Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Sisi binadamu tofauti tofauti tuna hobies mbalimbali, wengine wanapenda kutulia sehemu moja, wengine wanapenda kusafiri safiri.

Mimi hobby yangu ni safari, na kula. yaani travelling na eating delicious meals na feasting on anything good! Yaani napenda sana kusafiri na kula vitu vizuri.

Mastori.

Nikiwa shule nilipenda kusomea sheria ili niwe mwanasheria, lakini kwa vile nilikuwa kijana ambaye damu inachemka sana, nikiwa sekondari ya Ilboru, na baridi la mlima Meru, nikajikuta sijatulia hivyo kukosa division 1, ya kuingia sheria.

Enzi zetu ukimaliza form six lazima upite jeshini JKT kwa mujibu wa sheria, na kufuatia mimi kusoma Shule za boys only, Tambaza na Ilboru, jeshini ndio sehemu yangu ya kwanza ya ujana kuchanganyika na wasichana.

Nilipangiwa JKT Makotupora Dodoma, mabweni ya kiume waliita Ngorongoro na ya kike Serengeti. Japo wengi jeshini waliona ni mateso lakini baadhi yetu ile kuangalia tuu wanyama wa Serengeti, kwetu raha!.

Kwa vile napenda kula, JKT ndiko nilikoanza kuharibikia maana misosi ni ya kumwaga!. Ilikuwa ni kata mti, panda mti, unajilia tuu!.

Kufuatia kuona raha sana jeshini, mtu ukikipenda kitu unakifanya vizuri kwa moyo wa kujituma, hivyo jeshini nikawa a very good performer kwenye somo la kulega shabaha, yaani nilikuwa sharp shooter, nikilenga, nagonga, na hit the bull!. Post za chuo kikuu zilipotoka nimekosa sheria!.

Hivyo baada ya kumaliza JKT nikapelekwa moja kwa moja kujiunga na JWTZ na kupiga deppo mpya ya JW pale Airwing Ukonga kusubiria kwenda cadet.

Jeshini JWTZ ndipo nikajigundua sijatulia kupokea kila amri, jeshi linataka nidhamu ya hali ya juu, mchana ni mafunzo na usiku ni kupumzika, kufuatia mimi kupenda kula, ikawa mchana ni mafunzo na usiku ni hakuna kulala!, ni unakimbizana na misosi ya mitaani!.
Jeshi likanishinda!.

Ndipo nikajiunga na chuo cha uandishi wa habari TSJ enzi hizo kiko Ilala Bungoni. Serengeti na Ngorongoro za TSJ ziko mkabala, hivyo kwa upande wa misosi ni kujilia tuu!. Kumaliza TSJ nikapostiwa RTD, na kujichukulia jumla ka swala fulani ka TSJ.

Kazi ya uandishi wa habari inahusisha kusafiri sana, ni trips na trips na kila nikisafiri mahali popote hupendelea sana kula the local foods za mahali hapo.

Japo baadaye, huku nikiwa ni mwandishi wa habari, nikikuja kusoma sheria, lakini kufuatia kupenda trips na kula, niliendelea na kazi ya uandishi wa habari, ila sasa naelekea 60, nimeanza kuzeeka, hivyo kupunguza kula maana meno hayawezi tena kutafuna sana nyama, labda vitu laini laini kama maini na vi spring chicken mara moja moja!.

Vyakula tofauti tofauti vina tastes tofauti tofauti, kuna vyakula kwa kuvitazama tuu kwa macho unaviona they look good to taste hivyo ukila utafaidi lakini unapokula unakuta ni tasteless, na kuna vyakula kusema ukweli ukivitazama machoni kama zile nyama za mnadani, they don't look so good au mazingira kama ya kwa Mromboo pale Arusha, mazingira ni horrible fulani but the meat is so good, so tasty!, ukila una enjoy!, hivyo don't judge the book by its cover!.

Wewe unaweza kukumbuka baadhi ya vyakula ulivyokula vya makabila, jamii, na mataifa mbalimbali? Vipi ulifaidi, ukikumbuka unajisikia raha?

Kwa upande wangu nimewahi kula vyakula vya makabila haya, jamii hizi na mataifa haya;
  • Moshi Wachagga wa Kirua Vunjo​
  • Moshi Machame​
  • Moshi Kibosho​
  • Moshi Siha​
  • Moshi Wapare​
  • Arusha Waarusha​
  • Arusha Wameru​
  • Arusha Wamasai​
  • Babati Wambulu​
  • Singida Wanyaturu​
  • Singida Wanyiramba​
  • Dodoma Wagogo​
  • Morogoro Wapogoro​
  • Morogoro Waluguru​
  • Morogoro Wakaguru​
  • Pwani Wadengereko​
  • Dar es Salaam, Wazaramo​
  • Iringa Wahehe​
  • Iriga wabena​
  • Iringa Wakinga​
  • Mbeya Wanyakyusa​
  • Songea Wangoni​
  • Songea Wanyasa​
  • Tanga Wasambaa​
  • Tanga Wadigo​
  • Tanga Wabondei​
  • Bukoba Wahaya​
  • Bukoba Wahangaza​
  • Lindi Wamachinga​
  • Mtwara Wamakonde​
  • Musoma Wajita​
  • Tarime Wakurya​
  • Ukwerewe Wakerewe​
  • Mwanza Wasukuma​
  • Tabora Wanyawezi​
  • Zanzibar Wazanzibari​
  • Pemba Wapemba​
  • Mafia Wamafya​
  • Kigoma Waha​
  • Kenya Wakikuyu​
  • Kenya Wakamba​
  • Uganda Watoro​
  • Uganda Waganda​
  • Uganda Wanyankole​
  • Rwanda Wanyarwanda​
  • Burundi Warundi​
  • Zambia Wazambia​
  • Malawi Wamalawi​
  • Msimbiji Wasumbiji​
  • Angola wa Mulato​
  • Swaziland Wazwazi​
  • Lesotho Wasotho​
  • South Africa Wazulu​
  • South Africa Wakhosa​
  • South Africa Africans​
  • Zimbabwe wa Matebele​
  • Malawi Wamaawi​
  • Congo Wakongo​
  • Ghana Waghana​
  • Liberia wa Liberia​
  • Cote d'ivoire Wakote​
  • Ethiopia Wahabeshi​
  • Sudan ya Kusini Wasudani​
  • Somalia Wasomali​
  • UK Waingereza​
  • US Waamerica​
  • Swiss Wa Swiss​
  • Italy Wataliano​
  • Sweden wa Swedish​
  • Norway wa Norwegians​
  • Finland wa Fini​
  • Germany Wajerumani​
  • Poland wa Polish,​
  • Canada wa Canadian​
  • India Wahindu​
  • Russia Warusi​
  • China Wachina​
  • Japan Wajapan.​
Ukisafiri ukifika popote ukalala hata kwa usiku mmoja, hakikisha usiishie kula vyakula vya hoteli tuu, toka nje, walk around, grab a local taxi, madereva taxi wanajua wapi you can get a local good tasty meals, kama unapenda kula kila ukisafiri hakikisha you feast the good stuff kuonja difference taste!.

Kwa vile leo tumeanza Kwaresma, baada ya Kwaresma nitarejea kwenye uzi huu niwape mastori ya kwa upande wapi vyakula vya wapi ni vitamu na nilifaidi!.

NB. Kwa vile vyakula vipo vya aina nyingi, na vinaliwa wakati tofauti tofauti, mfano cha asubuhi ambacho ni breakfast, cha mchana ambacho ni lunch, na cha usiku ambacho ni dinner, it's worldwide believed kuwa kitamu zaidi sio cha asubuhi au cha mchana bali ni cha usiku!, hivyo hapa mimi nazungumzia kile 'chakula cha usiku!'!, na ndio maana mialiko mingi ya chakula cha usiku hutanguliwa na kualikwa dinner au kutolewa out, kisha unaishia kujilia!.

Kwa leo nawatakia Kwaresma njema.

Paskali
 
Vyakula vya kichina - hivi nimekula kwa miaka mingi, jamaa wana mapishi lukuki na misosi yao ni mitamu haswa (miaka ya nyuma nishawahi weka uzi) cc Mshana Jr, kuna jamii ya Wachina wanatokea jimbo la Xinjiang kaskazini magharibi mwa Uchina, wana aina moja ya msosi unakuwa ni mchanyato wa kuku kaanga na viazi kaanga ndani ya mchuzi mzito wa viungo (Da pan ji), hatari sana hiki kisinia....

Vyakula vya kihindi/kipakistan - majina siyajui lakini miaka ya nyuma nimekula sana haswa nikiwa Hong Kong, vingi ya vyakula vyao vina mahadhi ya kipwani, viungo, michuzi michuzi yenye vikorombwezo haswa...

Vyakula vya Kiindonesia - Huko huko uchina katika kusaka misosi yenye mahadhi ya Kiafrika, nikaangukia kwenye mgahawa wa hawa mabwana, kuna kuku fulani shatashata wa mchuzi wenye nazi nzitoooo...hatari sana!

Vyakula vya kipopo (Naija) - Hawa jamaa nao wana vyakula vya michuzi mingi yenye mafuta na pilipili, lakini wana wali wao mmoja mtamu huo unaitwa 'jollof rice', hii upate iliyotiwa pilipili na pande la kuku...noma sana...
 
Nimekumbuka pia kuna wakati nimefika Nairobi kwa mara ya kwanza, wenyeji waliniambia ukiwa hapa ni bora kula ugali kuliko mchele (wali)....

Nikapelekwa chimbo kula ugali matumbo na sukuma...huo ndio ukawa mwanzo wa kupenda hii msosi maana jamaa wanaweka nyma nyingi hatari
 
Wanabodi,
Sisi binadamu tofauti tofauti tuna hobies mbalimbali, wengine wanapenda kutulia sehemu moja, wengine wanapenda kusafiri safiri, mimi napenda sana kusafiri, na napenda kula. Kila nikisafiri, mahali popote hupendelea sana kula the local foods za mahali hapo!.
Kule Ntwara kuna kitu kinaitwa Upupu duuh Mlo mtamu hatareee. Konde boy&girl like kwa wingi
 
Wanabodi,
Sisi binadamu tofauti tofauti tuna hobies mbalimbali, wengine wanapenda kutulia sehemu moja, wengine wanapenda kusafiri safiri, mimi napenda sana kusafiri, na napenda kula. Kila nikisafiri, mahali popote hupendelea sana kula the local foods za mahali hapo!.

Vyakula tofauti tofauti vina tastes tofauti tofauti, kuna vyakula kwa kuvitazama kwa macho unaviona they look good hivyo ukila utafaidi lakini unapokula unakuta ni tasteless!, na kuna vyakula kusema ukweli ukitazama machoni kama zile nyama
Mbute hazina mfano wake
 
Wanabodi,

Sisi binadamu tofauti tofauti tuna hobies mbalimbali, wengine wanapenda kutulia sehemu moja, wengine wanapenda kusafiri safiri, mimi napenda sana kusafiri, na napenda kula. Kila nikisafiri mahali popote hupendelea sana kula the local foods za mahali hapo.

Vyakula tofauti tofauti vina tastes tofauti tofauti, kuna vyakula kwa kuvitazama kwa macho unaviona they look good hivyo ukila utafaidi lakini unapokula unakuta ni tasteless, na kuna vyakula kusema ukweli ukitazama machoni kama zile nyama za mnadani, they don't look so good au mazingira kama ya kwa Mromboo pale Arusha, mazingira ni horrible fulani but the meat is so tasty.

Wewe unaweza kukumbuka baadhi ya vyakula ulivyokula vya makabila, jamii, na mataifa mbalimbali? Vipi ulifaidi, ukikumbuka unajisikia raha?

Kwa upande wangu nimewahi kula vyakula vya makabila haya, jamii hizi na mataifa haya;
  • Moshi Wachagga wa Kirua Vunjo​
  • Moshi Machame​
  • Moshi Kibosho​
  • Moshi Siha​
  • Moshi Wapare​
  • Arusha Waarusha​
  • Arusha Wameru​
  • Arusha Wamasai​
  • Babati Wambulu​
  • Singida Wanyaturu​
  • Singida Wanyiramba​
  • Dodoma Wagogo​
  • Morogoro Wapogoro​
  • Morogoro Waluguru​
  • Morogoro Wakaguru​
  • Pwani Wadengereko​
  • Dar es Salaam, Wazaramo​
  • Iringa Wahehe​
  • Iriga wabena​
  • Iringa Wakinga​
  • Mbeya Wanyakyusa​
  • Songea Wangoni​
  • Songea Wanyasa​
  • Tanga Wasambaa​
  • Tanga Wadigo​
  • Tanga Wabondei​
  • Bukoba Wahaya​
  • Bukoba Wahangaza​
  • Lindi Wamachinga​
  • Mtwara Wamakonde​
  • Musoma Wajita​
  • Tarime Wakurya​
  • Ukwerewe Wakerewe​
  • Mwanza Wasukuma​
  • Tabora Wanyawezi​
  • Zanzibar Wazanzibari​
  • Pemba Wapemba​
  • Mafia Wamafya​
  • Kigoma Waha​
  • Kenya Wakikuyu​
  • Kenya Wakamba​
  • Uganda Watoro​
  • Uganda Waganda​
  • Uganda Wanyankole​
  • Rwanda Wanyarwanda​
  • Burundi Warundi​
  • Zambia Wazambia​
  • Malawi Wamalawi​
  • Msimbiji Wasumbiji​
  • Angola wa Mulato​
  • Swaziland Wazwazi​
  • Lesotho Wasotho​
  • South Africa Wazulu​
  • South Africa Wakhosa​
  • South Africa Africans​
  • Zimbabwe wa Matebele​
  • Malawi Wamaawi​
  • Congo Wakongo​
  • Ghana Waghana​
  • Liberia wa Liberia​
  • Cote d'ivoire Wakote​
  • Ethiopia Wahabeshi​
  • Sudan ya Kusini Wasudani​
  • Somalia Wasomali​
  • UK Waingereza​
  • US Waamerica​
  • Swiss Wa Swiss​
  • Italy Wataliano​
  • Sweden wa Swedish​
  • Norway wa Norwegians​
  • Finland wa Fini​
  • Germany Wajerumani​
  • Poland wa Polish,​
  • Canada wa Canadian​
  • India Wahindu​
  • Russia Warusi​
  • China Wachina​
  • Japan Wajapan.​
Ukisafiri ukifika popote ukalala hata usiku mmoja, hakikisha usiishie kula vyakula vya hotel, toka, walk around, grab a local taxi, madereva taxi wanajua wapi you can get a local tasty meal, kama unapenda kula kila ukisafiri hakikisha you feast the taste.

Leo tumeanza Kwaresma, baada ya Kwaresma nitarejea kwenye uzi huu niwape mastori wapi ni kitamu na nilifaidi.

Kwa leo nawatakia Kwaresma njema.

Paskali
Wengine tupo sensitive sana na vyakula.

Roho ikikataa unaachana nacho.
 
Chakula cha wa Eritrea chapati hiyo ni kubwa ina kuwa sour alafu inawekwa kwa sinia then juu yake ndio linamwagiwa hilo limboga la kulia. Jamani hiyo kitu ni taaaaamu. Inawekwa na pilipili ya kutosha. Saa ya kula mnakaa chini then u share. Wote mnalia kwenye kile kisinia. I used to date an Eritrean guy while i was living in Nairobi akawa ananipeleka mahali panaitwa Hurlingam ndio Eritreans wengi huishi huko na wana restaurants pia.

Ilikuwa akinipeleka huko tukirudi kwa apartment yani nampa kila kitu 😆😜
 
Chakula cha wa Eritrea chapati hiyo ni kubwa ina kuwa sour alafu inawekwa kwa sinia then juu yake ndio linamwagiwa hilo limboga la kulia. Jamani hiyo kitu ni taaaaamu. Inawekwa na pilipili ya kutosha. Saa ya kula mnakaa chini then u share. Wote mnalia kwenye kile kisinia. I used to date an Eritrean guy while i was living in Nairobi akawa ananipeleka mahali panaitwa Hurlingam ndio Eritreans wengi huishi huko na wana restaurants pia.

Ilikuwa akinipeleka huko tukirudi kwa apartment yani nampa kila kitu
Yaani Kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakula cha wa Eritrea chapati hiyo ni kubwa ina kuwa sour alafu inawekwa kwa sinia then juu yake ndio linamwagiwa hilo limboga la kulia. Jamani hiyo kitu ni taaaaamu. Inawekwa na pilipili ya kutosha. Saa ya kula mnakaa chini then u share. Wote mnalia kwenye kile kisinia. I used to date an Eritrean guy while i was living in Nairobi akawa ananipeleka mahali panaitwa Hurlingam ndio Eritreans wengi huishi huko na wana restaurants pia.

Ilikuwa akinipeleka huko tukirudi kwa apartment yani nampa kila kitu 😆😜
Mpaka mtandao pendwa?
 
Niki read between the line na was was na chakula na hisi ni kile chakula kingine maana mtoa mada ni bingwa la fasihi , na sifa ya fanani wa fasihi ni kuongea asichomaanisha and beyond
 
Back
Top Bottom