Umekopa mwenyewe, nikikudai unakasirika!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,175
Reaction score
143,960
Mimi kwa kawaida huwa si mchoyo kabisa.

Pia ni mtu mwenye huruma sana. Kwa mfano huwa nikiona ombaomba [silipendi hili neno sema basi tu sina neno jingine lililo zuri] barabarani huwa ninapatwa na simanzi kubwa sana.

Hususan kama ombaomba huyo ni mtoto au ni watoto. Kama nina hela mfukoni huwa nawapa tu bila hata ya kujiuliza mara mbili.

Kwa hiyo mtu akinijia na shida yake aombe nimkopeshe hela mara nyingi sana huwa sikatai.

Lakini kwa vile huwa ni mkopo basi huwa ninatoa masharti yangu. Huyo mtu akiyakidhi na kama hicho kiasi ninacho basi namkopesha.

Sasa inapotokea mtu anakuja kukukopa na kukuahidi kuwa atakulipa siku fulani, yaani anakubembeleza kweli hadi anataka kulia, na wewe kwa huruma zako unamkopa kwa masharti.

Siku ya kurudisha mkopo ikifika yeye hatokei. Ukianza kumtafuta ili akulipe anaanza kukukwepa.

Ukizidisha kumtafuta anaanza kukasirika na kukuletea jeuri.

Watu wa hivi siwapendi kabisa mimi. Kwa nini unikasirikie wakati nakudai hela zangu?

Kama hutaki nikufuatilie nilipe hela zangu na mimi wala sitakutafuta hata kwa salamu tu.

Umejileta mwenyewe na vishida vyako na kuanza kujiliza halafu unaniletejea jeuri kunilipa hela zangu.

Mijitu mingine sijui ikoje tu. Kama unadai hela uliyokopa ni ndogo nisikusumbue iweje hukuwa nayo sasa?

Shenzi pambaaf kabisa. Siku ingine ukinijia na vishida vyako ntakwambia nenda baa ukategeshe.
 
mimi ninalimit ya kudai deni kama liko ndani ya uwezo wangu wa kusaheme.
nikisamehe nalibadilisha kutoka hadhi ya mkopo hadi hadhi ya msaada.
baada ya hicho kitendo huyo mtu nampiga lifeban ya msaada wa kifedha.
sio lazima nikukopeshe mimi, dunia ina watu bilion7 kawatafute hao.
 
Wanaboa sana watu wa hivyo aisee.

Hela yako halafu ukimdai anakasirika.

What kinda fcuked sense does that make?
 
mimi ninalimit ya kudai deni kama liko ndani ya uwezo wangu wa kusaheme.
nikisamehe nalibadilisha kutoka hadhi ya mkopo hadi hadhi ya msaada.
baada ya hicho kitendo huyo mtu nampiga lifeban ya msaada wa kifedha.
sio lazima nikukopeshe mimi, dunia ina watu bilion7 kawatafute hao.
Hii naichukua kama reference asante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Pia Bor Muandikishiane Ktk Karatasi. Maana Kukopeshana Kwa Mdomo Inakuaga Ngumu KuEnforce Mahakamani Akikataa Unabakia On The Losing Side.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Mimi kwa kawaida huwa si mchoyo kabisa.

Pia ni mtu mwenye huruma sana. Kwa mfano huwa nikiona ombaomba [silipendi hili neno sema basi tu sina neno jingine lililo zuri] barabarani huwa ninapatwa na simanzi kubwa sana.

Hususan kama ombaomba huyo ni mtoto au ni watoto. Kama nina hela mfukoni huwa nawapa tu bila hata ya kujiuliza mara mbili.

Kwa hiyo mtu akinijia na shida yake aombe nimkopeshe hela mara nyingi sana huwa sikatai.

Lakini kwa vile huwa ni mkopo basi huwa ninatoa masharti yangu. Huyo mtu akiyakidhi na kama hicho kiasi ninacho basi namkopesha.

Sasa inapotokea mtu anakuja kukukopa na kukuahidi kuwa atakulipa siku fulani, yaani anakubembeleza kweli hadi anataka kulia, na wewe kwa huruma zako unamkopa kwa masharti.

Siku ya kurudisha mkopo ikifika yeye hatokei. Ukianza kumtafuta ili akulipe anaanza kukukwepa.

Ukizidisha kumtafuta anaanza kukasirika na kukuletea jeuri.

Watu wa hivi siwapendi kabisa mimi. Kwa nini unikasirikie wakati nakudai hela zangu?

Kama hutaki nikufuatilie nilipe hela zangu na mimi wala sitakutafuta hata kwa salamu tu.

Umejileta mwenyewe na vishida vyako na kuanza kujiliza halafu unaniletejea jeuri kunilipa hela zangu.

Mijitu mingine sijui ikoje tu. Kama unadai hela uliyokopa ni ndogo nisikusumbue iweje hukuwa nayo sasa?

Shenzi pambaaf kabisa. Siku ingine ukinijia na vishida vyako ntakwambia nenda baa ukategeshe.
Dah... Hii mistari ungeisajili chief...... Wajanja wataitia biti ikatoka taarabu nzuri halafu ukaanza kulialia tena umeibiwa wimbo[emoji23] [emoji23]

Sent from my beretta ARX 160 using JamiiForums Mobile App
 
mkuu Nyani Ngabu njia rahsi andikishaneni asipokulipa muitie Yono Auction Mart... kama waliweza piga mnada nyumba za lugumi hawawezi mshindwa mdaiwa wako
 
Back
Top Bottom