Kiranga hebu twende taratibu. Kwanza suala la nani anaamua nini kwenye jamii haliko kwa namna unavyotaka kuliweka na ndiyo maana kwa nchi kama Marekani mtoto aliye chini ya miaka 18 hawezi kuamua chochote bila idhini ya anayemsimamia lakini kinyume chake sivyo (Msimamizi anaweza kuamua chochote bila idhini ya mtoto/watoto anaowasimamia). Na ndiyo maana kuna mamlaka zilizowekwa na kukubalika na jamii husika kufanya maamuzi na kuna taratibu za kuamua mambo.
Inaonekana hunisomi, kama unanisoma hunielewi, kama unanielewa unaendekeza ubishi tu.
Nimeandika mara kadhaa kuhusu habari za minors, nikaongelea habari za watoto kama neno "minors" labda litawapiga chenga wengine.
Watoto habari za kujamiiana vyovyote haziwafai, hawatakiwi kuzijua nje special cases za madarasa ya baiolojia.
Kwa hiyo suala la watoto si suala la whether the issue is about gay people or not.
Watoto hawatakiwi hata kuwa exposed kuhusu habari za kujamiiana katika ya mtu mume na mtu mke.
Kwa hiyo kuhusu watoto huna argument, your point is moot.
Kuna post nimepost leo hii hii, less than 12 hours ago, nimeongelea kuto support gay parades wala straight people's public display of affection kwa sababu nina strong concerns kuhusu kuwa expose watoto kwenye mambo ya kujamiiana (haijalishi straight au gay) kabla ya muda wao.
You have no point there as far as I am concerned.
Kulingana na utaratibu uliopo, jamii husika huweza kuamua kuwa tabia fulani ni mbaya, kwa mfano hapa ni ushoga. Uamuzi huo hauwafanyi walio na tabia hizo kuwa na uwezo wa kuamulia wengine. Kwa hiyo hapa hoja tunayojadili ni ushoga, hivi wewe kwa akili zako kama mtu anapinga ushoga unadhani kuna nafasi yeyote ya yeye kukubali kuamuliwa mambo na watu wenye tabia za ushoga?
Swali la msingi hujalijibu.
Kuhusiana na watu wazima, kwa nini mtu mzima mmoja ampangie mtu mzima mwingine kuhusu nani anatakiwa kulala naye na anatakiwa kulala naye vipi?
Na kama unakubali mtu mzima mmoja kumpangia mwingine, kwa maana straight people wapige marufuku kisheria habari za gay relationships, kwa nini iwe sawa kwa upande huo tu na gays nao wasiwe na haki ya kupiga marufuku straight relationships?
Unataka kufanya "Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu"?
Swali la muhimu kabisa ni hili, je, inafaa kwa mtu mzima mmoja kumuamulia mtu mzima mwingine alale na nani na alale naye vipi?
Kama unajibu ndiyo, jibu lako haliishii kwenye gay/ straights tu.
Utajikuta umeruhusu wazungu wabaguzi waseme kwamba hawataki weusi waoe wanawake wazungu.
Au vichaa wanaotaka kuchanganya rangi za watu wote wa dunia wakataze watu weusi kuoana na watu weusi, iwe ni lazima kwa kila mtu mweusi kuoa/ kuolewa na mtu wa rangi tofauti.
Once you accept that premise, it's a slippery slope.It can take you anywhere.
Kitu kingine, suala la mtu kuitwa mtu mzima halimfanyi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika kila jambo, kwa hiyo suala la kusema ni maamuzi binafsi inategemea na maamuzi yenyewe. Ndiyo maana serikali nyingi zimeharamisha madawa ya kulevya, ingawa ni uamuzi wa mtu mwenyewe kutumia.
Unafananishaje madawa ya kulevya na gay relationship?
Wazungu wangeweza kutumia argument yako kusema hawa watu weusi hawajakomaa kufanya maamuzi sahihi, tuwabakishe wawe katika makoloni tu, tukiwapa uhuru ni sawa na kuwaachia watu wasio na akili timamu wajidunge madawa ya kulevya.
Unatumia kigezo gani kusema huyu mtu ana uwezo wa kufanya maamuzi yake na huyu hawezi inabidi jamii imfanyie maamuzi?
Moja ya argument inayotumiwa dhidi ya gays ni kwamba homosexuality is unnatural, sasa kama ni hivyo, na hawa ni watu unnatural, kwa nini hamuwaachi wakamalizike vizazi vyao huko kwa kuchukuana wenyewe kwa wenyewe bila uwezo wa kuzaliana?
Mnataka kuwalazimisha waende kuoa na kuolewa ili iweje? Ili wajaze dunia watu unnatural?
Mimi sipendi ushoga, kwa sababu haya mambo yamepelekea sasa hivi mtu anaweza kuuliza una bwana. Wewe naona ushazoea hayo maswali, ndio maana unaona poa tu.
Sio wote wanaouliza "una bwana" wanaweza kumaanisha bwana wa ushoga, mlokole anaweza kukuuliza "u na bwana" akimaanisha kwamba , je umemkubali bwana Yesu Kristo?"
Mimi binafsi siukubali ushoga, kwa sababu nawapenda sana wanawake na sioni inakuwaje mwanamme ampende mwanamme. Lakini hilo halimaanishi kwamba siwezi kumtetea anayependa ushoga kivyake vyake bila kunihusisha mimi. Namtetea awe na haki yake kama mimi nilivyo na haki yangu.
Speaking on The NAZI progroms...
Martin Niemöller is perhaps best remembered for the quotation:
First they came for the Socialists, and I did not speak out--
Because I was not a Socialist.
Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out--
Because I was not a Trade Unionist.
Then they came for the Jews, and I did not speak out--
Because I was not a Jew.
Then they came for me--and there was no one left to speak for me.
Martin Niemöller: "First they came for the Socialists..."
Wataanza na gays, who knows who will be the next target if the tradition of personal freedom is not vigorously advocated for.
I don't want to be too late when they come for the diaspora crew/ Sukuma/ atheists, and no one with guts to speak for me is left.