Umekopa mwenyewe, nikikudai unakasirika!

Mimi kwa kawaida huwa si mchoyo kabisa.

Pia ni mtu mwenye huruma sana. Kwa mfano huwa nikiona ombaomba [silipendi hili neno sema basi tu sina neno jingine lililo zuri] barabarani huwa ninapatwa na simanzi kubwa sana.

Hususan kama ombaomba huyo ni mtoto au ni watoto. Kama nina hela mfukoni huwa nawapa tu bila hata ya kujiuliza mara mbili.

Kwa hiyo mtu akinijia na shida yake aombe nimkopeshe hela mara nyingi sana huwa sikatai.

Lakini kwa vile huwa ni mkopo basi huwa ninatoa masharti yangu. Huyo mtu akiyakidhi na kama hicho kiasi ninacho basi namkopesha.

Sasa inapotokea mtu anakuja kukukopa na kukuahidi kuwa atakulipa siku fulani, yaani anakubembeleza kweli hadi anataka kulia, na wewe kwa huruma zako unamkopa kwa masharti.

Siku ya kurudisha mkopo ikifika yeye hatokei. Ukianza kumtafuta ili akulipe anaanza kukukwepa.

Ukizidisha kumtafuta anaanza kukasirika na kukuletea jeuri.

Watu wa hivi siwapendi kabisa mimi. Kwa nini unikasirikie wakati nakudai hela zangu?

Kama hutaki nikufuatilie nilipe hela zangu na mimi wala sitakutafuta hata kwa salamu tu.

Umejileta mwenyewe na vishida vyako na kuanza kujiliza halafu unaniletejea jeuri kunilipa hela zangu.

Mijitu mingine sijui ikoje tu. Kama unadai hela uliyokopa ni ndogo nisikusumbue iweje hukuwa nayo sasa?

Shenzi pambaaf kabisa. Siku ingine ukinijia na vishida vyako ntakwambia nenda baa ukategeshe.

Sina uelewa sana wa nchi nyingine lkn huwa nahisi kwa Tanzania na hasa mijini tuna tatizo kubwa sana na hii hali, na watu wanavyo changanya 'kindness with weakness' ndo balaa yaani wanaona ni haki kukopa na sio haki kulipa kwa ufupi maisha yetu hayana kabisa uadilifu kwa hili kuanzia wote wa misikitini mpaka makanisani na huwa nashangaa vitu vidogo kama uadilifu huu mdogo wa kukopa na wakati wa kulipa inakuwa usumbufu kweli kwa watu wengi

Mimi ni muhanga sana wa hii kitu na upande wangu nikichukua kitu cha mtu nina hofu kweli mpaka nimpe haki yake nakosa amani kabisa lakini wengine wala hawajali

Na kwa wengine unaona kama uadilifu huu tu watu wengi unatushinda na tunasema ni watu wa mungu sasa kwa sisi ambao tupotupo tu hata hatuendi ktk 'majengo' tunashangaa kweli mahubiri/mawaidha yanayotolewa huko je hawasisitizi uadilifu kwa watu wao kurudisha amana 'mikopo' waliyochukua
 
Mimi kwa kawaida huwa si mchoyo kabisa.

Pia ni mtu mwenye huruma sana. Kwa mfano huwa nikiona ombaomba [silipendi hili neno sema basi tu sina neno jingine lililo zuri] barabarani huwa ninapatwa na simanzi kubwa sana.

Hususan kama ombaomba huyo ni mtoto au ni watoto. Kama nina hela mfukoni huwa nawapa tu bila hata ya kujiuliza mara mbili.

Kwa hiyo mtu akinijia na shida yake aombe nimkopeshe hela mara nyingi sana huwa sikatai.

Lakini kwa vile huwa ni mkopo basi huwa ninatoa masharti yangu. Huyo mtu akiyakidhi na kama hicho kiasi ninacho basi namkopesha.

Sasa inapotokea mtu anakuja kukukopa na kukuahidi kuwa atakulipa siku fulani, yaani anakubembeleza kweli hadi anataka kulia, na wewe kwa huruma zako unamkopa kwa masharti.

Siku ya kurudisha mkopo ikifika yeye hatokei. Ukianza kumtafuta ili akulipe anaanza kukukwepa.

Ukizidisha kumtafuta anaanza kukasirika na kukuletea jeuri.

Watu wa hivi siwapendi kabisa mimi. Kwa nini unikasirikie wakati nakudai hela zangu?

Kama hutaki nikufuatilie nilipe hela zangu na mimi wala sitakutafuta hata kwa salamu tu.

Umejileta mwenyewe na vishida vyako na kuanza kujiliza halafu unaniletejea jeuri kunilipa hela zangu.

Mijitu mingine sijui ikoje tu. Kama unadai hela uliyokopa ni ndogo nisikusumbue iweje hukuwa nayo sasa?

Shenzi pambaaf kabisa. Siku ingine ukinijia na vishida vyako ntakwambia nenda baa ukategeshe.
 
Alafu hiyo ya kudharau kiasi cha pesa unachodaiwa wakati kipindi unakopa haukuwa nayo huwa inanichosha kweli, ubinadamu kazi.

Utasikia...hela yenyewe elfu mbili tu inayokufanya unisumbue...

Huku kasahau hiyo hiyo elfu mbili hakuwa nayo hadi akaamua kukopa.
 
Si ndio hapo sasa! Na kama ndi ndogo si arudishe sasa!
 
Back
Top Bottom