Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

kweli huyu nyoka mpaka umkanyage, niliwahi kuchunga ng'ombe utotoni nikabanwa na haja kubwa porini, nilipomaliza kukata gogo natafuta jani nichambe, kumbe pale karibu kabisa na niliposhusha gogo alikuwa katulia ananichora tu, ilibidi niondoke taratibu, nikaenda chambia sehemu nyingine, kumsimulia babu akasema huyo sio swila, huyo mpaka umkanyage, ndio akung'ate, na vile vile inasadikika katika kabila langu ukiwakuta kwenye shamba lako la mihogo basi mihogo itanenepa kama lenyewe na inakuwa hivyo, hizo ni imani tu za wahenga
oya acha tufanye kazi kwanza.. Sio kwa kunichekesha huku...
 
Asante sana kwa kutuelewesha ila hiyo ya kucheka khaa
 
Kwanza huyu nyoka ni mpole.

Kinachomfanya aue sana na harak ni sumu yake kuwa nyepesi sio nZito so inasafiri kwa urahisi sana

Kingine huyu jamaa ni mlain sana, nimewah wapiga na jembe unawakat vizuri, wana body laini
 
Onto kwa taarifa yako kumuona kifutu tangu kichwa hadi mkia anakatiza njia yako kama unaenda mwenye biashara au Kazi ya kukupa kipato ni mkosi babu kubwa kuna lolote litatokea hadi kufilisika si nyoka mzuri
Na kama mko watu wawili mmesimama, halafu akapita katikati yenu, maana yake ni nini?
 
Na kama mko watu wawili mmesimama, halafu akapita katikati yenu, maana yake ni nini?
na mm nasubiri jibu la swali hili maana ishawahi kunitokea huyu kifutu mida ya usiku alipita mbele yetu nikiwa na ba mdogo wangu tukafanikiwa kumuua tulipopiga hatua tena kadhaa tukakutana na mwingine anakatisha barabara tukamuua. kesho yake tukapokea taarifa mbaya ya msiba ndugu wawili wa familia moja kaka na dada wamefariki na walipishana masaa machache katika vifo vyao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom