Umbali kutoka Dar kwenda Mwanza {km}

Tip Master

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
490
532
Ndugu wanajamvi,

Kwa yeyote mwenye kufahamu umbali wa kutoka Dar kwenda Mwanza kwa njia ya barabara anifahamishe, maana nataka nifahamu ili niweze kutenga bajeti nzuri ya mafuta kwani sijawahi kwenda Mwanza.

Asanteni
 
Mkuu naona wadau hapo juu wamejaribu tu kuguess, ukweli ni 1154 km...hii ni kwa mujibu wa jedwali la umbali toka Dar kwenda mikoani ambalo hutolewa na SUMATRA
 
Dar to Mwanza ni km 1128 kwa gari la private utatumia masaa 14 na dk 36

Sasa we na wewe, nway mradi umechangia..
Kiburudisho (nikitaja hli jina namuwaza mwanamke) umetaja umbali bila source, mbaya zaidi umetaja na muda bila kufikiria japo kidogo kuhusu spidi ya uendeshaji unaoujua wewe na uendeshaji wa mwenye thread.. Huwezi taja umbali na muda bila kutaja spidi..

Zaidi ya hapo hakuna hata mmoja aliyesema umbali kuanzia sehemu gani kwa Dar (zero km) je Kibamba, kigamboni, Pugu, au Masaki.. Na je zero km ya mwanza ni Buswelu, Pasiansi, Igoma au Kamanga.. So tuwe smart kidogo katika kujibu hoja.. Bora aliyetaja source ya Sumatra twaweza sema wanajua zero km za miji..

Mbumbumbu Intelligent
 
Km ni gari yenye matumizi ya kawaida, kwa maana ya 1800 - 2000CC tenga laki 6 ya mafuta na laki 2 ya emergence km traffic law violation, breakdown, puncture, na vingine visivyotarajiwa. Mi nimekwenda muda c mrefu na gari ya 2000CC nimetumia mafuta ya laki 6, na nikarejea nyumbani kwangu Dar nikiwa na half tank! Safari njema, kuwa makini na tochi za barabarani, zingatia vibao vya alama, ukijihisi kuchoka au usingizi pumzika, hy ni safari ndefu c vita!
 
dar kwenda misunwi,magu au ukerewe? Sema eneo husika naona wengi wanatoa dar to Nyegezi stand
 
barabara hiyo kuanzia dodoma mpaka shinyanga inaudhi sana kwa matutu mengi.
Kila kijiji kina matuta 3 la katikati ni kubwa sana kwa hiyo utakuta unaenda Km120-150 kwa muda mfupi tu.
Na maeneo ya singida yana traffic police wengi wenye kamera.
 
Sasa we na wewe, nway mradi umechangia..
Kiburudisho (nikitaja hli jina namuwaza mwanamke) umetaja umbali bila source, mbaya zaidi umetaja na muda bila kufikiria japo kidogo kuhusu spidi ya uendeshaji unaoujua wewe na uendeshaji wa mwenye thread.. Huwezi taja umbali na muda bila kutaja spidi..

Zaidi ya hapo hakuna hata mmoja aliyesema umbali kuanzia sehemu gani kwa Dar (zero km) je Kibamba, kigamboni, Pugu, au Masaki.. Na je zero km ya mwanza ni Buswelu, Pasiansi, Igoma au Kamanga.. So tuwe smart kidogo katika kujibu hoja.. Bora aliyetaja source ya Sumatra twaweza sema wanajua zero km za miji..

Mbumbumbu Intelligent

We unaleta fani yako ya umbumbumbu kwenye barabara. Mimi sioni alichokosea hapo. Hivi kama yeye ni dereva wa masafa ana haja ya kutaja source?

Wewe unapenda source au uhalisia kutoka kwa wanaoitumia barabara?

Mtu anaposema umbali ni km kadhaa na wote tupo hapa Tanzania, ukiwa na akili kidogo utajua tunazungumzia allowed maximum speed ambayo ni 80km/h +/- 10 na huo ni wastani kwani kuna milima na dharura za hapa na pale.

Wewe ulitaka tu kuleta ujuzi na kujifanya wewe ndio unajua saana. Pasiansi, Igoma na Isamilo hiyo yote ni Mwanza na sidhani mtu akishafika Nyegezi au Nyakato bado atauliza namna ya kufika Mwanza na ungekuwa na akili kidogo ungejua muanzisha mada anataka msaada wa kufika Mwanza na sio Pasiansi. Na ndio maana yeye aliuliza Mwanza na hakutuuliza kijijini kwake anakokwenda

Kama bado unabisha, karibu ila ujiandae. Mimi ni mjuaji kuliko wewe na muda ninao
 
Dar to Mwanza ni km 1128 kwa gari la private utatumia masaa 14 na dk 36

Inabidi

1-Ataje aina ya gari anayotumia?
2-Atakuwa na familia?
3-Atakula njiani na kunywa?
4-Atachukua abiria njiani?...etc

Hapo ndio tuta estimate atachukua masaa mangapi, sie wengine Dar - Mwanza huchukua siku mbili hadi tatu kwani ni lazima kutoa stress mahali fulani kama sio Dodoma, basi Singida au Shinyanga na ukifika usemi wa kwanza ni gari imesumbua sana njiani
 
Ndugu wanajamvi kwa yeyote mwenye kufahamu umbali wa kutoka dar kwenda mwanza kwa njia ya barabara anifahamishe,maana nataka nifahamu ili niweze kutenga bajeti nzuri ya mafuta kwani sijawahi kwenda mwanza.asanten

Jamani sio lazima kila kitu uulize hapa JF. You can just google and get the distance from Mwanza to Dar Es Salaam.

Tiba
 
Back
Top Bottom