Nilipatwa na tatizo la akili mganga akasema ni jini

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Anaadika mdau

Mwaka mmoja uliopita nilipatwa na tatizo la akili na kunipelekea ndugu zangu kuanza kuhangaika sehemu mbalimbali kutafuta Tiba kabla ya kufika hospital.

Tatizo lilianza ghafla Baada ya kupata habari ya mshtuko kuhusiana na kazi yangu, muda mwingi niliishi kwa hofu, nilikuwa naona kama tupo wawili kwenye kichwa changu,nilikuwa nasikia sauti za ajabu, ajabu yaani watu wanaongea nawasikia Mimi Ila waliopo pembeni hawasikii wala hawawaoni basi Bana kila ndugu aliongea lake maana wengi wao walikuwa wanasema nimetupiwa jini kazini dah basi bana, baada ya siku kadhaa ikabidi tutafute mganga huku na kule mganga akapatikana nikapelekwa kufika Kwa mganga kaniangalia na kupiga ramli zake akawajibu ndugu zangu kuwa nimepigwa jini tena jini hatari aidha nife au niwe chizi

Ndugu zangu wakaingiwa na hofu sana hawajui nini cha kufanya. Mganga akasema Kwa Leo nitampa dawa za kulipoza Hilo jini Wakati Mie naenda shamba kutafuta dawa mbalimbali za mitishamba ili Siku ya tatu nirudi amtoe jini. Haya Bana nikapewa madawa mbalimbali ya miti shamba ya kupaka na kunywa mengine yalikuwa na harufu Kali za kutia kinyaa.

Siku ikakucha mganga akapigiwa simu akasema amekosa usafiri wa kurudi mjini Kwa hyo kesho kutwa ndio twende Dau la kazi yote ni laki 3, mmmh sio mchezo basi Bwana nilikuwa na kahela benki ikabidi nikitoe siku moja kabla nikijiandaa siku ya pili twende Kwa mganga.

Naam siku ikafika mganga akasema tuonane usiku ndio mda mzuri wa kufanya hiyo kazi haya Bana nikawa nipo tu nyumbani nasubiria muda mara puuh kuna mgeni anaingia kucheck ni shemeji yangu kaja kuniona tukasalimiana hapa na pale akaniuliza kuhusu ugonjwa na nini kinachonisibu nikaanza kumfungukia mwanzo mwisho mpka suala la maganga kuniambia nimetupiwa jini, nikaona shemeji yangu anatabasam nikamuuliza vipi kaniambia tatizo lako sio jini hilo ni tatizo la akili kuna mtu lishawahi kumkuta mwanawe alikuwa boarding school naye alipelekwa Sana kwenye maombi lakini wapi hakupona mpaka walipoenda hospital na kukutana na daktari bingwa wa MAGONJWA ya akili. Mie mmmh basi inaweza kuwa kweli.

Shemeji akaniambia subiri nimpigie atupatie namba za daktari ili kesho ikiwezekana ukamuone kweli Bana akampigia Yule mama akatupatia namba za daktari.

Tukampigie na ndugu zangu wengine wakiwepo pale pale nikamuaelezea daktari the way navyojisikia akaniambia nakutumia jina la dawa za usingizi Kwanza then kesho njoo hospital tuonane.

Kweli nikatumiwa message ya dawa za usingizi maana nilikuwa sijapata usingizi kama siku 4 hivi kitu ambacho sio kawaida,nikaenda Duka la madawa nikanunua nikameza kweli usiku wake nilala vizuri tu.

Dah kuamka asubuhi nikakuta missed calls kibao za mganga na jamaa za jamaa yangu aliyenuunganisha Kwa mganga.wala sikujibu nikajiandaa na kuelekea hospital,nikaamsha usafiri mpka hospital nikaona na daktari akanihoji tatizo limeanzaje na lina muda gani nikamuaelezea kiundani kabisa akaniuliza na history ya MAGONJWA kwenye familia yetu nikamuaelezea akasema hilo tatizo lako ni dogo Sana tena ni la ubongo ambalo linapelekea kutokea Kwa repeatitive signals za ubongo inform of thoughts ndio maana unahisi kama mpo watu wawili kwenye kichwa kimoja mainly hili tatizo linaitwa psychosis ni MAGONJWA ya kurithi kwenye genes za wazazi.

Dah daktari alinisanua kinaga ubaga nikahisi kama naota Kumbe ndio Hali halisi niliyokuwa napitia mwisho akaniandikia dozi ya dawa kama tatu au nne akaniambia hizi dawa hazipatikani maduka haya ya mtaani hata zikipatikana bei ni ghali Kwa Hyo niende kwenye maduka ya mjini nitazipata Kwa uhakika na Kwa bei rahisi.

Kweli nikanunua dawa na kunza kumeza Kwa kipindi cha almost a year mpka nilipokaa sawa na kujiona niko fiti kabisa.

Funzo; MAGONJWA ya akili yapo na Tiba zipo Ila sio Kwa waganga.
 
Ukishasikia magonjwa ya kurithi...

Familia Zina magonjwa ya kurithi mengi kichaa ikiwa ni mmojawapo...

Hapo itakuwa muendelezo kizazi mpaka kizazi yaani haishi...

NB: Familia za kitanzania na Uchawi

Inachotakiwa ni kuvunja agano la Uchawi kwa kujenga madhabahu sahihi ili kuvunja madhabahu ya kichawi...
 
Tunashukuru kwa huu MKASA, juu ya Afya ya AKILI, ila nadhani tatizo hili ni kubwa( maana sina takwimu rasmi) na litazidi kadili siku ziendavyo, na nadhani sababu kuu zitakuwa ni÷

1.Matumizi makubwa ya POMBE
2.Matumizi ya Bange na madawa yote ya kulevya
3.Ugumu wa maisha
4.Migongano ya kifamilia hasa talaka
5.Kuiga mfumo wa maisha wa nchi za magharibi ambao unachochea upweke

Hivyo nitoe RAI kwa Serikali na Taasisi zisizo za kiserikali(NGOs) kutoa ELIMU kubwa kwa jamii juu ya TATIZO hili,.ziige mbinu za MEWATA ya Dr Njelekela na Kansa ya Matiti
 
Anaadika mdau

Mwaka mmoja uliopita nilipatwa na tatizo la akili na kunipelekea ndugu zangu kuanza kuhangaika sehemu mbalimbali kutafuta Tiba kabla ya kufika hospital.

Tatizo lilianza ghafla Baada ya kupata habari ya mshtuko kuhusiana na kazi yangu, muda mwingi niliishi kwa hofu, nilikuwa naona kama tupo wawili kwenye kichwa changu,nilikuwa nasikia sauti za ajabu, ajabu yaani watu wanaongea nawasikia Mimi Ila waliopo pembeni hawasikii wala hawawaoni basi Bana kila ndugu aliongea lake maana wengi wao walikuwa wanasema nimetupiwa jini kazini dah Basi Bana Baada ya siku kadhaa ikabidi tutafute mganga huku na kule mganga akapatikana nikapelekwa kufika Kwa mganga kaniangalia na kupiga ramli zake akawajibu ndugu zangu kuwa nimepigwa jini tena jini hatari aidha nife au niwe chizi

Ndugu zangu wakaingiwa na hofu Sana hawajui nini cha kufanya. Mganga akasema Kwa Leo nitampa dawa za kulipoza Hilo jini Wakati Mie naenda shamba kutafuta dawa mbalimbali za mitishamba ili Siku ya tatu nirudi amtoe jini. Haya Bana nikapewa madawa mbalimbali ya miti shamba ya kupaka na kunywa mengine yalikuwa na harufu Kali za kutia kinyaa.

Siku ikakucha mganga akapigiwa simu akasema amekosa usafiri wa kurudi mjini Kwa hyo kesho kutwa ndio twende Dau la kazi yote ni laki 3, mmmh sio mchezo basi Bwana nilikuwa na kahela benki ikabidi nikitoe siku moja kabla nikijiandaa siku ya pili twende Kwa mganga.

Naam siku ikafika mganga akasema tuonane usiku ndio mda mzuri wa kufanya hiyo kazi haya Bana nikawa nipo Tu nyumbani nasubiria muda mara puuh kuna mgeni anaingia kucheck ni shemeji yangu kaja kuniona tukasalimiana hapa na pale akaniuliza kuhusu ugonjwa na nini kinachonisibu nikaanza kumfungukia mwanzo mwisho mpka suala la maganga kuniambia nimetupiwa jini,nikaona shemeji yangu anatabasam nikamuuliza vipi kaniambia tatizo lako sio jini Hilo ni tatizo la akili kuna mtu lishawahi kumkuta mwanawe alikuwa boarding school naye alipelekwa Sana kwenye maombi lakini wapi hakupona mpaka walipoenda hospital na kukutana na daktari bingwa wa MAGONJWA ya akili.mie mmmh basi inaweza kuwa kweli

Shemeji akaniambia subiri nimpigie atupatie namba za daktari ili kesho ikiwezekana ukamuone kweli Bana akampigia Yule mama akatupatia namba za daktari.

Tukampigie na ndugu zangu wengine wakiwepo pale pale nikamuaelezea daktari the way navyojisikia akaniambia nakutumia jina la dawa za usingizi Kwanza then kesho njoo hospital tuonane.

Kweli nikatumiwa message ya dawa za usingizi maana nilikuwa sijapata usingizi kama siku 4 hivi kitu ambacho sio kawaida,nikaenda Duka la madawa nikanunua nikameza kweli usiku wake nilala vizuri tu.

Dah kuamka asubuhi nikakuta missed calls kibao za mganga na jamaa za jamaa yangu aliyenuunganisha Kwa mganga.wala sikujibu nikajiandaa na kuelekea hospital,nikaamsha usafiri mpka hospital nikaona na daktari akanihoji tatizo limeanzaje na Lina muda gani nikamuaelezea kiundani kabisa akaniuliza na history ya MAGONJWA kwenye familia yetu nikamuaelezea akasema Hilo tatizo lako ni dogo Sana tena ni la ubongo ambalo linapelekea kutokea Kwa repeatitive signals za ubongo inform of thoughts ndio maana unahisi kama mpo watu wawili kwenye kichwa kimoja mainly hili tatizo linaitwa psychosis ni MAGONJWA ya kurithi kwenye genes za wazazi.

Dah daktari alinisanua kinaga ubaga nikahisi kama naota Kumbe ndio Hali halisi niliyokuwa napitia mwisho akaniandikia dozi ya dawa kama tatu au nne akaniambia hizi dawa hazipatikani maduka haya ya mtaani hata zikipatikana bei ni ghali Kwa Hyo niende kwenye maduka ya mjini nitazipata Kwa uhakika na Kwa bei rahisi.

Kweli nikanunua dawa na kunza kumeza Kwa kipindi cha almost a year mpka nilipokaa sawa na kujiona Niko fiti kabisa

Funzo; MAGONJWA ya akili yapo na Tiba zipo Ila sio Kwa waganga
Matatizo mengi ya akili (>90%) hasa ya vichaa ni ya kiroho/uchawi. Wewe tatizo lako lilikuwa la kisaikolojia, stress, hofu na upweke.
 
Hakuna Kiroho wala Uchawi matatizo mengi Ya akili yanatibika Phyical(Hospitali) na Ipo kipindi kizazi kijacho watatushangaa tuliwezaje kuamini matatizo ya akili ni ya kichawi.
Kama unavyoona leo tunavyomshangaa mtu ambae anaamini Malaria ni tatizo la kichawi.
 
Kichaa huwa akiponi,
Anaadika mdau

Mwaka mmoja uliopita nilipatwa na tatizo la akili na kunipelekea ndugu zangu kuanza kuhangaika sehemu mbalimbali kutafuta Tiba kabla ya kufika hospital.

Tatizo lilianza ghafla Baada ya kupata habari ya mshtuko kuhusiana na kazi yangu, muda mwingi niliishi kwa hofu, nilikuwa naona kama tupo wawili kwenye kichwa changu,nilikuwa nasikia sauti za ajabu, ajabu yaani watu wanaongea nawasikia Mimi Ila waliopo pembeni hawasikii wala hawawaoni basi Bana kila ndugu aliongea lake maana wengi wao walikuwa wanasema nimetupiwa jini kazini dah basi bana, baada ya siku kadhaa ikabidi tutafute mganga huku na kule mganga akapatikana nikapelekwa kufika Kwa mganga kaniangalia na kupiga ramli zake akawajibu ndugu zangu kuwa nimepigwa jini tena jini hatari aidha nife au niwe chizi

Ndugu zangu wakaingiwa na hofu sana hawajui nini cha kufanya. Mganga akasema Kwa Leo nitampa dawa za kulipoza Hilo jini Wakati Mie naenda shamba kutafuta dawa mbalimbali za mitishamba ili Siku ya tatu nirudi amtoe jini. Haya Bana nikapewa madawa mbalimbali ya miti shamba ya kupaka na kunywa mengine yalikuwa na harufu Kali za kutia kinyaa.

Siku ikakucha mganga akapigiwa simu akasema amekosa usafiri wa kurudi mjini Kwa hyo kesho kutwa ndio twende Dau la kazi yote ni laki 3, mmmh sio mchezo basi Bwana nilikuwa na kahela benki ikabidi nikitoe siku moja kabla nikijiandaa siku ya pili twende Kwa mganga.

Naam siku ikafika mganga akasema tuonane usiku ndio mda mzuri wa kufanya hiyo kazi haya Bana nikawa nipo tu nyumbani nasubiria muda mara puuh kuna mgeni anaingia kucheck ni shemeji yangu kaja kuniona tukasalimiana hapa na pale akaniuliza kuhusu ugonjwa na nini kinachonisibu nikaanza kumfungukia mwanzo mwisho mpka suala la maganga kuniambia nimetupiwa jini, nikaona shemeji yangu anatabasam nikamuuliza vipi kaniambia tatizo lako sio jini hilo ni tatizo la akili kuna mtu lishawahi kumkuta mwanawe alikuwa boarding school naye alipelekwa Sana kwenye maombi lakini wapi hakupona mpaka walipoenda hospital na kukutana na daktari bingwa wa MAGONJWA ya akili. Mie mmmh basi inaweza kuwa kweli.

Shemeji akaniambia subiri nimpigie atupatie namba za daktari ili kesho ikiwezekana ukamuone kweli Bana akampigia Yule mama akatupatia namba za daktari.

Tukampigie na ndugu zangu wengine wakiwepo pale pale nikamuaelezea daktari the way navyojisikia akaniambia nakutumia jina la dawa za usingizi Kwanza then kesho njoo hospital tuonane.

Kweli nikatumiwa message ya dawa za usingizi maana nilikuwa sijapata usingizi kama siku 4 hivi kitu ambacho sio kawaida,nikaenda Duka la madawa nikanunua nikameza kweli usiku wake nilala vizuri tu.

Dah kuamka asubuhi nikakuta missed calls kibao za mganga na jamaa za jamaa yangu aliyenuunganisha Kwa mganga.wala sikujibu nikajiandaa na kuelekea hospital,nikaamsha usafiri mpka hospital nikaona na daktari akanihoji tatizo limeanzaje na lina muda gani nikamuaelezea kiundani kabisa akaniuliza na history ya MAGONJWA kwenye familia yetu nikamuaelezea akasema hilo tatizo lako ni dogo Sana tena ni la ubongo ambalo linapelekea kutokea Kwa repeatitive signals za ubongo inform of thoughts ndio maana unahisi kama mpo watu wawili kwenye kichwa kimoja mainly hili tatizo linaitwa psychosis ni MAGONJWA ya kurithi kwenye genes za wazazi.

Dah daktari alinisanua kinaga ubaga nikahisi kama naota Kumbe ndio Hali halisi niliyokuwa napitia mwisho akaniandikia dozi ya dawa kama tatu au nne akaniambia hizi dawa hazipatikani maduka haya ya mtaani hata zikipatikana bei ni ghali Kwa Hyo niende kwenye maduka ya mjini nitazipata Kwa uhakika na Kwa bei rahisi.

Kweli nikanunua dawa na kunza kumeza Kwa kipindi cha almost a year mpka nilipokaa sawa na kujiona niko fiti kabisa.

Funzo; MAGONJWA ya akili yapo na Tiba zipo Ila sio Kwa waganga.
Pole kwa changamoto na hongera kwa kupata ufumbuzi.
 
Niambie ni kipimo gani cha msongo wa mawazo nilionao nikapime ndgu
Mkuu wahi hospital

Mimi nimepitia hiyo kitu yaani jambo naweza kuwaza asubuhi mpk usiku nikilala kidogo nikiamka naamka nalo!

Nashukuru msongo wa mawazo umepungua!
 
Kwa hatuwa hii nahisi niliyonayo ni afya ya akili iliyodhofika pakubwa ,je Kwa anaejua Kwa mwanza hospital gani inatoa huduma hiyo
 
magonjwa yote yana asili ya shetani. yote!

baada ya anguko la mwanadamu pale bustanini, ndipo tabu zote hizi zikaibuka.

YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Back
Top Bottom