Umeshawahi kukutana na mtu aliyepandisha jini/ mwenye majini? Tupe uzoefu wako

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
2,927
2,000
Kaka yangu alimwacha mke wake wa kijijini akaoa wa mjini, binti wa kizaramo. Binti anapandisha mashetani, eti anataka cheni na pete za gold. Kaka akamnunulia, baada ya wiki mbili majini yanataka tea simu enzi hizo imetoka S9 Samsung. Akampiga mateke na mabao, majini yakakoma
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,069
2,000
Nakumbuka miaka ya nyuma kulikiwa na mkuu wa mkoa mwanamke jijini Dar es Salaam. Huyu mama hakuwa mwingine ila Mary Chipungahelo au waweza mama Chips.

Huyu mama alikuwa ni mbabe haswa, asiyeyumbishwa wala kuburuzwa wala kupelekeshwa. Ameshawahi kumzingua kichizi Jenerali Ulimwengu.

Basi kipindi hicho nilikuwa naishi Kijitonyama Kisiwani, asubuhi na mapema nikatembelewa na mgeni, mdada wa haja, kapanda, ana bonge la shepu na sura nzuri.

Dada akaanza kunikumbusha kwamba tuliishi wote zamani tukiwa wadogo huko Nkajha kwa Kisugujhila.

Nikamkumbuka, akaaza kunipa kisa cha maisha yake. Akasema yeye ameolewa mitala, yeye ni mke mdogo.

Mumewe ni tajiri wa Kiarabu na alikutana naye Zanzibar ambapo alikuwa anafanya kazi ya uuguzi katika hospitali moja binafsi.

Kutokana na utajiri wa huyo Mwarabu, binti akaona abadili dini ili aweze kuolewa mke wa pili kisheria.

Bi mkubwa hakupenda, hapo ndio visa na mikasa ya kiganga ikaanza.

Dada akatumiwa majini yamuuwe, lakini dada naye alikuwa vizuri,majini hayakuwez kumuua ila kumtesa tu.

Siku hiyo alipokuja home, kuna dada mmoja alikuwepo na tulikuwa na mihadi ya kukutana na dada mwingine, Lulu Peter Muga.

Tukiwa tumekaa sebuleni, tukasukia mlango ukigongwa, ikajua Lulu anakuja, nikainuka kwenda kufungua. Lakini yule dada mke wa Mwarabu akasema usiende, hilo ni jini linautafuta. Ukienda hutoona kitu ila kuku, kimoyomoyo usinizingue. Nikaenda. Kweli sikukuta mtu ila kuku. Nikarudi ndani, nikaulizwa umeona nini? Nikajibu nimeona kuku.

Basi tukaendelea na mazungumzo huku akiendelea kutusimulia mikasa ambayo amekuwa akifanyiwa na majini.

Hodi ikapigwa tena, nami nikaenda kufungua. Akaniambia getini utawakuta wanafunzi wanataka maji, beba jug na vikombe kabisa. Nikampuuza, nilipofika getini nikakuta kuna waafunzi wanaomba maji, nikarudi ndani kwa aibu, nikachikua jug na vikombe nikaenda kuwapa watoto maji.

Hodi ikapigwa tena, akasema huyo ni mgeni wako kampokee. Kweli, alikuwa Lulu Peter Muga. Nikamkaribisha ndani.

Dada aliendelwa na story zake za kusisimua na kuogopesha sana za majini wanaoitaka roho yake.

Geti likagongwa tena, akasema huyo mtu anayekuja ni mchafu. Nikaenda kufungua, alikuwa Chips mtoto wa mkuu wa mkoa.
Chips alikuwa ametoka kuvuta bangizake, na bangi na majini havipatani.

Dada mashetani yakapanda, akavua nguo zake zote, na cheni, na Pete zake za dhahabu, akatoka mbio, alikuwa na nguvu za ajabu, hatukuweza kumdhibiti.

Baada ya wiki mbili, nikiwa naangalia taarifa ya habari, nikasikia geti likigongwa. Nilipoenda kufungua, alikuwa yule binti amekuja, ameng'aa yuko na mama yake, wenge hana tena.

Mama yake akaeleza kuwa walienda kwenye maombi, sasa binti yuko safi.

Nikawapa nguo zao, pochi, simu, fedha na mikufu na Pete zake za dhababu.

Tukala, wakaondoka.
Kama unawasiliano nae mwambie anirushie majini yake PM

Harafu chief ile story yako ya baba mkwe iliishia wapi?
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
9,838
2,000
Nimeshuhudia sana matukio ya watu wakipandisha majini ila kuna tukio ambalo sitolisahau, kuna siku mida ya jioni nimekaa zangu kibarazani nyumbani kwa rafiki yangu mara ghafla kwa nyumba ya mbele na nilipokaa(kwa rafiki yangu pia) namuona binti anatoka nje na kanga moja (bila kufuli) huku akionekana ametoka kuoga. Nilipoona vile tu nikajua wazi huyu kapandisha akiwa bafuni maana nilikuwa namfahamu na najua kuwa ana hilo tatizo la kupandisha jini,sasa mtihani ukawa nafikiria naendaje kumzuia na hali ile ya kanga moja maana kumzuia kwake pale lazima tu utumie sana nguvu na lazima umkumbatie ndio utaweza kumzuia na kibaya alikuwa anaelekea sehemu yenye kiwanja ambapo kuna watu wengi maana watu walikuwa wakicheza mpira(cha ndimu). Basi ikabaki namuangalia tu nafikiria nifanyaje na sikutaka kuwaambia watu pale wanisaidie kumkamata maana hadi muda huo watu waliyokuwepo pale hawakuwa wanamzingatia hivyo hawakuwa wakijua kibachoendelea.

Basi mpaka nakuja kufanya maamuzi ya kuwaambia kwao yule binti keshafika uwanjani huko kwenye watu wengi hivyo kilichotokea ni kwamba alidharirika sana yule binti wa watu maana kadri alivyokuwa anazuiliwa zile purukushani basi ndio alikuwa anazidi kukaa uchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom