the wildernes"
Black mamba ni nyoka asiyependa bughudha na usumbufu akikuona unamfuata kama alikuwa ametulia utamuona anaanza kuondoka ,

Hakuna nyoka duniani anayekimbiza ,nyoka wote wanamuogopa binaadamu kuliko binaadamu anavyomuogopa nyoka
 
hahahah, nimecheka sana. mimi ngeenda kuchambia home kabisa😀😀
mkuu ukiwa unachunga mifugo porini kuonana na nyoka mnapishana kama swila, kifutu, chatu ni vitu vya kawaida na ikitokea chatu kakamata mbuzi inabidi upambane nae ile mbaya, kuna kitu nakumbuka chatu alikosea step akaenda mdaka ng'ombe sasa ng'ombe nahisi alimuona, chatu kufyatuka na ng'ombe karuka hivyo chatu akaambulia kudaka miguu, ili amuangushe si ng'ombe akakojoa, ule mkojo kumdondokea chatu, aisee alifyatuka kama radi, nikahisi mkojo wa ng'ombe inawezekana ni sumu kwa joka lile, nilitafuta sehemu nyingine yenye jani nikachamba, ukiwa mwoga porini huwezi kwenda, yani inafikia kipindi unaona kawaida tu, kuna nyoka wengine nao sijawahi kuwaona mpaka leo lakini kule wapo, sijui siku hizi manake naona mapori mengi watu wamelima na yashakuwa makazi ya watu,
 
Huyu nyoka mpole sana wanapatikana sana maeneo ya baridi , siku moja nikiwa mafinga jkt nilitoroka mkesha nikaenda kulala porini nilikuwa na blanket nikiwa nmelala kumbe likaja likifutu na kuingia kwenye blanket asubuhi nashtuka linanitekenya...
Wala halikunidhuru
Me ningezimia mike na ningeacha kudoji aisee..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimuona pasua nlikua ndani ya gar la kuni ye anavuka zake barabara, yan had niliweweseka. kule wanamuita moma mlinz wa mashamba ya mpunga
 
Kiswahili labda kina uchache wa maneno. Kuna aina mbili kubwa za VIFUTU ambazo kwa kimombo ni Puff adder na mwingine ni gaboon viper (kubwa lao). Nahisi hiyo picha ni ya gaboon viper!
 
Kila mchangiaji hapa amekumbana kwa namna moja au nyingine na nyoka huyu hatari porini au shambani ..NI RISK SANA KUISHI AFRIKA!!
Actually africa hakuna nyoka nkuu..! Nyoka wapo asia..! Especially the indian subcontinent..! Kule ndo kunaongoza kwa kuwa na nyoka wengi na wakali zaidi..! Wanasema watafiti kuwa mtu mmoja hufa kila baada ya dakika sita kutokana na kung'atwa na nyoka...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unapona lakini lazima kuna mawili either utembee kama kilema, au mguu unaweza ukavimba au mkono usirudi katika hali yake ya kawaida, au ukatwe kabisa, manake sumu yake ni kama ina kansa huyu kifutu, na ukimuona tembea yake kama kinyonga hana haraka
Huyu nyoka ni kweli ana sumu kali sana lakini ina aina mbili tofauti

Ana sumu ile ya kuua.
Kuna dawa yake ambayo ndani ya Dakika 30 utakuwa umemaliza sumu yote mwilini na utakuwa salama kabisa.

Sumu ya kuozesha.
Sumu hii huozesha sehemu aliyo kung'ata ila yenyewe haiui, pindi akikung'ata unaweza pata dawa usife lakini pale alipokuuma pataoza na kama ukipelekwa hospital unaweza kukatwa mguu ama mkono (inategemea amekuuma wapi)

Kuna dawa yake ambayo inauwezo wa kuondoa sumu hiyo ndani ya wiki moja bila kupata kilema chochote.
 
kwa mie niliyekulia kijijini nimeona watu waliokuwa waking'atwa na huyu kifutu walikuwa wanapona lakini kiungo kinakuwa hakipo ok,
 
mkuu ukiwa unachunga mifugo porini kuonana na nyoka mnapishana kama swila, kifutu, chatu ni vitu vya kawaida na ikitokea chatu kakamata mbuzi inabidi upambane nae ile mbaya, kuna kitu nakumbuka chatu alikosea step akaenda mdaka ng'ombe sasa ng'ombe nahisi alimuona, chatu kufyatuka na ng'ombe karuka hivyo chatu akaambulia kudaka miguu, ili amuangushe si ng'ombe akakojoa, ule mkojo kumdondokea chatu, aisee alifyatuka kama radi, nikahisi mkojo wa ng'ombe inawezekana ni sumu kwa joka lile, nilitafuta sehemu nyingine yenye jani nikachamba, ukiwa mwoga porini huwezi kwenda, yani inafikia kipindi unaona kawaida tu, kuna nyoka wengine nao sijawahi kuwaona mpaka leo lakini kule wapo, sijui siku hizi manake naona mapori mengi watu wamelima na yashakuwa makazi ya watu,
Hahahah mkui we unatoka mkoa UPI!

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Huyu nyoka akikung'ata mtu huwa anakunywa maji kama kichaa.
Bado sehemu uliying'atwa uharibika vibaya kwa kuvimba zaidi.
 
Back
Top Bottom