Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

na mm nasubiri jibu la swali hili maana ishawahi kunitokea huyu kifutu mida ya usiku alipita mbele yetu nikiwa na ba mdogo wangu tukafanikiwa kumuua tulipopiga hatua tena kadhaa tukakutana na mwingine anakatisha barabara tukamuua. kesho yake tukapokea taarifa mbaya ya msiba ndugu wawili wa familia moja kaka na dada wamefariki na walipishana masaa machache katika vifo vyao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuu kumbe huwa wanatoa ishara mbaya
 
Ndugu kifutu anaweza kukudhuru kwa njia mbili:
1. Meno,hapa anakugonga kwa meno yake yaliyopo mdomon na akukugonga kwa njia hii ni rahisi kupona na matibabu yake ni mengi tu. Na mara nyingi huwa anajilinda kwa kukuuma kwa meno
2. Mwiba: nimeambiwa ana mwiba mkiani na una sumu kali sana akikuchoma nao,huwa hatumii sana njia hii kupambana na binadam lkn akiamua kukuchoma na mwiba huu ni majaariwa sana kupona na hata usipo-RIP basi utapata ulemavu wa kudum

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmh! Waliowahi kumuona akiwa hai au amekufa/ameuawa waseme. Hiyo ya kuambiwa haina mashiko. Hata ile picha yake katika uzi huu haioneshi huo mwiba. Hebu miss chagga utuambie kama yule wa Kawawa alikuwa na mwiba? Mimi ninamjua fika hana mwiba wowote, ila meno yake ya kung'atia(Fangs) ni marefu ukilinganisha na nyoka wengine wanaouma.
 
kweli huyu nyoka mpaka umkanyage, niliwahi kuchunga ng'ombe utotoni nikabanwa na haja kubwa porini, nilipomaliza kukata gogo natafuta jani nichambe, kumbe pale karibu kabisa na niliposhusha gogo alikuwa katulia ananichora tu, ilibidi niondoke taratibu, nikaenda chambia sehemu nyingine, kumsimulia babu akasema huyo sio swila, huyo mpaka umkanyage, ndio akung'ate, na vile vile inasadikika katika kabila langu ukiwakuta kwenye shamba lako la mihogo basi mihogo itanenepa kama lenyewe na inakuwa hivyo, hizo ni imani tu za wahenga
Hilo kabila lenu halifai kuwepo Duniani,inabidi litoeke liende kuanzisha maisha mapya kwenye sayari nyingine huko,maana lina mila za ajabu mno!!
 
Dah...minofu yake ni mitamu sana kuliko hata ya mamba...hasa ukimla kwa dona mix 😀😀😀
 
Hilo kabila lenu halifai kuwepo Duniani,inabidi litoeke liende kuanzisha maisha mapya kwenye sayari nyingine huko,maana lina mila za ajabu mno!!
kila kabila wana mambo yao mkuu, kama umezaliwa mjini na umekulia mjini huwezi kuyajua hayo mambo kamwe
 
Huyo nyoka nakumbuka nilimkanyaga na baiskeli nikiwa speed enzi za utoto tairi ya nyuma ilipomkanyaga nikateleza nikadondoka sikumuona maana ilikua eneo la vumbi baadae nikamwona akitokomea vikachani kwa speed sana niliporudi kumueleza mjomba akanijulisha usiende tens eneo hill atarudi tena..
Kama ulimwona akiingia vichakani kwa speed sana basi huyo hakuwa kifutu. kifutu hana mbio kabisa
 
watamu sana nimewawinda mno...nawaita nyoka bwege kwa siku nilikuwa nikiwakamata hata 20..fikiria kipindi hicho kifutu mmoja alikuwa akiuzwa shilingi mia mbili nilikuwa napeleka hadi wa elfu tano kuna raia wawili walikuwa wakiwapenda sana, mmoja wa cambodia na mwingine mzulu wa south....
 
kifutu1.jpg
kifutu1.jpg
 
Attachments

  • kifutu2.jpg
    kifutu2.jpg
    58.3 KB · Views: 52
kweli huyu nyoka mpaka umkanyage, niliwahi kuchunga ng'ombe utotoni nikabanwa na haja kubwa porini, nilipomaliza kukata gogo natafuta jani nichambe, kumbe pale karibu kabisa na niliposhusha gogo alikuwa katulia ananichora tu, ilibidi niondoke taratibu, nikaenda chambia sehemu nyingine, kumsimulia babu akasema huyo sio swila, huyo mpaka umkanyage, ndio akung'ate, na vile vile inasadikika katika kabila langu ukiwakuta kwenye shamba lako la mihogo basi mihogo itanenepa kama lenyewe na inakuwa hivyo, hizo ni imani tu za wahenga

Sema tu hukuchamba siku ile... sio kesi😉🙂
 
Mleta mada, huyo nyoka kweli anaitwa Kifutu au Moma?.
Kwa uelewa wangu na miaka yote ambayo niko porini, namfahamu kama Moma.
Kifutu ni nyoka wengine wana rangi ya brown ambao nao ni wapole lakini wana sumu kali zaidi.
Yote majina yake ila watu wanaita BOMA ,siku moja nikiwa mdogo nilikuwa nimeongozona na mdogo wangu mida ya saa 2 usiku ilikuwa giza,mdogo wangu alikuwa ametangulia njia ilikuwa nyembamba ina majani ,akamkanyaga huyu nyoka ila aliwahi kuruka sasa mie nikastuka ,nikajiuliza nirudi nyuma nizunguke ,nikapata maamuzi ya kurudi nyuma kisha nikimbie na kuruka pale alipokuwa nyoka,nikarudi nyuma nikatoka spidi nikaruka ,kumbe yule nyoka alikuwa kashasogea mbele kidogo si nikamkanyaga .Alinipiga meno usiombe maumivu yake yaani utadhani msumali wa moto uuweke kwenye ngozi ila nilipewa dawa za mitishamba nikapona
 
Back
Top Bottom