Umbali kutoka Dar kwenda Mwanza {km}

Umbali kutoka Dar kwenda Mwanza {km}

Hebu achaneni na mambo ya sumatra, chart, mimi niliendesha gari yangu kutoka Dar,tabata segerea mpaka Mwanza mjini Kirumba mwezi march kwa uhalisia kuna KILOMETA 1080.
Nilitoka dar saa kumi kamili alfajiri nikiendesha toyota primeo 1800cc.nikafika mwanza saa mbili usiku mwendo wa kawaida nilikuwa na familia.
ZINGATIA.
1.Hakikisha unatok dar mapema(at least 1hr before 0600am) ili usifatane na mabasi makubwa kwani ni masumbufu na yanaovertake ovyoovyo yanaweza kukuletea matatizo.
2.Barabara ya Shinyanga - Mwanza ina matuta mengi yale mabaya ya kukomoa madereva, kwa gari ndogo lazima upande kwa spidi Zero. Pana kilometa 168, lakini utatumia masaa matatu.

sent from my rollpad.

hakika wewe ndio naweza kuchukua uzoefu kwako,bro ulitumia lita ngapi mpaka kirumba
 
Dada Tiba, kuuliza ni kuuliza tu, be it Google or JF!

what a professional answer is this,mkuu watu wapumbavu wanajua kuuliza n google tu,wanataka kuweka mipaka ya vitu vya kuzungumza hapa jf,ama kweli kichwa ndio mtu.
 
We unaleta fani yako ya umbumbumbu kwenye barabara. Mimi sioni alichokosea hapo. Hivi kama yeye ni dereva wa masafa ana haja ya kutaja source?

Wewe unapenda source au uhalisia kutoka kwa wanaoitumia barabara?

Mtu anaposema umbali ni km kadhaa na wote tupo hapa Tanzania, ukiwa na akili kidogo utajua tunazungumzia allowed maximum speed ambayo ni 80km/h +/- 10 na huo ni wastani kwani kuna milima na dharura za hapa na pale.

Wewe ulitaka tu kuleta ujuzi na kujifanya wewe ndio unajua saana. Pasiansi, Igoma na Isamilo hiyo yote ni Mwanza na sidhani mtu akishafika Nyegezi au Nyakato bado atauliza namna ya kufika Mwanza na ungekuwa na akili kidogo ungejua muanzisha mada anataka msaada wa kufika Mwanza na sio Pasiansi. Na ndio maana yeye aliuliza Mwanza na hakutuuliza kijijini kwake anakokwenda

Kama bado unabisha, karibu ila ujiandae. Mimi ni mjuaji kuliko wewe na muda ninao
Afadhali umemweleza mkuu, maana watu wengine sijui wana tabia gani. Mtu kama una mawazo tofauti changia tu, huna haja ya kukejeli post za watu wengine.
 
Km ni gari yenye matumizi ya kawaida, kwa maana ya 1800 - 2000CC tenga laki 6 ya mafuta na laki 2 ya emergence km traffic law violation, breakdown, puncture, na vingine visivyotarajiwa. Mi nimekwenda muda c mrefu na gari ya 2000CC nimetumia mafuta ya laki 6, na nikarejea nyumbani kwangu Dar nikiwa na half tank! Safari njema, kuwa makini na tochi za barabarani, zingatia vibao vya alama, ukijihisi kuchoka au usingizi pumzika, hy ni safari ndefu c vita!
mkuu hiyo ni range au hammer mafuta ya laki nne unakwenda na kurudi
 
Ndugu wanajamvi kwa yeyote mwenye kufahamu umbali wa kutoka dar kwenda mwanza kwa njia ya barabara anifahamishe,maana nataka nifahamu ili niweze kutenga bajeti nzuri ya mafuta kwani sijawahi kwenda mwanza.asanten

ndugu watanzania naomba anayeju umabali toka bandari ya dar es salaam hadi singida aniambie,asanteni.
 
dar-mwanza kms 1,156 nilisafiri na toyota passo nilitoka dar saa 10.30 alfajiri na kufika mwanza saa 1.00 jioni nilitumia shs 275,000 mafuta.
 
Km ni gari yenye matumizi ya kawaida, kwa maana ya 1800 - 2000CC tenga laki 6 ya mafuta na laki 2 ya emergence km traffic law violation, breakdown, puncture, na vingine visivyotarajiwa. Mi nimekwenda muda c mrefu na gari ya 2000CC nimetumia mafuta ya laki 6, na nikarejea nyumbani kwangu Dar nikiwa na half tank! Safari njema, kuwa makini na tochi za barabarani, zingatia vibao vya alama, ukijihisi kuchoka au usingizi pumzika, hy ni safari ndefu c vita!
Duuuh!! laki 6?!! bora nipande precision au fast jet go & return haifiki hata laki 4,lisaa limoja na nusu tu nimefika, nakuwa nimesave muda wangu,sijachoka,nimeokoa lyf span ya gari langu na majanga mengine ya barabarani,na hela pia imebakia hata ya kukodi gari lingine kwa mizunguko ya hapo mwanza..ila ni mtazamo wangu tu...wengine starehe zao ni kuendesha magari huwezi jua.
 
Ndugu wanajamvi kwa yeyote mwenye kufahamu umbali wa kutoka dar kwenda mwanza kwa njia ya barabara anifahamishe,maana nataka nifahamu ili niweze kutenga bajeti nzuri ya mafuta kwani sijawahi kwenda mwanza.asanten

Ni sawa tu na umbali wa kutoka Mwanza kwenda Dar.
 
Duuuh!! laki 6?!! bora nipande precision au fast jet go & return haifiki hata laki 4,lisaa limoja na nusu tu nimefika, nakuwa nimesave muda wangu,sijachoka,nimeokoa lyf span ya gari langu na majanga mengine ya barabarani,na hela pia imebakia hata ya kukodi gari lingine kwa mizunguko ya hapo mwanza..ila ni mtazamo wangu tu...wengine starehe zao ni kuendesha magari huwezi jua.

huwezi jua labda wako watatu
 
Mkuu hata mimi ni shuhuda. Nimeendesha peke yangu bila kupumzika kutoka Dar(Segerea) hadi Bukoba(Kanyigo) Km 1542 bila kupumzika na nilitumia masaa 18.
Mkuu unataka kusema Km zote hizo hukusimama kwa ajili ya kula , kuchimba dawa? Kuongeza wese!

Kweli wewe si binadamu wa kawaida

Na nitakuwa wa mwisho kuamini maelezo yako
 
Huyu jamaa aliuliza hili swali mwana 2012,hajapata tu jibu?

Kama hajapata ni Km 1165!
 
Back
Top Bottom